REAL ACTIVIST
Member
- Dec 2, 2012
- 39
- 5
Mheshimiwa waziri wa elimu Dk.Shukuru Kawambwa naomba utambue tu kuwa jamii yote ya watanzania wakiwemo wasomi kama wewe inafahamu kuwa wewe ndiye waziri mwenye dhamana ya kuhakikisha gurudumu la maendeleo katika sekta ya elimu hapa Tanzania linazunguruka na kato huwezi kuliacha likalegalega na mwishowe likasimama.Sasa basi kama hivyo ndivyo,nadhani mheshimiwa waziri hutawaacha wanafunzi wa UDOM waliokuwa wamesimamishwa masomo na sasa wamerejeshwa masomoni aidha wafe njaa au mwisho wa siku wajepata shahada zenye viwango vya kuchechemea kwasababu ya kutopewa pesa za kujikimu kwa wakati muafaka kwa kufuata mujibu wa sheria na talatibu zilizoainishwa kwenye sera ya serikali ya elimu ya juu.Mheshimiwa waziri wa elimu,naamini hakuna usichokifahamu kuhusiana na wanafunzi hawa wa UDOM ambao wamerejeshwa masomoni baada ya kusimamishwa taangia mwaka wa jana.Mheshimiwa waziri wa elimu naomba ulitazame suala la wanafunzi hawa kwa upana na urefu ili kuwanusuru na maisha magumu wanayokumbana nayo kwa sasa kwani hawajapewa pesa za kujikimu taangia mwezi wa oktoba mpaka sasa.kwakuwa mheshimiwa waziri ni mwajibikaji katika wizara yako naamini utasikia hiki kilio cha hawa wanafunzi wahanga wa UDOM,Mungu ibariki UDOM,Mungu ibariki Tanzania Ameeeen.Naomba kuwasilisha.