Shule zetu zinazalisha waongea Kiingereza tu, hakuna critical thinking ability. Skills na competency ni zero

the power

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
407
Reaction score
799
Umenisikia na huo ndio ukweli, kuna siku nikipata nafasi nitachambua the current paradigm shift ya focus ya elimu yetu kuanzia kindergarten to Universities madhara yake tunayayaona leo na tutakayopata miaka ijayo.

Ni kweli kabisa focus ya shule zetu hasa hizi za English medium na ndizo zilizo nyingi, kwanza ni kumuwezesha mwanafunzi aweze kuandika na kuongea Kiingereza vizuri ili wazazi wafurahi, na cha pili ni kumkalilisha day and night huyu mwanafunzi aweze kumeza na kujua namna ya kujibu maswali ya mitihani ya mwisho ili shule ipate ufaulu mzuri, mwisho wa siku kuweza kuenroll wanafunzi wengi, ni biashara tu.

Contrary, shule zetu zilitakiwa kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri (critical thinking ability) ,kuwajengea wanafunzi uwezo wa kupambanua mambo na kuwa na uwezo wa kusolve issues na problems tunazokutana nazo katika jamii.

Ni kweli ukisikiliza kizazi cha sasa jinsi wanavyojenga hoja unaweza ukazimia; ofcourse ni wazuri kwenye hoja za mipira, betting na muziki, vitu vya kawaida kabisa. Kibaya huo uwezo mdogo unaonekana hata kwenye interviews ambayo mara nyingi ni entry point ya employment au kwenye kunegotiate terms za business ambayo ni entry point ya kubargain na kugain profits. Kwa uzoefu wangu interviewees wengi wana uwezo mzuri wa kuongea kiingereza kizuri tena cha Queen Elizabeth naongelea wale wa english medium na international schools, lakini content hakuna kabisa, ukiwapima their skills na competency zao ni zero, ni watupu kabisaaa.

Remember, employers care about the content and depth of your knowledge and understanding , they care about your skills and competency level, uwezo wa kuongea lugha nzuri ni kigezo cha mwisho labda kwenye journalism hata huko thinking na knowledge is still critical. Hata kwenye business we care about your critical thinking and your ability to negotiate terms and solving expected business challenges to maximize the profits.

Ni wakati sasa education system yetu iweze kufocus kubuild critical thinking, skills and competency ya watoto wetu ili kutoa vijana watakao peleka uchumi wetu kwenye hatua nyingine la sivyo kuna mtu alisema tutakuja kutawaliwa siku moja.

Wajibu huu ni wajibu wa Serikali, kuna vitu serikali inaweza kuviachia free market iweze kudetermine the direction lakini vingine lazima viwe controlled kama hili la elimu. Kuacha soko liendeshe elimu yetu ni sawa na kujichimbia kaburi sisi wenyewe.
 
Hapa ndio umeandika nn sasa

USSR
 
Hapa ndio umeandika nn sasa

USSR
Uwezo wako utakuwa ni mdogo sana kama hujaweza kuelewa nilichoandika. Na sina jinsi ya kukusaidia kwani inaonekana wewe ni mmoja kati ya wale victims niliokuwa nawaongelea kwenye andiko langu. Kijana aliyekwenda shule kama wewe labda mpaka university anashindwa kuelewa mada ndogo iliyo wazi kabisa, hiyo ni reflection ya poor critical thinking. Angalia hoja wanazotoa wachangiaji wengine walioelewa nilichoandika.
 
Kingereza kiwe na faida kisiwe na faida akikwepeki kwa Nchi zetu masikini.
Na mimi nimesema ni Kigezo muhimu lakini kigezo cha mwisho kwani ni lugha kama lugha nyingine, kisukuma, kihehe, kihaya ,kijaluo etc.
 
System yetu ya elimu ni kama ile ya muingereza, amerika and western Europe in general na gunduzi za kisayansi nyingi those that involve critical thinking zinatoka kwa system ya elimu kama ya kwetu. Tujiulize sisis tunakwama wapi?

Teaching /teachers ndio wabovu.Kuna concepts ambazo nilifundishwa O level na A level, zilinipa tabu sana kuzielewa. sasa naona kabisa kuwa tatizo lilikuwa kwa walimu, maana nawafundisha watoto wangu wanaelewa vema kabisa bila shida. Difficult concepts to grasp, those needing thinking in abstract, wanazielewa kirahisi.
 
WEWE NI DIVISION 5 NADHANI " VIINGEREZA" NI LUGHA YA WAPI? HILO NENO MAANA YAKE NINI?
 
Kamanda nakushauri uweze ku-focus kwenye content na mtiririko wa logic, achana na grammar, mwandiko au misamiati, hapa hatuko darasani au kwenye mitiani. cha muhimu ni je umeelewa hoja ya mandishi.
 
Language Proficiency ni kitu muhimu sana... ndio msingi wa hata hiyo Critical Thinking. Wewe kama lugha inakupiga chenga, huo uwezo wa kuchambua na kuelewa mambo critically utautoa wapi? Hizo knowledge za kukusaidia kuwa critical utazipata wapi? Kutokuwa proficient kwenye language ni moja kati ya vikwazo vya critical thinking.

Kitu kingine cha muhimu, wewe mzazi unafanya nini kumfanya mwanao awe na critical thinking?
 
Hakuna uhusiano , language proficiency ni simple sio kikwazo kwa maendeleo ya sasa ...lugha kuijua sio tatizo ila uelewa wa mtu na uwezo wa kufanya tathmini , kujifunza na utekelezaji .

Katika karne hii ambapo hata viongozi wa dunia wanatumia LAD (languagu Acquisition Device) kweny mikutano, lugha sio tatizo mbona dunia imeendelea sana , kuna vifaa vingi vya kujifunzia ...Wachina mbona wanafanya makubwa ndio maana hata yule dogo mweny IQ kubwa ni mtoto bado hata lugha za kigeni hajui na yupo Asia .

Uwezo kwa waafrica kiasili ni mdogo hata usemeje hakuna uhusiano na lugha , japo lugha ni muhimu kwa sababu ya kuweka umoja duniani kote , kirumi na kigiriki vilishakuwa kama English yao ila zama zao zimepita .

Lugha ya kingereza ni muhimu kusoma kutoka na mfumo wa elimu wa kujifunzia uliandaliwa kweny lugha hiyo katika mitaala ya kimataifa , ukisoma kwa kingereza unasoma chanzo cha asili ya elimu ya ssa ....Ni vzuri kusoma elimu kweny lugha yake ya asili haina tatizo tena bora zaidi .

Ila lugha sio tatizo .. Je , watu wanaelewa maana? wapo wazungu wanajua kingereza ila hata shule hawana maarifa .
 
Nakubaliana sana na wewe kabisa, sijajua your background kama wewe ni engeneer, daktari, fundi umeme, architecture , nurse, physiotherapist etc kama una moja ya profession hizo au nyingine utakubaliana na mimi kabisa skills na competence come first , fikiria hapo kazini kwako, mwisho wa siku performance yako inapimwa kwa unavyoongea au ulivyoweza kutumia skills na competence kuexcute your duties na kutoa matokeo.English jamani ni lugha tu kama kiswahili, kihaya , kihehe, ni muhimu ila tufocus kwenye skills na competence first.

Ila na mimi sijaignore roles ya language katika suala zima hili na nimesema, skills, competence na critical thinking come first, language nimeipa nafasi yake pia na nimesema inakuja ya nne. Hoja yangu ni kuwa shule zetu ,zimeconcentrate kwenye lugha on expense of building skills, competence na ciritical thinking, hapo ndipo naona kuna shida.

Otherwise nakubaliana na wewe kabisa kuhusu uhusiano wa language proficiency na critical thinking, upo lakini language sio determinant ya critical thinking. Kuna wazungu wengi tu wanaongea kiingereza kizuri sana ila critical thinking yao ni poor kwa hiyo unawaweka upande gani. Uhusiano ninaofikilia hapa ni kwenye lugha kusiadia muongeaji kuarticulate issues vizuri zaidi na ili uweze kuarticulate issues vizuri inategemea na uwezo wako wa kumaster the language unayotumia hapa ninarefer kwenye kiingereza..Yes nakubaliana na wewe wazazi pia wana role kubwa kushape critical thinking za watoto wao, ila muda ndio challenge.
 
Ni kwa vile dunia ya sasa imeaminishwa kwenda fika kwamba wingi na kasi ya maneno asemayo mtu humaanisha injini yake ya ubongo inachaji sawasawa.
 
Language inakusaidia kuwaelewa na watu kukuelewa, haikusaidii kufikiria. Ila ni bonus kubwa sana ku-master lugha. Mandela alipokuwa jela alijifunza Afrikana language(lugha ya Makaburu). Na akasema kabisa, bila kuelewa lugha ya mtu, ni ngumu kujua anafikiriaje.

Sio bahati mbaya kwamba Mkapa na Nyerere walikuwa critical thinkers kuliko (you know who). Wale wazee walisoma na wakasoma tena. Language profiency inakupa exposure ya critical materials za lugha hiyo.
 
Hakuna uhusiano , language proficiency ni simple sio kikwazo kwa maendeleo ya sasa ...lugha kuijua sio tatizo ila uelewa wa mtu na uwezo wa kufanya tathmini , kujifunza na utekelezaji .

Katika karne hii ambapo hata viongozi wa dunia wanatumia LAD (languagu Acquisition Device) kweny mikutano, lugha sio tatizo mbona dunia imeendelea sana , kuna vifaa vingi vya kujifunzia ...Wachina mbona wanafanya makubwa ndio maana hata yule dogo mweny IQ kubwa ni mtoto bado hata lugha za kigeni hajui na yupo Asia .

Uwezo kwa waafrica kiasili ni mdogo hata usemeje hakuna uhusiano na lugha , japo lugha ni muhimu kwa sababu ya kuweka umoja duniani kote , kirumi na kigiriki vilishakuwa kama English yao ila zama zao zimepita .

Lugha ya kingereza ni muhimu kusoma kutoka na mfumo wa elimu wa kujifunzia uliandaliwa kweny lugha hiyo katika mitaala ya kimataifa , ukisoma kwa kingereza unasoma chanzo cha asili ya elimu ya ssa ....Ni vzuri kusoma elimu kweny lugha yake ya asili haina tatizo tena bora zaidi .

Ila lugha sio tatizo .. Je , watu wanaelewa maana? wapo wazungu wanajua kingereza ila hata shule hawana maarifa .

Language ni funguo ya knowledge iliyopo kwenye hiyo lugha. The more knowledge you have, the more critical you can become.
 
Umenisikia na huo ndio ukweli, Kuna siku nikipata nafasi nitachambua the current paradigm shift ya focus ya elimu yetu kuanzia kindergarten to Universities madhara yake tunayayaona leo na tutakayopata miaka ijayo.

Ni kweli kabisa focus ya shule zetu hasa hizi za English medium na ndizo zilizo nyingi, kwanza ni kumuwezesha mwanafunzi aweze kuandika na kuongea kiingereza vizuri ili wazazi wafurahi, na cha pili ni kumkalilisha day and night huyu mwanafunzi aweze kumeza na kujua namna ya kujibu maswali ya mitihani ya mwisho ili shule ipate ufaulu mzuri, mwisho wa siku kuweza kuenroll wanafunzi wengi, ni biashara tuuuuu.

Contrary, shule zetu zilitakiwa kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri (critical thinking ability) ,kuwajengea wanafunzi uwezo wa kupambanua mambo na kuwa na uwezo wa kusolve issues na problems tunazokutana nazo katika jamii.

Ni kweli ukisikiliza kizazi cha sasa jinsi wanavyojenga hoja unaweza ukazimia; ofcourse ni wazuri kwenye hoja za mipira, betting na muziki, vitu vya kawaida kabisa. Kibaya huo uwezo mdogo unaonekana hata kwenye interviews ambayo mara nyingi ni entry point ya employment au kwenye kunegotiate terms za business ambayo ni entry point ya kubargain na kugain profits. Kwa uzoefu wangu interviewees wengi wana uwezo mzuri wa kuongea kiingereza kizuri tena cha Queen Elizabeth naongelea wale wa english medium na international schools, lakini content hakuna kabisa, ukiwapima their skills na competency zao ni zero, ni watupu kabisaaa.

Remember, employees care about the content and depth of your knowledge and understanding , they care about your skills and competency level, uwezo wa kuongea lugha nzuri ni kigezo cha mwisho labda kwenye journalism hata huko thinking na knowledge is still critical. Hata kwenye business we care about your critical thinking and your ability to negotiate terms and solving expected business challenges to maximize the profits.

Ni wakati sasa education system yetu iweze kufocus kubuild critical thinking, skills and competency ya watoto wetu ili kutoa vijana watakao peleka uchumi wetu kwenye hatua nyingine la sivyo kuna mtu alisema tutakuja kutawaliwa siku moja.

Wajibu huu ni wajibu wa Serikali, kuna vitu serikali inaweza kuviachia free market iweze kudetermine the direction lakini vingine lazima viwe controlled kama hili la elimu. Kuacha soko liendeshe elimu yetu ni sawa na kujichimbia kaburi sisi wenyewe.

Extremely sad. We don't equip our kids with globally demanded skills. Kiingereza is just one of those shits. Tunaamini katika yasiyoaminika.

If the kids have to master languages, then they must go for a combination of many different languages, including Kiswahili.
Kiingereza peke yake ni kujifunza ubabaishaji na kufikiria kuna mtu atajali.

Spain, Germany, France, Portugal, Russia, China etc have their own languages. It matters to them if you can communicate fluently in their mother tongue.
Waingereza wametuifunisha ubabaishaji na bado hatujachomoka
 
Back
Top Bottom