Wakuu, natafuta shule ya sekondari kwa mtoto wa kike, ambayo wanafunza maadili mema na kusaidia kurekebisha tabia. Naomba msaada kwa mwenye kujua shule za namna kama zipo Tanzania. Imekuwa changamoto kumwadhibu mtoto, inaweza kuleta balaa, hivyo naamini kuna watu wenye taaluma hizo. Angalizo, shule hizo zisiwe zile za kupeleka watoto waliofungwa na mahakama. Natafuta, shule wenye uzoefu wa kurekebisha tabia na kuwapa maadili mema.
Tafadhali nawalisha.
Kivosho girls nakataaa katakata,,,,yaani binti wa jirani aliondoka mzuri wa tabia ila huko kulimuharibu balaa,,,kama una pesa na upstairs yuko fresh mfungulie biashara,,akijishtukia ataomba kusoma mwenyewe,,,