DOKEZO Shule ya Sekondari Ntare ina michango mingi, inatishia wanafunzi kuacha shule

DOKEZO Shule ya Sekondari Ntare ina michango mingi, inatishia wanafunzi kuacha shule

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Tunaomba mtusaidie kufuatilia na kupaza sauti. Shule ya sekondari Ntare, iliyopo Kyerwa Ina michango mingi sana ya nje ya utaratibu.

Mtoto wa kidato cha nne, wanapeleka debe 8 za mahindi, na debe 4 za maharage kwa mwaka kwa kila mtoto.

Hapo hapo wazazi wanatoa 25,000 ya uendeshaji, jana kabla wanafunzi wa kidato cha nne kuondoka na magodoro yao walimu wameyashikilia kisa mtoto hajatoa 8,000 ya mashine ya kusaga.

Hili godoro mtoto hakulilalia toka amefika yalichukuliwa wakapewa walimu wa kujitolea mtoto akawa anashare kitanda na mwenzie.

Hapo ni michango nje ya ada ya 20,000. Wazazi walilazimishwa kuchanga 100,000 ya mahafali ya form iv.
 
Tatizo walimu wanataka kuzipa viwango vya private schools, kule songea kuna shule inaitwa madaba utakoma
 
Back
Top Bottom