A
Anonymous
Guest
Mimi ni Mdau wa Elimu ninayeishi Goba Mpakani, Mtaa wa Tegeta A, Kata ya Goba, kuna changamoto ambayo imejitokeza ni miezi kadhaa sasa inaendelea kuwa kikwazo kwa Watoto wa Shule kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu bora.
Kuna utaratibu ambao umeanzishwa na Uongozi wa Shule ya Msingi Goba Mpakani pamoja na Shule ya Sekondari Goba Mpakani.
Shule hizi zote ni za kutwa na zinapatikana eneo la Goba Mpakani, zipo karibu sana na zinatazamana, utaratibu ulioanzishwa ni kwamba kila siku Mwanafunzi anapeleka Shuleni Shilingi 1,000, kwa ajili ya kupikiwa chakula cha mchana hapo shuleni, ambapo wanapikiwa Wali Maharage.
Sasa changamoto inayojitokeza si kila Mzazi anaweza kumudu gharama hizo kwa kila siku kumpatia mtoto wake Shilingi 1,000 na ikizingatiwa unakuta mzazi mmoja ana watoto wawili au mpaka Watatu wengine wanasoma Shule ya Msingi na mwingine anaweza akawa anasoma Sekondari.
Uongozi wa Shule unachofanya kama Mwanafunzi amekosa Shilingi 1,000 anachapwa viboko na anatakiwa kurudi nyumbani hadi atakapokuja na hela.
Hivyo, Watoto wamekuwa hawaendi shule na wanakosa vipindi sababu ya kukosa 1,000 ya kula Wali Maharage.
Uongozi wa Shule umefanya kuwa mchango wa hela ni lazima na sio ombi, bila kuangalia ni kwa kiasi gani Wanafunzi wengi wanapata athari kitaaluma kwa kushindwa kuhudhuria vipindi vya darasani kwasababu kakosa buku ya chakula.
Hili jambo kama Mdau wa Elimu naliona linadhorotesha sana juhudi zinazofanywa na Serikali Kuu kuhakikisha kila Mwanafunzi au Mtanzania anapata elimu bure na bora kwa haki bila kujali hali ya uchumi wake.
Naomba hili suala likemewe, kwa Wazazi watakaoshindwa ku-afford hizo hela Watoto wao wapate fursa sawa ya kusoma kama ilivyo kwa wengine na sio kufukuzwa kurudi nyumbani ilhali masomo yanaendelea.
Pia soma: Mchengerwa: Wanafunzi wote wa kutwa wapate chakula shuleni