Shule ya Msingi Laalakir iliyopo Kijiji cha Partimbo, Kata ya Partimbo wilayani Kiteto Mkoani Manyara, imekuwa na matokeo ya alama "A" kwa miaka 10 mfululizo na kushika nafasi ya kwanza kiwilaya na kimkoa na haijawahi kufelisha mwanafunzi
Wanafunzi waliofanya mtihani mwaka 2022 ni 36, kati ya hao 35 wamepata alama A na B mmoja.
Shule hii ilijengwa na watu wa Jamhuri ya China kati ya shule tatu zilizojengwa, Tanzania Bara na Visiwani, moja ilijengwa Kiteto Manyara, nyingine Mkoa wa Pwani na moja Zanzibar.
Hao watoto wanao pata hizo alama A wako wapi now? Kuna kitu cha upekee wanacho mtaani? Au huko waliko? Ujue siku mitihani ikifutwa ndio siku tutaanza kuwa na elimu bora,
Kwa hiyo idadi ungefelisha? Yaani 36! Sasa hapa kwetu Kuna shule private haijawahi kutoa B ni mwendo wa A tu. Lakini za serikali Kuna shule ilikua na wanafunzi 233 wamefeli 27. Idadi ya wanafunzi darasani inaathiri matokeo.