Ukiona serikali inanunua magari ya fahari 700 wakati shule zinakosa vyakula, basi ujue kuwa kuna tatizo somewhere between serikali iliyoko madarakani na wapiga kura walioiweka serikali hiyo madarakani.
Na bado kuna mtu anatumia muda mwingi kutaka kujua ni kina nani wanaandika hapa JF badala ya kufanya bidii kulisha na kusomesha watoto walioko mashuleni.
Grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Hivi Kumbe Malisa bado ni Headmaster wa Moshi Technical? Hata akiwa Lyamungo shule ilikua ikifungwa kabla ya muda.Wakati mwingine hata holiday ilikua inarefushwa kuliko shule nyingine.Kuna kipindi shule ilikua na holiday ya miezi miwili na wiki tatu
Angalao alipohama hapo Nicholaus Burreta akawa Headmaster Mpya wa Lyamungo,mambo yalikua shwari na academic performance ilikua juu kiasi cha kuichangamsha hata Ilboru.Sasa huyu Malisa kipindi hicho sijui alikua na sababu gani.Najua serikali imezembea kwa kiasi flani lakini hata huyu Malisa ana matatizo binafsi
Mkuu Ben
Unaweza kuwa sawa ila kumbuka shule zilizofungwa ni nyingi. Tatizo ni hii shule moja imeripotiwa rasmi. Nyingine zimefungwa bila kuita waandishi wa habari. Ukiona hata waziri hajatoa tamko, na hakuna mwandishi aliyejitokeza kuhoji zaidi ya kuripoti jua ndo utaratibu wa Kitanzania ambao tumeuzoea
Mwita uko right,shule ina shamba kubwa sana la mahindi labda hali ya hewa haikuwa nzuri
Hizo karakana zilizokuwa zinazalisha sasa hivi hakuna kitu shule ina mradi wa mashine ya kusaga
Serikali pia ni ya kulaumiwa sababu hii shule ni moja ya shule yenye wanafunzi wengi mno nakumbuka kuna wakati olevel wakikuwa karibia 900 na a level walikuwa kama 50 kwa sasa naskia a level wameongezeka kuna combination 2 pcm na pcb