Hivi punde tu katika kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo, Meya wa Manispaa ya Kindondoni Yusuf Mwenda, amekiri katika mahojiano na mwendeshaji wa kipindi hicho kuwa Shule ya Msingi ya Oysterbay, katika manispaa hiyo, ambayo ni shule ya umma imeanza mwaka huu kufundisha kwa lugha ya Kiingereza kuanzia darasa la kwanza baada ya kuruhusiwa na Wizara ya Elimu mwaka jana. Amesema hatua hiyo ni baada ya kuomba shule za manispaa hiyo zifundishe kwa lugha hiyo baada ya kuona wanafunzi wakiingia shule za sekondari wanafeli sana kwa kuwa wanafundishwa kwa Kiingereza wakati shule ya msingi wanafundishwa kwa Kiswahili! Lakini akakiri kuwa huo ndio mfumo wa sasa kwa Tanzania nzima na kwamba wao wameruhusiwa kuanza na shule hiyo kwa kuwa imekuwa na wanafunzi wengi wenye asili ya nje ya nchi na wangependa kufundishwa kwa lugha hiyo ya kimataifa!! Hii imekaaje wanajamvi?