Shule ya kwanza Tanzania

Umbee,
Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu
kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.

Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa
mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma.

Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.

Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani
na makarani katika serikalini yao.

Wamisionari na wakoloni walishangazwa na ustaarabu huu na maendeleo
haya waliyoyakuta.

Hawa walikuja kustaarabisha watu ''washenzi'' badala yake wamewakuta
watu waliostaarabika na wenye utamaduni wa kupendeza na mfumo wao
wa elimu.
 
Usitukane wazee wetu... Ina maana kabla ya kujengwa jengo hilo ilikua hakukua na mahala pa kusoma watoto na kabla ya hapo ilikua wazee wetu hawajui kusoma na kuandika.lazima tujielewe na tujiheshimu hao wakoloni waliweza tawala nchi zetu lakini wasitawale akili zetu.
 
First Government secondary school,siyo First School
 
Kabla ya hapo zilikuwepo shule zilizo jengwa na waarabu , (tanga mjini,bagamoyo na mafia)kwa wadau wa historia hio sio shule ya kwanza.
 
Ule mtaa wa magila pale k'koo ndo jina la kuenzi huo mlima?
 
Iko Tanga hii.Shule ya kwanza ya secondary kabila ya Uhuru ni Old Tanga,iko Tanga na baada ya Uhuru ni hiyo Tanga School

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…