Shule ya Sekondari Moi yafungwa kufuatia tuhuma za mwanafunzi kubakwa

Shule ya Sekondari Moi yafungwa kufuatia tuhuma za mwanafunzi kubakwa

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Moi2.jpg


Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi imefungwa kwa amri ya Wizara ya Elimu baada ya tuhuma za kubakwa kwa wanafunzi wakiwa shuleni hapo.

Tuhuma hizo hazijaweka wazi idadi ya waliobakwa huku Mkuu wa Polisi wa eneo shule ilipo akitoa uthibitisho wa kubakwa mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili na taarifa nyingine zikidai wamebakwa watu watatu.

Mbakaji bado hajapatikana na Wizara imetoa amri shule ifungwe kwa angalau wiki moja ili kupisha uchunguzi. Wazazi wenye hasira walionekana shuleni hapo siku ya Jumapili wakichukua watoto wao kufuatia agizo la Serikali.

Moi.jpg


Ikumbukwe kuwa miezi 8 iliyopita shule hii ilipatwa na skendo nyingine baada ya mwanafunzi kuchoma moto bweni na kusababisha kifo cha mwenzie mmoja.

Akizungumza na waandishi habari alipoizuru shule hiyo, Waziri wa elimu, Bi. Amina Mohammed amesema uchunguzi unaendelea na kwamba wataimarisha usalama shuleni na kuhakikisha kwamba watoto watasoma kama inavyotakiwa.
 
Must hav been a case of teacher student relationship
 
Naona wameendelea siku hizi wameacha kubaka mifugo yao
 
Back
Top Bottom