People might claim that we are coming together as human beings. But the reality is, some of decision makers (elites) in Tanzania are monster. You dont need someone to tell, just look at the photos to make a judgement of yours.
Jamani pamoja na hali halisi ya shule zetu za msingi kama picha inayo onyesha hapo chini, bado wabunge wetu wanalipana mshahara wa mwezi milioni 7 bila kodi, mshahara ambao unaweza kujenga darasa moja likaisha. Picha hii imechukuliwa katika wilaya ya Bombo, Tanga.
Inasemekana darasa hili huweza kuchukua wanafunzi wa darasa la nne 45 kwa wakati mmoja.
source: Majira ya leo
Mkuu tuweke mambo sawa. Hakuna wilaya Bombo katika mkoa wa Tanga. Kuna eneo la Bombo katika jiji la Tanga ambalo ndipo iko hospitali ya mkoa. Pia kuna tarafa ya Mombo katika wilaya ya Korogwe.
Hivi unajua inatisha, watanzania wenzetu na serikali yetu hii,hii ya tanzania tunaomba Tuwe na huruma kuangalia maeneo kama haya. Hivi wahusika wakuu wa wilaya hii wapo au wapo kwa jina tu. Tunaomba serikali iliangalie sana swala hili na ilitendee kazi.
Kama wahusika wa wilaya hii wapo lakini wanashindwa kutekeleza majukumu ya kazi zao inabidi swala hili litazamwe mara mbili na kwa jicho la Tofauti. anayehusika asipofanya kazi lazima awajibishwe kwani anachafua serikali na anachafua chama tawala.
Mkuu tuweke mambo sawa. Hakuna wilaya Bombo katika mkoa wa Tanga. Kuna eneo la Bombo katika jiji la Tanga ambalo ndipo iko hospitali ya mkoa. Pia kuna tarafa ya Mombo katika wilaya ya Korogwe.