KERO Shule ya Msingi Mazengo Makang'wa (Dodoma) Wanafunzi wanafukuzwa na kulimishwa mashamba ya Walimu kwa kutolipa hela ya taaluma

KERO Shule ya Msingi Mazengo Makang'wa (Dodoma) Wanafunzi wanafukuzwa na kulimishwa mashamba ya Walimu kwa kutolipa hela ya taaluma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Licha taarifa ya baadhi ya viongozi wa Serikali ngazi za juu kusisitiza Wanafunzi wa Shule za Serikali wasirejeshwe nyumbani kutokana na kukosa kuchangia michango, hali ni tofauti kwenye ya Shule Msingi Mazengo Makang'wa iliyopo Kata ya Makang'wa Wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma.

Wanafunzi wengi ambao hawajachangia mchango uliopewa jina "pesa ya taaluma" wanafukuzwa kila mara kutokana kutokana na kutokamilisha pesa hiyo.

IMG-20150703-WA0098.jpg

Shule hiyo imeweka kiwango cha Tsh. 8500/= ambacho kila Mwanafunzi anatakiwa kuchangia kila muhula wa masomo, kama pesa ya taaluma.

Lakini kuna jambo la kusikitisha zaidi, ambapo baadhi ya Wanafunzi ambao wamekuwa wakikosa kuchangia mchango huo wanalimishwa kwenye mashamba binafsi ya baadhi ya Walimu walipo kwenye shule hiyo muda wa masomo.

Inashangaza sana Watoto wanatoka shuleni wamechakaa baada ya kufuatilia nikagundua kumbe wanapelekwa kwenye mashamba binafsi ya Walimu, ikiwemo mashamba ya mtama, alizeti na mazao mengine kisa hawajalipa michango hivyo hiyo ndio inakuwa kama adhabu mbadala endapo hiyo siku wameamua kutowafukuza au wale ambao wamechangia kiasi.

Wazazi tumeshapeleka malalamiko yetu shuleni lakini Uongozi wa Shule umepuuza, badala yake Watoto wanaendelea kunyanyasika kila siku kwa kukosa haki yao muhimu ya kusoma, asubuhi wakiondoka baada ya saa unaona wanarejea tena nyumbani.

IMG-20150703-WA0061.jpg
Imefikia hatua kuna muda Watoto wengine wakitoka nyumbani hawifiki shuleni kwa kuhofia adhabu ya kuchapwa na kupelekwa kulima au kufukuzwa jambo ambalo sio sahihi na kwa hali ilivyo linaloweze kupelekea baadhi ya watoto kuacha Shule au kukabiliwa na ukatili kutokana na kuwa maeneo yasiyo rasmi muda wa masomo kufuatia hofu waliojengewa.

Sasa Wazazi tunajiuliza hivi kweli hao Walimu wanawajibika kwa Serikali ipi, kama wameshindwa kuzingatia maelekezo ya viongozi wa Serikali, lakini pia tunajiuliza kwanini maelekezo ya Serikali yashindwe kuchukuliwa kwa uzito na hao Watumishi.

Kwa tulipofikia tunadhani mamlaka za ndani ya Wilaya zimeshindwa kufuatilia kinachoendelea kwenye maeneo yao, sasa tunaomba viongozi wa ngazi za juu akiwemo Waziri wa Elimu, Waziri wa TAMISEMI walifuatilie suala hili ambalo Wazazi linatupa mkanganyiko kwa sababu baadhi ya Walimu wamekuwa wakiwaambia Wanafunzi na sisi Wazazi tunaofika kufuatilia suala hilo kuwa "Hakuna cha bure".

IMG_20240814_100032_772.jpg

 
Swala kama ili sio dodoma tu sehemu nyingi wanafanya ivi kama hapa daa utasikia anatakiwa aende na era ya ulinzi
 
Back
Top Bottom