DOKEZO Shule ya Msingi Shungubweni (Pwani) ni hatari kwa maisha ya watu, majengo yapo hatarini kuanguka, Vyoo navyo ni aibu tupu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hii ni Shule ya Msingi Shungubweni, ipo Tarafa na Kata ya Shungubweni, Wilaya ya Mkuranga katika Mkoa wa Pwani.

Kama inavyoonekana hapo ndani haikidhi kabisa kwa matumizi ya Wanafunzi kwa kuwa majengo yake si rafiki na yanahatarisha usalama wa watumiaji wengi wao wakiwa ni Wanafunzi na Walimu.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ameshaandika barua sehemu tofauti kwa ajili ya changamoto iliyopo katika majengo ya shule hiyo lakini hakuna hatua ambazo zimechukuliwa.

Shule hiyo ina miradi inayojitegemea ikiwemo ya Mikorosho ambayo inawawezesha kupata fedha lakini pesa za matumizi ya Shule hazijulikani zinapokwenda, Mtendaji Kata amekuwa changamoto ya fedha kutoonekana na hazijulikani zinaenda wapi.

Shule hii ipo katika Jimbo la Mbunge na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Hamis Ulega.

Kinachoendelea ni aibu kwa kweli, tazaman video hizi zinazoonesha maisha wanayopitia Wanataaluma wa shule hii, angalia ukuta, nyufa, vyoo na madarasa yalivyo.

Mbali na usalama kuwa hatarini, kiafya pia kuna uwezekano mkubwa wa kuibuka kwa magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.
 
Mama anaupiga mwingi 😃😃😃
 
Mama anaupiga mwingi 😃😃

Hakika watoto wetu wapo hatarini sana...... Kuna haja ya wahusika kuchukua hatua kwa haraka
 
Kwenye kununua mavi8 na kutumbuaa
Wako faster

Ova
 
Back
Top Bottom