Si ajabu wangekuwa washadai yeye si Mtanzania!

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Yanayoendelea huko Kenya kuhusu suala la uraia wa Miguna Miguna yanasikitisha.

Lakini mwisho wa siku naamini Miguna atawabwaga tu mahakamani.

Na yote haya yamemfika kwa sababu tu alianza kumkosoa sana Uhuru Kenyatta.

Nakumbuka kwenye ule uchaguzi wa 2013 alivyokuwa anapendwa na watu wa Jubilee kwa sababu alikuwa akimnanga Odinga.

Alialikwa hadi kwenye hafla ya kusherehekea uapisho wa Kenyata.

Muda wote huu, hata kipindi akiwa mshauri wa Raila Odinga kipindi ni waziri mkuu, suala la uraia wake halikuwa na utata!

Kagombea mpaka ugavana wa Nairobi na uraia wake ulithibitishwa na tume yao ya uchaguzi.

Hata kitambulisho cha uraia wa Kenya anacho. Achilia mbali kuwa kazaliwa Kenya.

Sasa ghafla baada ya kuanza kumkosoa sana Uhuru eti ndo suala la uraia wake limeibuka.

Sasa huyu Miguna huwa namfananisha na Tundu Lisu kwa umachachari wao wa kuweza kuongea bila hofu.

Kwa mtaji huo, naamini kuwa kama Lisu angekuwa ni mzaliwa wa mikoa iliyo mipakani mwa Tanzania na nchi inayopakana nazo, kudhani au kuhisi kuwa uraia wake ungekuwa ushahojiwa si jambo la ajabu.

Baadhi ya kesi alizofunguliwa Lisu zinachekesha mno kiasi cha kuweza kumfanya mtu adhanie kuwa hao waliotoa maagizo ya yeye kukamatwa na kufunguliwa kesi ni wanafanya hivyo ili kumsumbua tu na si kwa nia ya kwamba wanamfungulia kesi ili hatimaye wampate na makosa na wamfunge jela.

Nadhani huwa wanajua kabisa kuwa kesi zao hazina mashiko.

Hata kwa Miguna Miguna nako ni vivyo hivyo tu.

Watawala wengi wa Afrika wanafanana kwa mengi. Hawapendi kukosolewa na hawana uvumilivu mwingi wa watu wanaotofautiana nao kimtazamo.

Na hulka hii haijalishi kama mtu yupo upinzani au la. Ni kwamba, mtu huyo akishapata madaraka na mamlaka makubwa anabadilika na kutaka kuwa mungu mtu!

Tuna safari ndefu sana na sidhani kama hata njia ya kutufikisha huko twaijua.
 
Kila lenye mwanzo halikos kuwa na mwsho.

Sema mwsho unaweza kuwa mzuri au mbaya.
 
he's back to lead the mother of all demostrations
 
Kimsingi wanasiasa wa Afrika wote ni sawa kitabia! Awe upinzani awe kwenye madaraka. Mimi huwa nashangaa sana watu wanaotaka kutoana roho kwa ajili ya wanasiasa. Mwaka 2012 ungeambiwa leo hii Lowassa angekuwa pro Chadema na Dr Slaa angekuwa pro CCM ungeamini? Kinachoongoza wanasiasa wetu ni kitu kimoja tu: maslahi yao!
 
Afadhali ya Kenya, lakini sio Tanzania ya tingatinga.....

Huyu ndugu tuombe Mungu amalize miaka yake aiache Tanzania ikiwa Salama.

Jamaa kila siku anapunguza mikoa kwa ushawishi, mwisho wa siku atakuwa laisi wa Kanda ya ziwa tu.

Alianza kanda ya kati Singida, akaja kanda ya kusini Iringa,Mbeya na Njombe sasa hivi yupo kanda ya kaskazini....Na hii kanda ilivyo na umoja na ushawishi imetapakaa kila idara ndani na nje ya nchi itamsumbua sana na itamjaza hasira mno.

Baba tuepushe na hiki kikombe.
 
Siasa ni biashara chafu, ukweli hugeuzwa uongo na uongo hugeuzwa ukweli kwa maslahi ya kisiasa.
Mara nyingine huwa najiona mjinga sana kushabikia biashara hizi chafu za watu.
 
Unajipendekeza?
 
Ndio maana mimi sio mpz sana wa Politics...maana wanasiasa vigeugeu hawachelewi kubadilika wewe unaewashabikia kutumia nguvu unabaki peke yako.
Msijidanganye. TL anajua udhaifu wa Polisi na Ofisi ya DPP ndo maana alikuwa anawachezea michezo yake.
 
Boss idawa Hauogopi Watu Wasiojulikana???!!! Haujui kukosoa ni Kosa la Jinai???!!! Umeongea vizuri na ukweli. Boss Mkuu alianza vizuri sana. Ila sasa sijui kalewa sifa au wanaomshauri na kujishauri wanamdanganya na kujidanganya.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…