Shutuma hizi kuhusu Befoward zina ukweli wowote..

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
14,834
Reaction score
32,522
Wakuu wakati nauliza uliza kuhusu kampuni gani niitumie kuagiza gari, nimekutana na shutuma kuwahusu hawa jamaa!
Wapo wanaodai jamaa huwa wanaleta magari mabovu au muda mwingine unaletewa gari lenye engine kubwa tofauti na ulivyoagiza na bado kuna hidden costs!
Je wazoefu hizi shutuma ni za kweli?
 
UONGO USIO NA MFANO BEFORWARD NDIO INAYOONGOZA KWA KUINGIZA MAGARI TZ na kila kitu kwao ni OPEN itakuwa wivu wa washindani wake
 

Hakuna kitu kama hicho mitandao karibia yote inayouza magari huwa ni wawazi wale sio waswahili kama sisi wanajielewa
 
Usisikilize story za watu...
Beforward hawana shida shida iko huku kwetu Bongo....
Kuna hawa jamaa wenye makampuni ya kuagiza magari....hawa ni miongoni mwa watu wanaoichafua Beforward ili watu muogope kwenda kununua Beforward, badala yake muwatumie wao ilihali wao wanaagiza huko huko BF

Beforwad ni kampuni kubwa sana hainannjaa ndogo ndogo za kuchakachua magari..

Nimewahi kuagiza gari mwenyewe beforward...lilikuja kama lilivyokuwa linaonekana kwenye picha zao....tena waliniwekea spare tyre mbili..

Mchezo wa uchakachuaji unafanyika hapa Bongo gari zikishafika...mfano kuiba redio, jeki, spare tyre au kushusha mileage.

Mimi gari yangu waliiba kale kafataki kekundu kanakokaa pale chini ya uvungu wa miguu ya abiria wa siti ya mbele..

Sina mpango wa kuagiza gari kupitia kampuni nyingine zaidi ya BF...coz bei zao zipo poa na uwazi mkubwa..
 
Usidanganywe ndugu yangu. Hakuna kampuni ya uagizaji magari walio wawazi kama Beforward, unaletewa gari lako kama ulivyoonyeshwa likiwa huko lilikotoka na hata ukiwatumia kama forwading and clearing agents wako utafurahi sana huduma zao. Usidanganywe na story za vijiweni. Hata kukitokea tatizo lolote hwa jamaa wako vizuri sana kulishughulikia tena kwa wakati.
 

Mkuu kale kadude kekundu ndiyo kalichomolewa? [emoji848][emoji848][emoji848] what kind of a fake thief was that?
 
Tamani niwaalike mje wakati wa kushusha magari muone watu wanavyohangaika kuibusti ili ishuke
 
Sio kweli, mimi nilichaguaga gari kabla sijalipia walinipa anagalizo kuwa lina kasoro mbili pamoja na oil seal ina tatizo na wakanishauti nichague jingine, na kweli waliniletea gari safi kabisa.
Huwa wanatoa cheyi wa ukaguzi wa kifaa kimoja kimoja na hali yake.
Wabongo roho mbaya fanya maamuzi na iyunze post hii
 
Uko sawa nami nimemjibu hivyo
Befoward huwa wanakuwa wawazi Sana Kwenye Magari Yao hata ukitembelea site Yao utaona Magari Yao kuanzia body,uvungu na engine.
Sometimes story za vijiweni zinaharibu Sana watu
 
Yes, kale kekundu kama kafataki[emoji848][emoji848][emoji848]
Me mwenyewe nilishangaa...coz tulipomaliza kulipia madocuments yote pale bandarini, derwva akaambiwa akachukue gari...akalikuta milango yote ipo wazi...limewashwa lipo silence, redio inaongea...akaambiwa tu..Gari hilo hapo....

Ina maana tungechelewa zaidi, redio, jeki nk visingebaki
Mkuu kale kadude kekundu ndiyo kalichomolewa? [emoji848][emoji848][emoji848] what kind of a fake thief was that?
 
Watu wa Beforward mnaanzisha uzi wenu halafu mnaanza kujijibu si mlipie commercial tu
Hapana bro....sisi si watu wa beforward bali ni wateja ambao tumeshawahi kupata huduma za beforward....binafsi sikujuta........
 
unataka kuagiza gari wakati bei tu za vitu vya mlimani city ulikuwa unalialia
 
Sasa zinahusiana vipi? Unafikiri kila anayelalamika bei za pale ni kwamba hana hela?
unataka kuagiza gari wakati bei tu za vitu vya mlimani city ulikuwa unalialia
 
Kwa umaarufu waliokuwa nao sidhani kama wanaweza kujiharibia biashara yao kwa kufanya vitu vya kipuuzi kama hivyo...
 
Tamani niwaalike mje wakati wa kushusha magari muone watu wanavyohangaika kuibusti ili ishuke
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] true nishaliona hiloo pale bandarini,mengine huwa yanavutwa kabisaa na kamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…