Shule yafungwa kisa Kinyesi

Shule yafungwa kisa Kinyesi

Super Handsome

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2013
Posts
3,844
Reaction score
6,448
Bunda. Shule ya Msingi Kibara B, iliyoko wilayani Bunda mkoani Mara, imefungwa na wananchi kwa muda kutokana na watu wasiofahamika kujisaidia kwenye vyumba vya madarasa, hali inayohatarisha afya za wanafunzi.

Mwenyikiti wa Kijiji cha Kibara B, Mafwili Mnyaga alisema kuwa shule hiyo imefungwa kwa muda usiojulikana tangu Aprili 28.

Alisema shule hiyo, iliyoko katika Mji Mdogo wa Kibara, imefungwa na wananchi wa kijiji hicho baada ya walimu kukuta asubuhi kila chumba kimejaa vinyesi milangoni, maeneo ya nje, pamoja na vyooni.

Aidha, alisema kuwa mbali na hali hiyo, pia mashimo ya vyoo hivyo yalikutwa yamezibwa kwa vitu vigumu, huku vinyesi vingine vikiwa kwenye ndoo za maji zinazotumiwa na wanafunzi kwa ajili ya kufanyia usafi.

Alisema kuwa, baada ya walimu wa shule hiyo ambayo iko katikati ya makazi ya watu, kukuta hali hiyo kwenye kila darasa walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji hicho ambao ulichukua hatua ya kuifunga shule kwa muda.

"Baada ya kufika shuleni hapo na kufanya mkutano, wananchi waliazimia kuwaruhusu watoto warudi nyumbani na kuifunga shule hiyo kwa muda," alisema.

Aliongeza kuwa walichukua hatua hiyo kwa kuhofia watoto kuugua magonjwa yasiyofahamika kwani wanaofanya tukio hilo hulifanya usiku na pia hawajui madhumuni yao.

Tayari uongozi wa kijiji umeandika barua kwenda kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya na mkuu wa wilaya kuomba msaada na ufumbuzi wa suala hilo.

"Tumeifunga shule kwa sababu hali hii ni mbaya na tatizo hili halikuanza leo na linafanyika nyakati za usiku.

Source: Mwananchi
 
duh,. Hii kali aisee!!

Shule haina mlinzi???
 
Duh! hao waliofanya hivyo inawezekana ni watoto wasiopenda kwenda shule ila wanalazimishwa, kwahiyo wanafurahi kuona muda wote wawe nyumbani.
 
Hao waliofanya hivyo wana mavi(midimba kwa lugha yetu)kiasi gani?Shule nzima?
 
Hapo unachoma sindano katika kila kimba,chamoto watakiona,------ na kabang zao zitawasha vibaya sana wenyewe watajitokeza....
 
Inamaana mtu alipakua vyoo na kuja kumwaga shuleni? Au wanga ?
Si wangezoa wafanye fumigation halafu maisha yaendelee? Au walikuwa wanatafuta aababu?
 
Nasikia kuna dawa inaitwa mvuje, ukiitia kwenye mavi ya mtu basi mtu anaharisha
 
Bunda is in the spotlight again. From one of your MPs I can understand why the school is full of shit
 
bunda ina pepo gani jamani dr nchimbi secondary iliypo bunda mjini nayo imefungwa na wakaguzi kwa kuwa na majengo mabovu angali mkuu wa shule na uongozi mzima wa wilaya haukuona tatizo
 
Back
Top Bottom