Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Shule ya sekondari ya Noonkopir Girls iliyoko kaunti ya Narok imewatuma nyumbani wanafunzi wote baada ya kesi za usagaji kukithiri shuleni humo.
Kwa mujibu wa ripoti zilizowasilishwa kupitia gazeti la the Star, wanafunzi hasa wanaojiunga na sekondari wamekuwa wakilalamika kwa wazazi kwamba wanapigwa na wenzao wakuu kwa kukataa kujiunga na makundi ya wasagaji shuleni humo.
Aidha wazazi wameripoti kuwa wanafunzi walipewa uhuru kupita kiasi wakati wa likizo ya Pasaka, jambo ambalo lilichochea uovu huo wikiendi iliyopita.
"Watoto wetu wameripoti kupigwa na wenzao wa kugoma kuingia makundi ya wasagaji na pindi wanaporipoti kwa Walimu hakuna lolote linalofanyika zaidi ya kuambiwa kuwa hata wasagaji wanayo haki ya kupata elimu." Alielezwa mzazi mmoja.
Mkurugenzi wa elimu katika kaunti hio ya Narok Martin Cheruiyot amesema kwa wamefungua jalada la uchunguzi, alisema madai hayo ni mazito na yanastahili kuchukuliwa kwa uzito mkubwa.
"Hili Suala ni zito kwa kweli. Hatuna budi ila kuchukua hatua stahiki kabla hali kuwa mbaya hata zaidi." Amesema Martin Cheruiyot.