SoC03 Shule za vipaji maalumu

SoC03 Shule za vipaji maalumu

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Jun 5, 2019
Posts
43
Reaction score
61
Andiko langu linagusia uboreshwaji wa shule za vipaji ziwe katika vipaji vyote na sio katika uwezo wa akili darasani tu. Mathalani, kuwepo na shule za;

1. Vipaji vya sanaa kama wachongaji, wachoraji na waimbaji.

2. Shule za vipaji vya michezo kama mpira wa miguu, rugby , mpira wa kikapu, mpira wa tenisi, ndondi na riadha.

3. Shule za vipaji vya akili kwa ambao wana uwezo wa kukumbukumbu au uwezo wa masomo .

4. Shule za vipaji vya ufundi kwa ambao wana uwezo wa ubunifu na ufundi wa kuunda vifaa vya tekinolojia ya kisasa kama magari, ndege na vifaa vya umeme.



Sababu za hizi shule

1. Kutokana na janga la wasomi wengi kukosa ajira mtaani na hii ni kwa sababu ya kua wanakosa kuboreshewa vipaji vyao tangu wakiwa watoto na hivyo mpaka wanakua wakubwa wanakua hawajavitumia na hawawezi tena kuvitumia vipaji vyao katika soko la ajira.


2. Vipaji Vinatakiwa Vijengwe muda mrefu walau tangu utotoni ili wakati wowote ikitokea fursa, watoto au vijana waweze kuzichangamkia kwa urahisi na ufanisi wa hali ya juu na sio kubahatisha.

3. Shule zitasabaisha kuwepo na urahisi wa mawakala au wadau kuweza kuwafikia vijana wenye vipaji kwa urahisi na kuongeza wigo mpana wa vijana kufurahia vipaji vyao kupata ajira.

4. Shule hizi zitasaidia vijana au watoto kujengwa katika vipaji vyao kitaalamu zaidi na wakufunzi wabobevu na watoto vipaji vyao kukua katika viwango vya kimataifa.




Dhana za jamii mtaani

Jamii nyingi mtaani inaamini kua vipaji havisaidii na watoto wengi wanapaswa kupambana na elimu darasani. Jamii nyingi inapenda na kuona ufahari mtoto anapotamka na kufuata ndoto za kazi zinazotambulika kwenye jamii zetu kama udaktari, uhandisi, uhasibu , unesi, uanasheria na urubani.

Jamii haipendi kuona watoto wakisema wanataka kua wachoraji, wachongaji, wanamziki , wanariadha, wachezaji wa mpira kwa maana wanaona ni ngumu kufikia hizo ndoto kiurahisi.


Uhalisia ni kua katika nchi yetu ya Tanzania hakuna mipango mizuri ya serikali katika kutoa kipaumbele cha kuendeleza vipaji na kutafuta masoko ya vipaji vizuri vilivyoko mtaani. Hii inasababisha vijana kutumia nguvu nyingi kuonesha vipaji vyao ambavyo havina nuru katika soko la kimataifa na kufikia kupoteza muda mwingi mtaani. Vijana wengi hukata tama na kutopea kwenye uraibu wa madawa ya kulevya na uhuni.


Jamii inawaona vijana wengi mtaani wanaopambania vipaji vyao ni kama wazazi wao wamewatupa na wamekata tamaa ya maisha. Mfano vijana waimbaji kuanza kuchora michoro kwenye miili yao kujifananisha na wasanii wa nje bila kujua maadili ya kwenye jamii hayataki hayo mambo.





Nini kifanyike kwa kila aina ya shule za vipaji?

1. Shule za vipaji vya sanaa

Shule za vipaji vya sanaa zinaweza zikawa sio nyingi ila zikagawanywa makundi mawili ambayo ni shule za muziki na shule za sanaa zengine kama uchoraji , uchongaji na ufinyanzi. Shule za sanaa zitakua zinafundisha masomo ya darasani kama kawaida

Shule za muziki zitakua na masomo ya kujifunza mziki kiundani na ala mbali mbali kama namna ya kupiga gitaa, vinanda, tarumbeta na ngoma. Hii itasaidia kuongeza wataalamu wengi katika vifaa vya muziki na nchi yetu kupata wasanii wenye uwezo wa kufanya maonesho kwa ufasaha majukwaani mubashara.

Shule za sanaa za uchongaji, uchoraji n.k, zitakua zinatoa mwangaza wa kuleta uhalisia wa kazi ili zifanane na vitu vyenyewe halisi vinavyochora au kuchongwa. Kadhalika zitasaidia kujifunza namna bora ya kuwasilisha ujumbe kipekee ili kazi zao za sanaa ziwe zenye mvuto kizazi hadi kizazi.



2. Shule za vipaji vya michezo

Shule hizi zitasaidia katika sekta za michezo kupata wanamichezo walio bora na kuendana na soko la kimataifa.

Mtoto au kijana atajengwa katika shule hizi kimchezo kuanzia ulaji bora wa vyakula na mfumo mzima wa mazoezi na kupumzika kila siku.

Kupitia hizi shule itakua rahisi kwa wadau kutafuta vipaji na kuvitambulisha nje ya nchi kwa ajili ya mafanikio ya maisha ya vijana



3. Shule za vipaji vya akili

Shule hizi zitasaidia katika kuendeleza vipaji vya uwezo wa watoto wenye uelewa mpana wa masomo na kumbukumbu nzuri.

Mtoto mwenye kipaji hiki akiwa katika shule hizi serikali inatakiwa imtengenezee mazingira mazuri katika ndoto zake kama za udaktari au labda kua mtaalamu mkubwa wa sheria aweze kupata elimu kubwa katika shule bora za hapa duniani ili kupata wasomi wakubwa katika taaluma ngumu hapa duniani.



4. Shule za vipaji vya ufundi

Hapa nazungumzia shule za watoto wenye vipaji vikubwa vya kutengeneza au kuunda vifaa mbalimbali.

Mtoto akiwa katika hizi shule anatakiwa ajifunze kiundani kwa kupewa rasilimali za vifaa mbalimbali ili walau aweze kujiamini na kutengeneza vifaa vingi.

Kadhalika serikali inatakiwa iwatafutie ufadhili ili wakifika hatua nzuri kielimu waendelee kujifunza kwa shule zengine bora zaidi duniani. Baadaye tutapata wataalamu bora ambao wataweza kujiajiri wenyewe na sisi kizalishwa bidhaa bora kwa soko la ndani nabla nje.



Hitimisho

Serikali ijitahidi kuboresha vipaji katika jamii tutapunguza wimbi kubwa la vijana kumaliza kusoma na kuwaza ajira serikalini au sekta binafsi na kuongeza vijana kujiajiri wenyewe. Pia wizara ya elimu na wizara ya michezo ikae kuangalia namna bora ya kubadilisha baadhi ya shule kua za vipaji maalumu na kujenga shule zengine ili kuongeza watoto wengi kunufaika na huu mpango.
 
Upvote 6
Wazo zuri Sana Ila kwa Karne hii, tz hayo yatabaki kuwa story , bado access to education ni shida ,serikali haitaki kucommit serious Hela towards education , bado tupo mbali kufikia progressive education
 
Wazo zuri Sana Ila kwa Karne hii, tz hayo yatabaki kuwa story , bado access to education ni shida ,serikali haitaki kucommit serious Hela towards education , bado tupo mbali kufikia progressive education
Ni kweli ila kazi yetu kama wadau na wananchi tunao itakia mema serikali yetu na ustawi mzuri wa jamii yetu ni kushauri na kushauri zaidi. Yamkini katika haya tunayo shauri serikali ikayafanyia kazi mawazo yetu yote au baadhi..
 
Back
Top Bottom