Shule ya Msingi Mbuyuni-Morogoro: Mwalimu awalaghai wanafunzi wake

Shule ya Msingi Mbuyuni-Morogoro: Mwalimu awalaghai wanafunzi wake

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
25,225
Reaction score
25,488
Habari nilizozipata hivi punde ila hazijadhibitishwa ni kuwa kuna mwalimu mmoja wa shule ya msingi Mbuyuni , mtaa wa Magulumbasi ulioko Manispaa ya Morogoro (jina ninalihifadhi mpaka ushahidi utakapo patikana), ambaye anafundisha somo linalo'husisha' kuchora kwa kutumia kalamu ya risasi/penseli (somo nalo kwa sasa silitaji pia) ametuhumiwa kuwalaghai wanafunzi wake shuleni hapo na kujipatia pesa kinyume na utaratibu na sheria za nchi.

Mwalimu huyo...amewaagiza wanafunzi wake kila mmoja kuleta shilingi za kitanzania mia sita (TZS.600/=) kwa ajiri ya kununua penseli na ufutio (eraser) maalumu kutoka kwake; vifaa hivyo vingetumiwa na wanafunzi kufanya mtihani wa majaribio wa Wilaya ambao atausimamia yeye. Idadi ya wanafunzi kwenye darasa husika wanafika tisini na mbili (92).

Kwa mujibu wa chanzo changu cha habari, mwalimu alikusanya fedha hizo kutoka kwa kila mwanafunzi bila hata kuwapa risiti ya manunuzi ya vifaa hivyo (siku, muda , darasa yalipofanyika malipo hayo siutaji kwa sasa). Baada ya kujiridhisha kuwa kila mwanafunzi ametoa fedha hizo , aliwapa kalamu na ufutio ambazo zimekwisha tumika...huku kalamu nyingine zikiwa hata hazijachongwa vizuri. Baadaye aliwapatia mtihani huo wa "majaribio wa Wilaya" na wakaanza kuufanya.

Baada ya wanafunzi kumaliza mtihani huo, mwali huyo aliwanyang'anya kalamu na ufutio.

Ninaendelea kufuatilia ukweli juu ya ulaghai huu nikipata ushahidi usiyo na shaka nitataja mambo yote ambayo nimeandika kuwa siyataji kwa sasa.

Rai yangu kwa walimu wote na wafanyakazi wa idara nyingine za serikali na binafsi ni kufuata maadili ya kazi zao na kuacha kabisa ulaghai kwa wale wanaowatumikia.Kama kuna yeyote anayefanya au alikuwa anapanga kufanya vitendo vinavyofanana na hivi aache mara moja.
 
Huyo mwalimu, hiyo sasa njaa ni mwanamalegeza.
Nadhani hasira za kutochaguliwa ujumbe bunge la katiba anazimalizia kwa wanafunzi ambao hawana hatia...!
 
Ulaghai wake ni upi?
Kamusi ya neno ulaghai inasemaje?
 
Inawezekana 600 ni gharama za uandaaji wa mitihani na usahihishaji mkuu
 
Inawezekana 600 ni gharama za uandaaji wa mitihani na usahihishaji mkuu

Angewaeleza ukweli wanafunzi...hata hivyo nimeahidi kufuatilia suala hili kujua ukweli hasa tena kwakupata ushahidi usiyo na shaka.
 
Ulaghai wake ni upi?
Kamusi ya neno ulaghai inasemaje?

Nimekosa Kamusi ila nimepata maelezo haya...(Jukwaa la Elimu hili)

Kiswahili ni Ulaghai, kwa kiingeraza ni fraud

Tafsiri ya kiingereza ya neno Fraudi ni :-

noun
noun: fraud; plural noun: frauds

1.
wrongful or criminal deception intended to result in financial or personal gain.

Example: "he was convicted of fraud"

[TABLE="class: vk_tbl vk_gy"]
[TR]
[TD="class: lr_dct_nyms_ttl"][/TD]
[TD]synonyms:fraudulence, sharp practice, cheating, swindling, trickery, artifice, deceit, deception, double-dealing, duplicity, treachery, chicanery, skulduggery, imposture, embezzlement;
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
acha umbea..wacha watoto wasome
 
600/= *wanafunzi 92= 55200/=.
Nakushauri usipoteze mda wako kwa kunusuru 55,200/ ambazo mwl.ametumia kufanikisha mtihani wa wilaya kwa wanafunzi 92.
Hapo kunakupiga p/copy kwa mitihani yote kwa idadi ya wanafunzi,then wafanye mazoezi ya kusiliba kwa kutumia HB2 pencil.Hiyo pesa kwanza ni ndogo sana wala usijichoshe kumsumbua mwalimu.
Kama una ubavu nenda Halmashauri ya mji uone.Gari imeenda kijijini km 30 imewekewa lita 400 za mafuta,na kwa mwezi imeenda mara 40.(huo ni mfano)
 
Mkuu acha kumfuatilia huyo mwalimu,kama mtihani ameufanikisha na wnafunzi hawakutozwa zaidi ya hiyo shs 600/=,binafsi sioni kama kuna wizi hapo,hata atakuwa amepata maji ya kunywa ambayo hayazidi shs 10,000/=.Angalia sehemu zenye ufisadi uliokithiri mkuu.
 
Unaweza sababisha mwalimu akapoteza ajira yake kwa ajili ya Ths 55,200/=.Mkuu nenda kwenye maofisi ya umma ,watu wanajiandikia masafari ya sikuu kadhaa,wanachota hela na safari zenyewe haziendwi,anaandikia report ya hiyo safari akiwa kwenye hotel na kimwana pembeni
 
umbea tu unashauri kazi za watu wakati ya kwako huiwezi? Utaandikaje kitu usichokua na uhakika nacho?
 
Tsh 55,ooo.oo ni "negligible" sana.acha mwalimu awatoe matongotongo watoto wetu.
 
ANGALIZO: Hii habari bado ni tetesi.

acha umbea..wacha watoto wasome

Nikipata ushaidi usiyo na shaka nadhani , hautatumia neno hilo

600/= *wanafunzi 92= 55200/=.
Nakushauri usipoteze mda wako kwa kunusuru 55,200/ ambazo mwl.ametumia kufanikisha mtihani wa wilaya kwa wanafunzi 92.
Hapo kunakupiga p/copy kwa mitihani yote kwa idadi ya wanafunzi,then wafanye mazoezi ya kusiliba kwa kutumia HB2 pencil.Hiyo pesa kwanza ni ndogo sana wala usijichoshe kumsumbua mwalimu.
Kama una ubavu nenda Halmashauri ya mji uone.Gari imeenda kijijini km 30 imewekewa lita 400 za mafuta,na kwa mwezi imeenda mara 40.(huo ni mfano)

1. Mwalimu alitakiwa kuwaeleza ukweli wanafunzi wake kuwa hiyo nigharama ya kuandaa na hata kusimamia mtihani...kuliko kuwalaghai kuwa anawanunulia kalamu na futio speisheli kwa ajiri ya mtihani...na baadaye anawanyang'anya. Yeye kama mwalimu ameonyesha upungufu wa weledi na uaminifu kwa wanafunzi...jambo ambalo linaathiri moral ya wanafunzi wake kwenye siku za usoni juu ya weledi, uaminifu, kiasi kuona suala la kulaghai ni suala la kawaida katika jamii...huku ni kuua moral ya kizazi kijacho na hili halikubaliki.

2. Kweli kwa kuzingatia vigezo 'ulivyovitumia'..ni pesa 'ndogo' sana...hata hivyo, udogo wa pesa hiyo siyo ruhusa ya kulagahai wanafunzi wake ...kiasi cha kuwajengia tabia za kudanganya hapo baadaye. Pia kwa mwalimu kama ameshidwa kuwa mkweli kwa pendogo hiyo je akikabithiwa pesa nyingi si ndo ataifisidi...kabisa.
3. Kitendo hiki cha mwalimu "kinatuondolea" hadhi ya kukemea maovu nchi ...kwani nisisi tunaoimiza kufanyika vitendo vya kujenga kizazi chenye kutenda maovu (ufisadi, wizi, ubinafsi wakupindukia na vingine kama hivyo). Tujenge kizazi chenye kutenda mema kwa kukemea tabia zote zenye kujenga kizazi ovu kama aliyoonyesha mwalimu.

Mkuu acha kumfuatilia huyo mwalimu,kama mtihani ameufanikisha na wnafunzi hawakutozwa zaidi ya hiyo shs 600/=,binafsi sioni kama kuna wizi hapo,hata atakuwa amepata maji ya kunywa ambayo hayazidi shs 10,000/=.Angalia sehemu zenye ufisadi uliokithiri mkuu.

Rejea majibu yote matatu hapo juu. Pia kwa nyongeza...tuanze kuondoa boriti (ufisadi mdogomdogo) zetu (sisi wananchi wa kawaida) kwanza, tukishajisafisha ndipo kwa pamoja tukemee kuondoa magogo (ufisadi mkubwa). Ni vigumu kufanikisha vita ya ufisadi mkubwa endapo nasi tunashiriki ufisadi mdogo.

Unaweza sababisha mwalimu akapoteza ajira yake kwa ajili ya Ths 55,200/=.Mkuu nenda kwenye maofisi ya umma ,watu wanajiandikia masafari ya sikuu kadhaa,wanachota hela na safari zenyewe haziendwi,anaandikia report ya hiyo safari akiwa kwenye hotel na kimwana pembeni

Rejea majibu ya hapo juu. Nyongeza...kujuana, kuoneana aibu, kuoneana huruma kwa mambo ambayo yana haribu kizazi hiki na kijacho, hakupaswi kuvumiliwa. Tuukemee wote kwa kukutenda haki kulingana na nyazifa tulizonazo.

umbea tu unashauri kazi za watu wakati ya kwako huiwezi? Utaandikaje kitu usichokua na uhakika nacho?

Rejea jibu nililompatia data

Tsh 55,ooo.oo ni "negligible" sana.acha mwalimu awatoe matongotongo watoto wetu.

Rejea majibu yote hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
kawapigie kelele akina lowasa, chenge na wezi wengine wa EPA achana na huyo teacher kwanza mshahara wa walimu mdogo..hizo ndio ration na marupurupu ya walimu km vp pga kelele mshahara wa walmu upande uone kama ataendelea
 
Lazima tujenge uhalali wa kuwapigia kelele wengine kwa kujenga moral authority, hatuwezi kuwapigia kelele wengine...wakati sisi tunafanya ama tunaunga mkono wanayofanya huku chini.....
Walimu na wafanyakazi wa kada zingine...mishahara haitoshi kulingana na gharama za maisha kwa sasa....lakini ni baadhi ya walimu hawa hawa na wafanyakazi wengine linapokuja suala la kudai haki zao hawachukui hatua stahiki kuwaunga mkono viongozi wao badala yake wanawahujumu kwa kuvujisha mikakati stahiki ya kudai haki....

Narudia hatuwezi kuondoa ufisadi nchini ikiwa na sisi tunashiriki kufanya na kupandikiza tabia za ufisadi kwa kizazi hiki na kijacho...!

Tujisafishe kwanza.
 
Back
Top Bottom