Wizara ya elimu imetangaza kuwa masomo katika shule za kutwa zilizokuwa zimefungwa leo katika kaunti za Nairobi, Kisumu na Mombasa yatarejelewa kesho Alhamisi.
Awali Serikali ilitangaza kufunga shule hizo kutokana na vuguvugu la maandamano linaloshuhudiwa nchini lakini sasa imeeleza kuwa utulivu umerejea.
Ikumbukwe Upinzani umepanga kufanya maandamano ya siku tatu mfululizo.