GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Naamini sitamkasirisha mtu kwa maoni yangu! Hivi ndivyo niaminivyo.
Uwe ni mweusi sana au mweupe mno ( japo inasemekana hakuna mtu mweusi wala mweupe)!
Uwe mfupi mno au mrefu kuliko kawaida!
Uwe na miguu mirefu au ngozi inayong'aa hata bila mafuta!
Vyo yote vile! Maadam hukuchangia chochote kuwa hivyo, haifai kujisifia. Labda umshukuru Mungu! Naam, afanyaye hivyo ana akili njema.
Maumbile ya mtu ni "ascribed status" na si "achieved status '. Maadam hana mchango alioutoa kuwa hivyo, hastahili kujisifia wala si haki kukejeliwa na mtu yeyote yule. Ukiona mtu anamkejeli kwa sababu ya mwonekano wake wa kuzaliwa ujue ana shida katika kufikiri kwake!
Alau kwa aliyejijengea uwezo wa kunyanyua vitu vizito kwa sababu ya mazoezi makali anaweza akajisifia. Kafikia hapo kwa juhudi zake. Ni achieved status!
Inasikitisha kuona baadhi ya watu wakijisumbua kurekebisha maumbile yao, si kwa sababu za kiafya, bali ili tu aonekane anavutia!
Wengine, hasa mabinti, wamejidunga sindano ili wawe na makalio makubwa! Kuna waliofanya makubwa zaidi ya hayo. Wapo wa kiume na wa kike.
Lakini yote hayo ni kwa sababu ya kutokujikibali! Kwa aliyejikubali, hata kama maumbile yake hayaonekani kama ni ya kawaida, ataheshimika tu!
Nilisoma mitandaoni kipindi fulani kuwa binti mmoja kutoka Sudan, nafikiri, ambaye alikuwa mweusi sana, alipofika Marekani, mwonekano wake huo uligeuka kuwa fursa kwake! Sikumbuki vizuri, lakini nafikiri alipata kazi inayoendana na uanamitindo hivi! Inawezekana kwa Waafrika wenzake alionekana kituko, lakini kwa sababu alikuwa amejikubali hakukimbilia mikorogo kujikoboa sura yake awe kama Mzungu. Alijikubali, hivyo na watu wengine waliishia kumkubali na kumtunuku!
Nigeria kulikuwa na wachekeshaji maarufu: AKI NA UKWA ( sijui wako wapi kwa sasa). Inawezekana kule kuwa wafupi sana ndiyo kulichochea wao kuwa maarufu sana duniani, mpaka nikaweza kuwafahamu.
Nick Vujicic kazaliwa hana miguu wala mikono! Lakini kwa kuwa amejikubali, kwa sasa anafanya jitihada kuwatia moyo watu wengine, wengi wao wakiwa ni watu waliozaliwa na viungo vyote kujikubali na kuyaishi maisha yao kikamilifu!
Usitafute kuishi kwa ajili ya kuwaridhisha watu wengine! Hsutaweza!
Mwenye akili hawezi kujivunia maumbile ya kuzaliwa nayo! Mwenye akili timamu hawezi kuwakejeli wengine kwa sababu ya upekee wa maumbile yao ya kuzaliwa!
Kitu anachoweza kufanya mwenye akili ni kumtukuza Mungu!
Jikubali ili ukubaliwe!