Shule za serikali zianze mpango wa kuchukua wanafunzi "Private"

Shule za serikali zianze mpango wa kuchukua wanafunzi "Private"

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,346
Wadau wa elimu, kuna wazo linanijia...

Pamoja na kujengwa shule nyingi za sekondari Tanzania, bado idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba/kidato cha nne na kukosa nafasi ya kidato cha kwanza/sita ni kubwa.

Kwa kuwa wazazi wengi bado hawana uwezo wa kuwapeleka watoto hawa shule za binafsi (ambazo nyingi hutoza ada ya juu), mi napendekeza plan iwepo ya kupanua capacity ya shule "za kata" na za serikali, ili ziweze kuchukua wanafunzi wengi zaidi. Katika hili, serikali iendelee na utaratibu wa kuwadahili wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba/kidato cha nne. Hata hivyo wanafunzi ambao hawajafanikiwa kufikisha viwango vya ufaulu, lakini wana nia na uwezo wa kuendelea waruhusiwe kuomba kujiunga na shule za serikali zilizo karibu nao na zenye space, lakini watozwe ada kubwa zaidi (but realistic), ambayo strictly itatumika kuzijengea uwezo shule husika.

Ukiangalia ada inayotozwa kwa wanafunzi wa shule za serikalii kwa sasa ni ndogo na kwa kuwa serikali "haijaweza" kupeleka fedha za kutosha kwenye shule hizo, maendeleo ya huduma za kielimu kama nyumba za walimu, maabara, maktaba nk yamedumaa. Ina maana hii itakuwa fursa nzuri, sio tu ya kuwasaidia wasio na uwezo wa kwenda shule za private, bali pia kuharakisha maendeleo ya shelu zetu za sekondari...

Wadau wa elimu mnasemaje...
 
Hata hueleweki umeeambiwa public school wewe unataka ziwe private school
 
Yan kama ndani ya shule moja kuwe na aina mbili za wanafunzi?

Yan public students na private students?

Mfano Jangwani kuwe na wanafunzi walofaulu na kulipiwa na serikali na pia kuwe na wanafunzi walofeli wanajilipia wenyewe??
 
Back
Top Bottom