Kumbuka kuwa muundo wa mahakama ni Mahakama ya rufaa kama mahakama ya juu kabisa, hii ipo Dar es Salaam, ingawa hufanya vikao vyake kwenye kanda za mahakama kuu. Mahakama kuu, sharia imegawa mahakama kuu kwenye kanda, kwa sasa karibu kila mkoa ni kanda ya mahakama kuu isipokuwa mikoa ya shinyanga, kigoma, pwani, morogoro,Singida,Lindi, Mara na Manyara ( utanisamehe mikoa mipya siifahamu). mahakama ya hakimu mkazi ambazo zipo kila mkoa na mahakama ya wilaya, ambazo zipo kila wilaya ( mahakama ya wilaya na hakimu mkazi zina karibu mamlaka sawa, na chini kabisa kuna mahakama za mwanzo. Mahakama za mwanzo ndizo nyingi sana na ziko vijijini. Kwa muundo huu utaona kuwa mahakama ya mwanzo inahudumia wananchi wengi kutokana na ukweli kuwa ni mahakama ya chini na imetapakaa karibu kila mahali. Sheria hairuhusu mawakili kufanya uwakilishi kwenye mahakama za mwanzo na kwa sababu hiyo mawakili kisheria hawawezi na hawatakiwi, kisheria kuhudumu kwenye mahakama hizo.Gharama sio tatizo kwani kuna mashirika mengi yanayayotoa msaada wa bure wa kisheria kama vile NOLA, kituo cha sheria na haki za Binadamu, Chama cha wanasheria wanawake TAWLA, WILDAF na kadhalika. Sambamba na hivyo kuna paralegals ambao ni wanasheria ambao sio mawakili na wao wanajikita kutoa msaada wa kisheria bure kwa wahitaji wa huduma hiyo. Kwa misingi hiyo sioni kama kuwa na kanda za shule ya sharia ni suluhisho la tatizo.