SoC04 Shule za Ghorofa ndio suluhu ya upungufu wa madarasa na maeneo ya ujenzi wa majngo ya shule za sekondari

SoC04 Shule za Ghorofa ndio suluhu ya upungufu wa madarasa na maeneo ya ujenzi wa majngo ya shule za sekondari

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kayugumis

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
107
Reaction score
97
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika adhima yake ya kuleta maendeleo kwa wanachi imekua ikifanya maboresho katika sekta ya elimu msingi , sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu (Vyuo vikuu) ikiwemo kuwapa fursa watanzania wote kuweza kupata elimu ya msingi na sekondari bila malipo kupitia sera ya elimu bure kwa kufuta ada. Hatua hii ya serikali kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari zimefanya kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi katika shule zetu za msingi na sekondari hvo kuathiri mchakato wa kujifunza na kujifunza tokana na uwepo wa wanafunzi wengi kuliko miundombinu ya shule hasa madarasa, madawati, vyoo na viwanja vya michezo.

Tatizo kubwa lililo kwenye shule zetu hasa za msingi na sekondari ni wingi wa idadi ya wanafunzi ukilinganisha na idadi ya madarasa yaliopo na eneo la shule kua finyu hasa kwa shule za mjini. kwa kawaida darasa moja linatakiwa kuchukua wanafunzi wasiozidi 40 ila kwa sasa shule nyingi darasa moja linabeba wanafunzi mpaka 100 na kuzidi.

Licha ya serikali kujitahidi kuongeza idadi ya madarasa kwa kujenga madarasa mapya kupitia fedha za UVIKO-19,SEQUIP, BOOST na EP4R na pesa za hamlashauri ila bado changamoto ya upungufu wa madarasa na ukosefu wa maeneo ya kujenga madarasa maeneo ya mjini bado ipo pale pale.

Serikali imepitisha sera mpya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 pamoja na mtaala mpya kwa elimu ya sekondari. Sera hii mpya ni kwamba elimu ya msingi itaishia darasa la 6 ,hvo wanafunzi walio shule ya msingi darasa la 3 mwaka huu 2024 wataishia darasa la 6 badala ya la saba. Hvo mwaka 2027 darasa la sita na la saba ambao kwa sasa wapo darasa la nne watamaliza elimu ya msingi na kujiunga elimu ya sekondari ambapo miundombinu ya madarasa na maeneo ya kujenga madara mapya haitoshelezi hata kwa sasa.

Kwa mfano hivi sasa shule X wanamaliza kidato cha nne wanafunzi 210 ila wanaokuja kujiunga kidato cha kwanza ni zaidi ya wanafunzi 400 hvo kusababisha upungufu wa miundombinu ya kujifunzia na ufundishaji kama vile madarasa, madawati, vyoo,maabara, walimu nk. Sasa mwaka 2028 wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza watakua zaidi ya mara mbili ya uwezo wa shule kuwachukua (accomodate) tokana na uchache wa madarasa na ukosefu wa ardhi (eneo) la kujenga hayo hasa kwa shule za mjini ambazo nyingi zimejengwa kwenye makazi ya watu na viwanja vidogo ambavyo hata viwanja vya michezo vineshindwa kujenga. Kwa jiji kama Dar es Salaam ambalo lina idadi kubwa ya watu na wengi wanaishi makazi holela na shule za kata zimejengwa katika maeneo hayo holela inakua ni vigumu kujenga mdarasa mapya sababu hakuna eneo la kufanya ujenzi mpya au upanuzi, hii ina maana kwamba madarasa hayatoshi na pia eneo la kuongeza madarasa halipo.

Ili kuepukana na changamoto hii, serikali na halmashauri wa jiji, manispaa, wilaya na miji ambazo ndio wamiliki wa shule hizi za kata wanapaswa kuchukua hatua hizi zifuatazo:

1. Kuandaa, kujenga na kuziendeleza shule katika mfumo wa ghorofa na kuachana utaratibu sasa wa kujenga shule kwa kutawanya majengo ambao unahitaji eneo kubwa la ardhi.

Shule nyingi za sekondari za kata hasa zilizo mjini zimejengwa katika maeneo yasio rafiki na kwenye viwanja vidogo (vifinyu) na pia majengo yake yametawanya hvo kuchukua eneo kubwa. Ujenzi na upanuzi wa madarasa kwa shule nyingi za mjini unakumbwa na changamoto ya ukosefu wa eneo.Shule zimepakana na makazi ya watu hvo kushindwa kuruhusu upanuaji wa madarasa hvo suluisho hapo ni kujenga kwa mtindo wa ghorofa ambao unachukua eneo dogo licha ya gharama za ujenzi kua kubwa. Kufanya ujenzi wa shule za maghorofa tutakua tumepata ufumbuzi wa upungufu wa madarasa na ukosefu wa maeneo ya kujenga au kupanua shule zetu za umma. Kwa kujenga shule za ghorofa tutakua tunatumia ardhi /eneo dogo kujenga madarasa mengi na ili litawezesha kutumia maeneo yaliobakia kujenga viwanja ya michezo kama basketball,netball na mpira wa miguu. Siku hizi ukitembea shule za mjini hata zilizokua na viwanja vya michezo sa hz havipo tena bali tumejenga madarasa na bado hayatoshelezi.

2. Tokana na gharama za ujenzi wa shule za ghorofa kua kubwa tofauti na hizi za kawaida basi Halmshauri chini ya idara ya ardhi na mipango miji watengeneze ramani za ghorofa hata kama wana bajeti ya kujenga ground floor tu. Msingi wa majengo yote iwe ya ramani za ghorofa ili hapo kila bajeti inapokaa vizuri basi wanakua wanajenga floor moja baada ya nyingine kuliko kutawanya majengo kama hivi sasa. Kwa kua na ramani na msingi wa ghorofa kutaepusha ujenzi holela wa madarasa na majengo mengine katika eneo dogo.
Tunaweza kuanza na ramani za ghorofa 3-5 kisha mwaka wa kwanza tunajenga ground floor pekee,mwaka wa pili tunapandisha floor ya kwanza, mwaka wa tatu floor ya pili nk,

3. Kwa kujenga muundo wa ghorofa katika shule zetu za sekondari tutaweza kupata maeneo ya kujenga viwanja ta michezo kama ili kuwawezesha wanafunzi kushiriki na kuendeleza vipaji vyao, tofauti na sasa ambapo shule nyingi za kata hazina kabisa viwanja vya michezo maana shule zinapakana na makazi ya watu. Ukosefu wa viwanja unadumaza uwezo wa wanafunzi kushiriki katika extra curricular activites na kukuza vipaji vyao.Mwanafunzi asiyeshiriki michezo mara nyingi uwa anakua na uelewa hafifu na mzito kuelewa ukilinganisha na wale wanaoshiriki michezo.

Kwa kumalizia, ili tuweze kuendana na idadi ya wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2028 serikali inatakiwa kuchukua hatua sasa na kufanya maandalizi ili kuhakikisha pindi wanaojiunga na elimu ya upili watoto hawa wanaendana na miundombinu ya shule. Changamoto za upungufu wa madarasa na udogo wa eneo la shule hasa za mjini ziwe zimepatiwa ufumbuzi kwa kujenga shule za ghorofa ambazo hazichukii eneo kubwa na pia litazifanya shule zetu ziwe za kuvutia na kuwapa watoto utulivu wa akili na nafsi tofauti na majengo tunayoyajenga sasa hivi.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom