Shule za bweni zimenifanya niyachukie Maharagwe, nifanyaje?

Shule za bweni zimenifanya niyachukie Maharagwe, nifanyaje?

likandambwasada

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
5,402
Reaction score
6,081
Hamjambo!

Mimi ni miongoni mwa vijana waliosoma shule za boarding za serikali kuanzia kidato cha 1 hadi 6

Nilimaliza kidato cha sita mwaka 2010 (shule zote ni boys)

Kama mnavyojua tena shule za boarding za serikali maharagwe ndiyo mboga kuu inayoliwa kwa wastani wa siku 6 kwa wiki.

Hali hii imenifanya niyachukie maharagwe kiasi kwamba hata ninapokwenda mgahawani ninagoma kabisa nisiwekewe maharagwe?

Je, wataalamu wa afya, hali hii kitaalamu inatokana na nini? Nifanyaje ili niwe na hamu ya kula maharagwe?

MUHIMU: Ustaarabu muhimu katika kushauri.

Cc. Sky Eclat
 
Umekwisha iweka akili yako iamini huyapendi maharage na ukiyaona tu mwili unarespond hivyo. Chakula chochote unachokichukia ukiletewa ukiwa na njaa sana unamudu kukila. Jaribu kufunga alafu ufungue na mlo wa maharage utaona utaweza.
 
Mie sina taaluma ya ushauri wa kiafya na makulaji ila nachokuambia subiri utakapozunguka town na bahasha ya khaki kwa mwaka 1na nusu bila kazi hayo maharage utayaona matamu kama samaki changu au tasi!!!unless uwe mtoto wa kigogo unaetegemea kupachikwa mahali kiujanja ujanja.

sent from my Infinix S2 Pro using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom