wanabodi kwanza tuelewe kuwa misingi bora ya elimu huanzia pale nyumbani,kuna ile general IQ build up kwa mtoto, tuwe acive kuwajengea watoto tabia ya kujiamini na kujiona wanaweza.Na haswa wanapokuwa primary school tuwaangilie kwa ukaribu mno maendeleo yao. Baada ya haya ndipo tugeukie shule sasa. Binafsi napenda sana shule zinazonjenga mtoto ajitegemee na sio kuwa spoon fed. Ajengwe kumuogopa Mungu na kuheshimu wenzake wote regardless of their faith,color,race,sex,etc. Na hapo ndipo kura yangu inadondokea kweye shule za misheni. Tuwe wakweli na nafsi zetu, wakatoliki na elimu hawana mchezo, maadili na mazingira ya nidhamu kwao ni namba moja. Hata hao viongozi kuanzia kikwete wanakimbiza watoto wao huko na wakifika huko adabu mbele.
Someone asked about boys school
hapa Dar ipo Feza boys ni nzuri kwa nidhamu na elimu.Inaendeshwa na waturuki. Ada ya sekondari boarding ni Tsh Millioni 3
ni kweli kwa wavulana feza ni nzuri sana, kitabia vijana wanakuwa gentlemen, bila kujali alilelewa vipi kabla, ila spoon feeding imewaharibu wajinga, na hakuna kufanya kazi yoyote zaidi ya kusoma. Wanakula vizuri sana na wanafaulu pia sana.
Shule za misheni za kikatoliki na kilutheri wanazingatia sana nidhamu ya muda, muda wa kazi, kusoma, kusali, na kucheza kidogo. Hazingatii comfort sana.
mfano Zile za lushoto na St. Josef Goba watoto wanalalamika chakula etc.
Kuchagua sekondari ya mtoto kunataka mzazi namtoto waongee wajue wanategemea nini, kama ni michezo hakuna pa kwenda ila Mgulani au Filbert Bayi.
Choice ya wavulana ni ndogo sana kuliko ya wasichana.
kuna shule zina programs za lugha, sanaa, music nk. Mtoto wako anaweza kukuongoza, mpe homework mwenyewe pia.
mimi mwenyewe huwa natafuta shule kwa kufuata imani, extracurricula activities, nidhamu ya waalimu na wafanyakazi na jinsi wanavyowasiliana na wanafunzi. Elimu hii ya vitabuni hii ipo tu, mtoto atayajua tu kama tukimkalia kooni. (kufaulu mitihani ni muhimu pia)