A
Anonymous
Guest
Kumekuwa na wizi wa pesa zinazokusanywa kwenye Shule za Sekondari, Tsh. 50,400/-. Wakuu wa shule wamekuwa wakikusanya pesa hizo lakini hawawapatii bima Wanafunzi hadi wanamaliza masomo yao hasa wale wa Advance (Kidato cha 5&6). Hili lipo haswa kwenye Shule ya BUGENE SEKONDARI iliyopo Mkoa wa Kagera Wilayani Karagwe.
Wanafunzi walioko Kidato cha Sita sasa hawajapewa bima zao na muda wa kuhitimu unamalizika, Taarifa zilizopo ni kwamba hata wale waliohitimu Kidato cha Sita, May - 2024 katika kipindi chao chote cha masomo hawakupewa bima.
Hii inaleta kadhia kwa Wazazi na Wanafunzi pale Mwanafunzi anapougua na kupelekwa hospitali kama vile Nyakahanga Hospital, Wazazi wanalazimika kulipia gharama za matibabu licha ya kuwa michango ya bima wameshalipia shuleni.
Viongozi wa shule hiyo wameendelea uhujumu michango hiyo kwa kuwapatia Wanafunzi Bima za Tsh. 6,000/- na hii ni baada ya wanafunzi na wazazi kulalamika.
Tunaomba serikali iingilie na kufanya uchunguzi wa jambo hili ili wahusika wote wawajibishwe, kwasababu wanafunzi wakikosa ela ya kulipia hospitali hawapewi huduma. Na michango yote iliyokusanywa irejeshwe kwa wanafunzi hata ambao wameshahitimu wapewe pesa zao.
Pia kuwekwe utaratibu mzuri wa NHIF kuwa na wawakilishi pale shuleni ili wakusanye wenyewe hiyo pesa na kuwapatia wanafunzi bima kwa wakati. Asante