Tetesi: Shule Maalum kufunguliwa Bukoba kumuenzi Ruge Mutahaba

Tetesi: Shule Maalum kufunguliwa Bukoba kumuenzi Ruge Mutahaba

Nelson Masaduki

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2017
Posts
346
Reaction score
380
Watanzania wenzangu,

Nimefurahishwa na wazo lililotolewa Bukoba kuwa, itaanzishwa shule maalum ili kumuenzi Ruge Mutahaba. Tangu alipopumzishwa ndugu yetu Ruge Mutahaba, watu wengi wametoa yaliyomo mioyoni mwao na kuthibitisha kuwa, licha ya Ruge kuwa ni mtu wa kawaida katika masuala ya sanaa, burudani na tasnia ya habari - Kijana huyo alikuwa ni kiungo mzuri katika kuwasaidia vijana kuziona fursa. Fursa ni moja ya maneno ambayo aliyatumia vizuri katika kuwajengea uwezo vijana kuona namna wanavyoweza kupata fedha ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Nadhani hatua hiyo ni ya kuungwa mkono na juhudi za Maprofesa walioko Bukoba zitasaidia kuiweka taasisi hiyo katika ubora unaotakiwa. Mungu ibariki Tanzania,

Nelson,
Geita
 
Whenever the opportunity is the optimistic gathered
 
Back
Top Bottom