Shule zetu za msingi na mishahara minono ya wabunge, mawaziri - ni aibu.

Shule zetu za msingi na mishahara minono ya wabunge, mawaziri - ni aibu.

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Posts
3,359
Reaction score
702
Jamani pamoja na hali halisi ya shule zetu za msingi kama picha inayo onyesha hapo chini, bado wabunge wetu wanalipana mshahara wa mwezi milioni 7 bila kodi, mshahara ambao unaweza kujenga darasa moja likaisha. Picha hii inaonyesha Wanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Bombo Mtoni iliyopo Kata ya Mashewa Wilayani Korogwe, Tanga wakimsikiliza mwalimu wao.

WANAFUNZI12.jpg

Inasemekana darasa hili huweza kuchukua wanafunzi wa darasa la nne 45 kwa wakati mmoja.

source: Majira ya leo
 
Last edited:
People might claim that we are coming together as human beings. But the reality is, some of decision makers (elites) in Tanzania are monster. You dont need someone to tell, just look at the photos to make a judgement of yours.
 
Tunawezaje kusanya picha za namna hii na kuziweka wazi mbele ya watanzania wote ili wajue what is going on?
Inaweza tengenezwa kama newsletter au kitu kama flier yenye picha hizi wakasambaziwa watanzania wote na kuambiwa jinsi wenzao wanavyokula uhondo wakati wana wao wakitaabika?
 
Jamani pamoja na hali halisi ya shule zetu za msingi kama picha inayo onyesha hapo chini, bado wabunge wetu wanalipana mshahara wa mwezi milioni 7 bila kodi, mshahara ambao unaweza kujenga darasa moja likaisha. Picha hii imechukuliwa katika wilaya ya Bombo, Tanga.

WANAFUNZI12.jpg

Inasemekana darasa hili huweza kuchukua wanafunzi wa darasa la nne 45 kwa wakati mmoja.

source: Majira ya leo

Mkuu tuweke mambo sawa. Hakuna wilaya Bombo katika mkoa wa Tanga. Kuna eneo la Bombo katika jiji la Tanga ambalo ndipo iko hospitali ya mkoa. Pia kuna tarafa ya Mombo katika wilaya ya Korogwe.
 
Yaani inasikitisha sana na hao hao wanainchi wamewakumbatia wabunge wao kama Miungu licha ya kuwa na sababu wazi kuwa wabunge wanaonekana kipindi cha uchaguzi na ziara ya viongozi vigogo kwenye majimbo hayo.
 
Mkuu tuweke mambo sawa. Hakuna wilaya Bombo katika mkoa wa Tanga. Kuna eneo la Bombo katika jiji la Tanga ambalo ndipo iko hospitali ya mkoa. Pia kuna tarafa ya Mombo katika wilaya ya Korogwe.

Asante kwa kunisahihisha nili-rush kidogo ktk kuandika hii issue kutoka kwenye gazeti, asante.
 
Hivi unajua inatisha, watanzania wenzetu na serikali yetu hii,hii ya tanzania! Tunaomba Tuwe na huruma kuangalia maeneo kama haya. Hivi wahusika wakuu wa wilaya hii wapo au wapo kwa jina tu. Tunaomba serikali iliangalie sana swala hili na ilitendee kazi.

Kama wahusika wa wilaya hii wapo lakini wanashindwa kutekeleza majukumu ya kazi zao inabidi swala hili litazamwe mara mbili na kwa jicho la Tofauti. anayehusika asipofanya kazi lazima awajibishwe kwani anachafua serikali na anachafua chama tawala.
 
Hivi unajua inatisha, watanzania wenzetu na serikali yetu hii,hii ya tanzania tunaomba Tuwe na huruma kuangalia maeneo kama haya. Hivi wahusika wakuu wa wilaya hii wapo au wapo kwa jina tu. Tunaomba serikali iliangalie sana swala hili na ilitendee kazi.

Kama wahusika wa wilaya hii wapo lakini wanashindwa kutekeleza majukumu ya kazi zao inabidi swala hili litazamwe mara mbili na kwa jicho la Tofauti. anayehusika asipofanya kazi lazima awajibishwe kwani anachafua serikali na anachafua chama tawala.

Mkuu naheshimu maoni yako ila katika serikali yetu hii sioni mtu wa kumwajibisha kiongozi asiyetekeleza wajibu wake. Labda Mnari tu ndiye alijaribu lakini naye aliishia kukiona cha moto. Usanii unaoendelea unahitaji nguvu kutoka nje ya mfumo wa utawala ili kusaidia wananchi kuamka usingizini na kudai huduma bora kwa kuwa wanalipa kodi. Vinginevyo hapo panaweza kuwa kituo cha kupigia kura 2010 na chama tawala kikashinda kwa 99%.
 
Mkuu tuweke mambo sawa. Hakuna wilaya Bombo katika mkoa wa Tanga. Kuna eneo la Bombo katika jiji la Tanga ambalo ndipo iko hospitali ya mkoa. Pia kuna tarafa ya Mombo katika wilaya ya Korogwe.

nadhani nimekwisha sahihisha makosa kwenye thread yangu, asante.
 
Back
Top Bottom