Shule zetu zinazalisha waongea Kiingereza tu, hakuna critical thinking ability. Skills na competency ni zero

Hilo neno kalipatia mahali pake haswa kwenye muktadha wa kile kinachojadiliwa.

Unaonekana kupwaya sana wewe.
Bora umwambie, ilibidi asome concept nzima na sentensi ilivyokaa, sentensi imekaa kiwingi nisingesema "kiingereza," na neno "viingereza" halipo au halijatumika kuelezea wingi tu bali linajaribu kufifisha umuhimu wa hiyo lugha kama tunavyofikiri ndicho kigezo cha kwanza. Nasema kufifisha kulingana na muktadha wa kinachojadiliwa. Sijasema kuondoa kabisa umuhimu wa kiingereza kwani lugha hii hahiepukiki, humu kuna vichwa vingine ni pasua kichwa. Ahhhhhhh
 
Kweli kabisa, naunga mkono hoja. Ingawa kuna sababu nyingi pia walimu ni sababu muhimu sana kwenye kueleta hii sintofahamu
 
Well said
 
Language inakusaidia kuwaelewa na watu kukuelewa, haikusaidii kufikiria.
You're being delusional. Jamii yoyote ambayo lugha yake imestawi, kwa kawaida na mafanikio yake yako juu.

Huwezi kamwe kutenganisha ubobevu wa lugha na uwezo wa kufikiri.

Never forget that we think (and eventually act) in terms of expressions called words.

Rudimentary language means crude social, political, economic and religious advancement.

The Jewish system had for very long been the best thanks to their singular dedication to Hebrew language.
 

Ndio kizazi chao kilivyo na ndio hao hao watakaokuwa makazini wakati wao watakuwa makazini wewe na kizazi chako hakitakuwa kwenye umri wa kuajiriwa.
 
Inaonekana definition ya kufikiri nayo inakupa tabu. Na pengine mada hujaielewa. The context hapa ni English language vs critical thinking. You dont need English language mastery to critically think.
 
Mkuu umenena kweli tupu.


Bora hata hizo shule, Kuna wajinga wanamaliza vyuo vikuku kwenye Kozi mbalimbali.

Asalaleeeee kile alichokisomea hawezi kabisa kukielezea, kukitumia Wala kukuweka kwenye matendo.

Utadikiaa "Nitajifunzia kazini mbele Kwa mbele".


Kwa muktadha huo, tuna kizazi Cha wafanya kazi wa kukalili, na hii inafanya ugumu wa matokeo chanya.


Wiki ilopita nmeangalia Bunge la Marekan lilivyokua linamuhoji Mkuu wa Kitengo Cha walinzi wa Rais

Aloooo Wazungu Wana akili za kuzaliwa ,yaan wanaongea Kwa kufikiriaa, Uwezo mkubwa wa upambuzinwa mambo ...

Kwa Tanzania akili za namna hii unazikuta Kwa Akina Lissu, MPINA, Nyerere, Mkapa, Mafuguli ,Mwabukusi .

Mimi najiulizaga, inakuaje mtu anajiita Msomi alafu mbumbumbu hivi??
 
Kamanda nakushauri uweze ku-focus kwenye content na mtiririko wa logic, achana na grammar, mwandiko au misamiati, hapa hatuko darasani au kwenye mitiani. cha muhimu ni je umeelewa hoja ya mandishi.
HUJUI KUWA KUNA TOFAUTI YA MAHARI NA MAHALI? NA HUJUI HATA MAANA INABADILIKA? BASI TATIZO LAKO NI KUBWA ZAIDI KULIKO NLIVYODHANI.
 
Mleta mada kama lengo lako ni kuonyesha mapungufu ya mfumo wetu wa elimu katika kujenga misingi ya maarifa, ujuzi, uelewa na weledi (knowledge, skills, competency) BASI unaharibu sana hii mada kwa kuingiza suala la Kiingereza.

Kwanza uwezo wa Kiingereza kwa wasomi wengi hapa nchini ni JANGA. Na unaendelea kudidimia. Usihangaike na shule za msingi na sekondari. Vyuoni tu hakufurahishi. Tuweke kando hili.

Kumezuka mchezo wa kuona suala la elimu kuwa ni mpambano wa Ujuzi vs Kiingereza. Watu wanajadili eti tuchague: ama tuweke mkazo kwenye kufundisha ujuzi au tuendelee kupoteza muda na Kiingereza! Hii mada nayo ina mwelekeo huo. Hilo ni kosa.

Kilicho dhahiri ni kuwa mfumo mzima wa elimu umeharibika kiasi kwamba haumuwezeshi mwanafunzi kupata ujuzi na weledi wa kitaaluma. Hata ujuzi wa lugha kwa ujumla umekuwa tatizo. Sio Kiingereza tu. Kiswahili nacho kinazidi kuwa ovyo. Hilo ndilo tatizo la kuzungumziwa na kutafutiwa ufumbuzi. Na usijidanganye kuwa Kiingereza kikiachwa basi jibu litapatikana.

Kifupi usilifanye kuwa tatizo la ujuzi vs Kiingereza. Acha wenye propaganda zao za kisiasa waendelee kudanganya wasiojielewa kuwa Kiingereza ndio tatizo.
 
Nimekuelewa kabisa mtoa hoja, ni kweli wakati wa kujadili hoja hii lazima tuwe makini kwani halikuwa lengo langu kuhusisha ujuzi, uelewa na Kiingereza. Ni ukweli kabisa masterly of language, proficiency kwenye lugha kunamuwezesha mtaalamu kuweza kuarticulate issue vizuri. Mimi nilikuwa naongelea mfumo wa sasa wa elimu jinsi unavyomislead muono wa nini cha kuconcetrate. Mimi nafikiri lugha hisiwe ndiyo kipaumbele cha kwanza, ujuzi, maarifa na competency ni priority namba moja.

Hakuna sehemu yeyote nimebeza umuhimu wa Kiingereza, Mimi ni mmoja wa victim niliyekuwa affected negetively na kutokujua kiingereza na jinsi ilivyoniathiri kimasomo O and A level pamoja na chuo kikuu.

Hata baada ya kugraduate lugha iliendelea kuniathiri kwenye efficiency ya kazi zangu ingawa nilikuwa mbishi na maanisha mikwara ya lugha ila internally nilikuwa najua nina gaps nyingi hasa kwenye grammar na pronounciation. Nakumbuka nikiwa internship nilijiapiza nitajitahidi nikachukue masomo yangu ya juu zaidi nje ya nchi na nilipigana kwelikweli,, sababu moja ni ili niweze kushape my english proficiency lakini nilitaka nipate new exposure.

For sure you cant run away from that language if you are planning to be profession in your area of focus.

Labda niseme ni kwa jinsi gani tunaweza kubalance priorities kati ya kuconcentrate kati ya lugha, skills and competency.
 
Mfumo wa Elimu nchini Tanzania umevurugwa vya kutosha kabisa na Wanasiasa katika nchi hii.
Unapaswa kubadilishwa wote kabisa.

Kwa sasa nchi hii inapaswa kujikita zaidi kwenye suala la Elimu ya Sayansi na Teknolojia ili Taifa letu liweze kusonga mbele. Mitaala yote kabisa ya Elimu kwa Sasa inapaswa ibadilishwe ili kuanzisha Mitaala Mipya yenye mlengo wa Sayansi na Teknolojia, mkazo mkubwa zaidi uelekezwe kwenye Elimu ya Vitendo yaani Vocational training (Competency Based Education System)
 
Kabisa, mimi kwa uzoefu wangu badala ya kukusanyika wataalamu walewale waliotupoteza miaka na miaka waangalie njia nyingine na watu wengine ili wapate mawazo mapya na kusave ghalama.

Wanaweza kutumia social media kama hizi kama sehemu ya group discussion na focus interview, wacraft evidence based open ended questions targeting specific education gaps e.g. mitaala, upungufu wa walimu kulingana na ikama, majengo, vitendea kazi, mahabara, uwezo pungufu wa walimu kitaalam, ki-teaching metodology na curriculum.

Inaonekana humu kuna mawazo mazuri na very creative watapata vitu vizuri.

Tatizo planner wetu, watunga sera wetu wanasubiri wapate billioni 15 ili waandae 5 national stakeholders meetings, kila meeting wakae wiki 2 |(siku 14) kujadili tena sehemu moja tu ya tatizo la elimu yetu e.g. curriculum; hizo hela hazitapatikana na hiyo njia ni very costy na non effective. Tungeomba wajiongeze na iwe steps by steps waweze kuaddressing one gaps after another.
 

Je swahili medium schools ambazo ndio nyingi kulinganisha na za kiingereza kuna competency kubwa na critical thinking pana zaidi?
 
Ni kweli kabisa focus ya shule zetu hasa hizi za English medium na ndizo zilizo nyingi,

Mkuu una takwimu kuwa za English ni nyingi zaidi ya za kiswahili? Ama nawe ndio kielelezo cha umahiri uliopotea katika elimu yetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…