Si hata Rais Mstaafu Mwinyi walisema anauza nchi? Kiko wapi?

Hivi unajua kuwa kabla ya JPM kuingia madarakani, TZ illikuwa inapata 4% tu ya faida ya uuzwaji dhahabu inayochimbwa Bongo?

Hiyo ni dhahabu, hapo hujagusa Tanzanite au Almasi ya Mwadui...

Tatizo ni CCM na sio Kambarage, Mwinyi, Mkapa, JK, JPM wala Samia
 
Ndio ameuza nchi kwa mwarabu wa Loliondo
 
Wewe ni muongo sana....! Kuna mambo machache umesema kweli lakini mengi umedanganya ili kusitiri agenda yako.

Mosi, siyo kweli kwamba kabla ya vita ya Kagera watanzania walipanga foleni kununua vitu madukani. Nataka nikukumbushe kwamba mwaka 1970 hadi 1973 uchumi wa Tanzania ulikuwa juu kuliko Malaysia , Indonesia, na karibu Nchi zote za Afrika mashariki. Dollar moja ya Maerkani ilikuwa sawa na shilling 5 za Tanzania. Madukani kulikuwa na bila zote muhimu.

Pili, Maduka ya Ujamaa yalianza baada ya kuanzishwa vijiji vya ujamaa 1974/1974. Na lengo kubwa ilikuwa ni kuwauzia watanzania bidhaa kwa bei nafuu. Wakati huo maduka ya watu binafsi bado yalikuwepo !!! Hali ngumu ya uchumi ilisababishwa hasa na mambo mawili.

1.Vita vya Kagera
2.Kutaifisha mashamba ya Mkonge na baadhi ya mashamba ya chai.

Baada ya vita vya kagera Nchi ilikuwa haina fedha za kigeni, hivyo kushindwa kuagiza bidha mbalimbali kutoka ng'ambo. Maduka yakaanza kukosa bidhaa na baadae kufilisika kabisa.

Uchumi huu wa sasa, ulikuja kurudi baada ya serikali yetu kupewa msaada wa dollar za kimarekani million 500 na Zimbabwe mwanzoni mwa 1990.Watu sasa wakaruhusiwa kuagiza bidhaa kutoka nje kwasababu fedha za kigeni zilikuwepo. Mpaka tunafika 1995 maduka yalikuwa yamejaa bidhaa mbali mbali . Ndio haya maisha tunayo endelea nayo mpaka sasa.

Rais Mwinyi kwanza alifanya siri kuwauzia Waarabu vitalu vya kuwinda wanyama huko Loliondo. Habari zilifichuliwa na Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi marehemu Stani Katabalo. Kwahiyo mtu wa Kwanza kuuza rasilimali zetu kwa wageni ni President Mwinyi.

Miaka 30 baadae Waarabu wamefanikiwa kutengeneza man made mbuga ya wanyama huko kwao, wanyama wote wamewatoa Tanzania.

Sasa jiulize, miaka 20 ijayo tutapata watalii kutoka Uarabuni kuja kwenye mbuga zetu??

MALI ZA WAJINGA HULIWA NA WEREVU.
 
Mlidai uhuru wa nini? Kama hamuwezi kujifanyia kitu? Kila miaka mitano mnakuja na slogan mpya.. Mara fagio la chuma, Mata ukweli na uwazi, mara viwanda,mara hapa kazi tu,mara kazi iendelee mara upuuzi kuuza tu... why msiseme tu kuwa hamna fikra mpishe wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…