Wakuu salam,
Naomba mwenye kujua shule ya sekondari (O-level) ya wasichana, yenye ghalama nafuu ya karo (walau 1.5M) na inafaurisha vizur. nina mdogo wangu nataka na yeye akasome aisee.
shukrani
Mpeleke Marian Girls ( Bagamoyo) iko vizuri sana and atafanya vizuri sana!!!
Mkuu kuna mambo ya kuzingatia! Mdogo wako kitaaluma yukoje? Maana unaweza kuta mdogo wako anapenda umiss wewe unataka awe daktari! Kama hana base nzuri hata ukutafuta hizo shule zitakugharimu tuu kununua form za kujiunga. Mind you form ziko kweye 20T and above. Walioomba 10,000 wanaochaguliwa 80 tuu. Kifupi shule zilizoko chini ya kanisa ziko vizuri lakini mkuu kizuri ni ghali! Jichanganye fasta maana wengi walishafanya interview tayari.