Shule ya CCM Ivumwe Mbeya Yamwangukia Rais Samia Ujenzi wa Miundombinu

Shule ya CCM Ivumwe Mbeya Yamwangukia Rais Samia Ujenzi wa Miundombinu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SHULE YA CCM MBEYA YAMUOMBA RAIS SAMIA TZS 40 MILIONI KUKAMILISHA UJENZI WA MAABARA

Uongozi wa Shule ya Sekondari Ivumwe, inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia Sh milioni 40 kukamilisha ujenzi wa maabara tatu mpya na za kisasa.

Shule hiyo inamilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imekuwa ikipata matokeo mazuri kitaaluma.

Akizungumza Januari 1, 2025, Mkuu wa Shule hiyo, Oscar Mwaihabi, amesema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma lakini inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu, hususan maabara.

Mwalimu wa masomo ya sayansi, Mrisho Mbombwe, amesema kukosekana kwa maabara kunarudisha nyuma maendeleo ya wanafunzi kwa kuwaelimisha kwa nadharia pekee badala ya vitendo.

Upande wake, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Mbeya, Abdul Komba, ameahidi kulifikisha ombi hilo kwenye kamati ya siasa ya chama ili kuhakikisha mwaka 2025 unakuwa wa mafanikio.

Shule ya Sekondari Ivumwe, inayotoa elimu kwa kidato cha kwanza hadi cha sita, inamilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa CCM, ambayo Mwenyekiti wake ni Rais Samia Suluhu Hassan.
 

Attachments

  • y2mate.com - SHULE YA CCM MBEYA YAMUOMBA RAIS SAMIA SH40 MILIONI KUKAMILISHA UJENZI MAABARA_360p.mp4
    20.2 MB
  • Screenshot 2025-01-03 at 21-38-11 Shule ya Ivumwe Mbeya yamwangukia Rais Samia ujenzi wa miund...png
    Screenshot 2025-01-03 at 21-38-11 Shule ya Ivumwe Mbeya yamwangukia Rais Samia ujenzi wa miund...png
    1.1 MB · Views: 3
hizi shule za jumuiya ya wazazi nafikiri zimulikwe kwa kuboreshwa vizuri kwani zinamaneo makubwa na zinaweza kutumika vizuri zaidi kuliko sasa
 
Back
Top Bottom