TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
Habari nilizozipata hivi punde ila hazijadhibitishwa ni kuwa kuna mwalimu mmoja wa shule ya msingi Mbuyuni , mtaa wa Magulumbasi ulioko Manispaa ya Morogoro (jina ninalihifadhi mpaka ushahidi utakapo patikana), ambaye anafundisha somo linalo'husisha' kuchora kwa kutumia kalamu ya risasi/penseli (somo nalo kwa sasa silitaji pia) ametuhumiwa kuwalaghai wanafunzi wake shuleni hapo na kujipatia pesa kinyume na utaratibu na sheria za nchi.
Mwalimu huyo...amewaagiza wanafunzi wake kila mmoja kuleta shilingi za kitanzania mia sita (TZS.600/=) kwa ajiri ya kununua penseli na ufutio (eraser) maalumu kutoka kwake; vifaa hivyo vingetumiwa na wanafunzi kufanya mtihani wa majaribio wa Wilaya ambao atausimamia yeye. Idadi ya wanafunzi kwenye darasa husika wanafika tisini na mbili (92).
Kwa mujibu wa chanzo changu cha habari, mwalimu alikusanya fedha hizo kutoka kwa kila mwanafunzi bila hata kuwapa risiti ya manunuzi ya vifaa hivyo (siku, muda , darasa yalipofanyika malipo hayo siutaji kwa sasa). Baada ya kujiridhisha kuwa kila mwanafunzi ametoa fedha hizo , aliwapa kalamu na ufutio ambazo zimekwisha tumika...huku kalamu nyingine zikiwa hata hazijachongwa vizuri. Baadaye aliwapatia mtihani huo wa "majaribio wa Wilaya" na wakaanza kuufanya.
Baada ya wanafunzi kumaliza mtihani huo, mwali huyo aliwanyang'anya kalamu na ufutio.
Ninaendelea kufuatilia ukweli juu ya ulaghai huu nikipata ushahidi usiyo na shaka nitataja mambo yote ambayo nimeandika kuwa siyataji kwa sasa.
Rai yangu kwa walimu wote na wafanyakazi wa idara nyingine za serikali na binafsi ni kufuata maadili ya kazi zao na kuacha kabisa ulaghai kwa wale wanaowatumikia.Kama kuna yeyote anayefanya au alikuwa anapanga kufanya vitendo vinavyofanana na hivi aache mara moja.