DOKEZO Shule ya Msingi Kambarage - Dodoma haina Ofisi ya Mwalimu Mkuu na Walimu wengine, wanabanana kwenye chumba kidogo

DOKEZO Shule ya Msingi Kambarage - Dodoma haina Ofisi ya Mwalimu Mkuu na Walimu wengine, wanabanana kwenye chumba kidogo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mzee wa Code

Member
Joined
Sep 23, 2024
Posts
61
Reaction score
91
Kati ya mambo yanastaajabisha nchi hii ni viongozi kuendekeza mambo yasikuwa na tija kwa wananchi na jamii, Serikali imeshindwa kujenga jengo la Ofisi ya Mwalimu Mkuu na Waalimu katika Shule ya Kambarage inayopatika ndani hya Jiji la Dodoma maeneo Vyeyula.

Shule hii yenye Walimu 12, wanarundikana katika ofisi yenye vyumba viwili, kachumba chenyewe kina dirisha moja na mlango mmoja.

Viongozi wa nchini hii sijui uwa wanafikiria kwa namna gani? Kweli Shule inakosa Ofisi ya Waalimu huku mnatoa pesa kwa ajili ya mambo yasiyokuwa na tija?

Mamlaka za Jiji la Dodoma katimizeni wajibu wenu Shule ya Kambarage kwa kuwajengea Ofisi Walimu, ni jambo embalo lipo ndani ya uwezo wenu.

Mbunge Dodoma Mjini, Antony Mavunde kutwa unadhamini mashindano ya mpira ya ndondo lakini miundombinu ya Shule ambayo itakuja kuzalisha wanataaluma wengi na hao wanamichezo mmeitupa.

Soma Pia: Shule ya Msingi Mazengo Makang'wa (Dodoma) Wanafunzi wanafukuzwa na kulimishwa mashamba ya Walimu kwa kutolipa hela ya taaluma

photo_2024-10-07_16-56-17.jpg

photo_2024-10-07_17-15-53.jpg

photo_2024-10-07_16-45-58.jpg


 
Back
Top Bottom