Shule za Msingi na Sekondari : Nyimbo Za Shule ziliishia wapi?

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
7,076
Reaction score
2,457
Wakati Baba_Enock akisoma Shule ya Msingi Rumuli/Kashasha na Shule ya Sekondari ya Ufundi Moshi/Sengerema, asubuhi kabla ya kuanza masomo kulikuwa na utaratibu wa kukusanyika wanafunzi wote na kuimba "Wimbo Wa Shule". Siku za hivi karibuni naona huu utaratibu umetoweka katika shule za msingi na sekondari. Wanafunzi wanaingia madarasani kama "ngombe wanaingia zizini"!

Inawezekana kuwa ni maendeleo, lakini hizi "nyimbo za shule" zilikuwa zinaleta sana hamasa kwa wanafunzi kuwa "watiifu" na "wawajibikaji" na pia "kuweka bidii katika masomo"!

Kwa mfano (Shule ya Sekondari ya Ufundi Moshi" tuliimba hivi:

Shule yetu Ufundi Mungu Ibariki,
Bariki wanafunzi nao Walimu,
Tupate Amani, Upendo, Umoja,
Ushirikiano nao udumu daima,

Kiitikio
Tuwe watu watii,
Tuwajibike,
Na Kuzibuni Mbinu za Kazi daima
X 2

Heshima ni muhimu kwa jumuiya,
Katika kuzibuni mbinu za kazi,
e.t.c

Skulimeti wangu Asprin anaweza kunishahihisha na kuongeza beti ya pili!

Swali: Kwanini Wizara imeamua kuua huu utaratibu?

Nawatakie Mapumziko mema ya mwisho wa mwaka na sikukuu njema ya Noeli
 
Last edited by a moderator:

Skulmet bila kupoteza muda...,.

Shule yetu ufundi Mungu ibarikiiiii
Bariki wanafunzi na waaalimuuu

Tupate amaniiii
Upendo umooooojaaa, Ushirikiano na udumuuuuu daimaaaaa

Tuwe watu watiii tuwajibikeee
Na kuzibuniiiii mbinu za kazi

Tupate amaniiii
Upendi umooojaaaa, Ushirikiano na udumuuuuu daimaaaaa

Heshima ni muhimu kwa jumuiyaaaaaa,
Katika kuzibuni mbinu za kaziiiii,
Sasa ni zamu yetu, kuinua ufundi
Katika ufanisi wa kaaaaziiiiii
Sasa ni zamu yetuuuu
kuinua ufundi katika ufanisi wa kaaaaziiiii daimaaaaaaa!!
Tuwe watu watii tuwajibikeeee
Na kuzibuni mbinu za kaziiii
Tuwe watu watii tuwajibikeeee
Na kuzibuni mbinu za kaziiii daimaaaaaa

Kwa heshima na kumbukumbu kwa:
Eugen Malale (RIP), Munuo (ze killer), Kasenge, Malisa, Futa, Mboya, Pyuza, Kileo, Msuya (Mr & Mrs), Lyimo (muzeya kemistri), Daffa (RIP) na Pande (we acha tu)

Na kwa skulmets Nasib M, Experious Kululya, Rutta R, Mangu M, Sylvia L, Vivian M,Soud A, Zacharia A, Njigula L (RIP),Shija M, Msemo Adinani Mfwangavo, Walter Mbonea, Minani Ndobewe, Mary Mushi, Martin Kinabo, Thobias Kimaro, Salvatory Mutaboyerwa, G Simbachawene, Moshi Robert et el....... Guys miss you mbaya!

Kama kuna mtu iko hapa, hebu iniPM niipemo Biya za bureeee!!

CC: Sikonge, fundi mchundo (wahandisi tumepotezeana, niaje?)
BCC: Mwita Maranya, ulikuwa umezaliwa enzi hizi?
 
Last edited by a moderator:

kwani wizara ndo inahusika na kuidhinisha hizo nyimbo mi nilifikiri mkuu wa shule ndo anahusika kwenye hilo, pia baadhi ya shule bado wanaimba hizo nyimbo
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi watoto wanashuka kwenye skuli bus wanakimbilia class. Hakuna hata kukaa mstarini na kukaguliwa soksi kama ni chafu ama zimetoboka!
 
Afu weeh Asprin, mbona mates wako wengi washa -rip? Ujue na wewe unakaribia! Andaa warithi wa wake zako.
 
Last edited by a moderator:
Afu weeh Asprin, mbona mates wako wengi washa -rip? Ujue na wewe unakaribia! Andaa warithi wa wake zako.

Rudi nyuma shetani.

Kwa hasira sitakukaribisha kwenye gradueshen ya Matesha. Ndo ukome.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja na mimi nijikumbushe wa shule yangu. Khu khu! Maaaazengo shule yetu twaipenda sana twaitakia barakaa...................
 
nimeipenda hiyo mkuu! kweli umenikumbusha mbali.

Wana Box 2 mpo naomba tukumbushane kawimbo ketu wanawane!
 
Ngoja na mimi nijikumbushe wa shule yangu. Khu khu! Maaaazengo shule yetu twaipenda sana twaitakia barakaa...................

Nimesahau ila kuna kipande kinamalizia na Elimu ni Mwanga, hapo wimbo wa shule unapigwa huku bendera ya bweni lililoshinda usafi inapandishwa kama motisha kwa wana bweni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…