KERO Shule zinateka watoto wetu kuhamia boarding, wanaweka ratiba ngumu ili kubana wazazi walipie boarding, wanajali maslahi yao huku watoto wanateseka

KERO Shule zinateka watoto wetu kuhamia boarding, wanaweka ratiba ngumu ili kubana wazazi walipie boarding, wanajali maslahi yao huku watoto wanateseka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Imekuwa ni kama fashini sasa

Mtoto mdogo kabisa mwenye miaka 9 au 12 anakuletea barua kutoka shuleni inasomeka mtoto aanze kwenda boarding kwasababu masomo yanaanza saa kumi na mbili asubuhi, kutoka hadi jioni saa 11, kuingia tena usiku saa moja hadi saa tatu na school bus haitaweza kutumika.

Huyu ni mtoto wa darasa la nne au la saba, kuna haja ya kukamia kiasi hiki ?

Huko shuleni kinachoendelea mzazi unaweza usijue chochote, matroni moja asimamie mamia ya watoto wapi na wapi ? matroni na yeye ana shughuli zake za mchana kujiongezea kipato, utampigia simu atakwambia mtoto anaendelea vizuri ilimradi alinde kazi yake.

watoto wapo bweni moja na wenzao wakubwa na kuna shule zina wanafunzi wa sekondari huwezi jua kinachoendelea.

Kuna kesi kadhaa huripotiwa za uonezi,

watoto wanapigwa na wanatishiwa wawe kimya
watoto wanaingiliwa mabafuni kinguvu (Kufir*a)
watoto wananjiingiza kwenye makubdi ya ajabu
n.k.

Shule zinachojali pesa imeingia, waongoze mitihani, n.k.

USHAURI

Ni muda umefika serikali iingilie kati shule zilazimishwe kufacilitate wanafunzi wa day na wa boarding

  • Day - wawe wanafika shuleni saa moja, kusoma hadi jioni, baada ya hapo warudi kwao.
  • Boarding - kuingia darasni saa 12 asubuhi (huwa wanaamshwa saa 11) 😞, wataungana na wenzao wa day saa moja hadi jioni, kisha wataendelea na ratiba za usiku.
 
Nini kifanyike sasa naona kama unalalamika tu.Wazazi wanahitaji matokeo mazuri.
 
Nini kifanyike sasa naona kama unalalamika tu.Wazazi wanahitaji matokeo mazuri.

Ni muda umefika serikali iingilie kati shule zilazimishwe kufacilitate wanafunzi wa day na wa boarding, hii mitego ya kuweka ratiba za kipuuzi kuwabana wazazi wapeleke watoto boarding ipigwe stop

wanafunzi wa day wasome kama wenzao wa shule nyingine za day - kuingia saa moja kutoka saa kumi

Wale wa boarding waendelee na ratiba zao za kuanza kusoma saa 12 asubuhi, watakutana na wenzao wa day saa moja, wenzao wataondoka jioni wao wataendelea na vipindi vya usiku
 
Utaona kabisa namna walivyoiweka ratiba wanaweka mazingira magumu kwa wazazi walazimike kukubali watoto wakae boarding, hivi regulators wa hizi shule wanafanya kazi gani, au wanakula na hao wamiliki? mtoto kusoma kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 11 jioni, na bado aendelee usiku huu ni utaratibu wa wapi, huyo mtoto amekuwa roboti?
 
Haipo sawa kabisa kupeleka watoto boarding wakiwa wadogo,

Boarding kuna wazazi huwa wanapeleka watoto wao watukutu walioshindikana kimkakati wanawatupa huko, shida inakuja ukiwa mix na watoto wengine, watoto wanapigwa sana bila utetezi, watoto wanaamua kuiga tabia zao ili kuwa salama, watoto wanaf*rwa mabafuni, n.k.
 
Back
Top Bottom