Si Hiroshima na Nagasaki pekee, Afrika pia inahitaji iombwe radhi

Si Hiroshima na Nagasaki pekee, Afrika pia inahitaji iombwe radhi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
9a6672ec32bdaa5cd6a8302cbd541ede.jpg

Ni ukweli kuwa pamoja na kufahamu yaliyotokea Japan Rais Obama anajua kuwa mataifa mengi ya Afrika yameumizwa na matendo ya Marekani ambayo pengine taifa hili linastahili kuomba msamaha.
Maumivu yalifanyika kupitia utumwa ambao ulisaidia kujenga uchumi wa Ulaya na Marekani. Matokeo yake Waafrika waliuzwa kama chumvi sokoni. Utumwa huu umesababisha kuibuka kwa jamii inayoitwa ‘Waniga’ au ‘Wanegro’ hawa ni Waamerika wa kizazi cha utumwa Marekani na Ulaya.
Ni jina linalotumiwa kuwadhihaki Waafrika wote popote wanapoonekana nje ya bara hili.
Lakini, pamoja na utumwa na ukoloni Amerika imehusika kurudisha nyuma maendeleo ya Afrika baada ya uhuru.
Ina mkono kwenye sera iliyojulikana kama ‘destabilization’. Ilidhoofisha Afrika, iliyumbisha serikali nyingi kama Somalia, Congo na Angola


1.UTUMWA

Japo inaonekana kuwa yaliyopita si ndwele (ndwele ni magonjwa), tugange yajayo, utumwa umebaki kuwa ugonjwa kwa familia nyingi na hasa za hao ambao wanajiona kuwa wako kwenye mizozo na wengine kujikuta kwenye taifa au mahala ambako hawakustahili kuwapo hawa ni Waamerika Weusi au Wanigro au ‘Niggers’.
Licha watu kudhalilishwa kama wanyama utumwa una kovu lisilokwisha kwa Waafrika. Ndicho chanzo cha kupewa jina la ‘Nigger’, Niga hadi leo linatumiwa kumaanisha mtu mweusi.
Ni tusi kubwa linalodhalilisha kuliko chochote katika historia ya majina ya binadamu Ndilo jina apewalo Mwafrika kila anapokanyaga nje ya bara lake. Mathalani, kuna wakati nilifika Finland nikasikia watu weusi wakiitwa ‘Monsta Henkel au Niker’ kwa hiyo ni alama iliyozalishwa na utumwa na ndiyo inayotumiwa hadi leo kuudhihaki Uafrika.
Kamusi za Kiingereza ‘Nigger’ ni neno lenye asili ya Kifaransa ‘Neegre’ na Kispaniola ‘Nigro’ yakimaanisha mwanadamu mweusi, mjinga, mtu duni, dhalili na zaidi mhanga aliyeathirika asiye na haki za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Ni tusi na jina lenye kuudhalilisha utu wa weusi. Haya ni matokeo ya biashara ya utumwa ambayo madhara yake yamesababisha hadi leo Waafrika kudharauliwa duniani kote. Licha ya miji mikubwa na viwanda kujengwa huko Marekani na Ulaya. Utumwa umeacha kovu kuanzia Tanzania hadi Togo.


2.UTAJIRI WA UTUMWA

Ipo benki kubwa duniani yenye matawi Afrika nzima pamoja na Dar, imeanzishwa kwa biashara ya utumwa. Historia ya mtaji wake ni kumwaga damu ya Mwafrika kwa kumdhalilisha mnadani na inadaiwa ilianzishwa miaka ya 1750.
Katika toleo lake la April 2007, Gazeti la Business Observer la Uingereza, ambalo taarifa zake zipo mtandaoni linaripoti kuwa benki hiyo inahusika na biashara ya kuuza , lakini baadhi ya maofisa wake wanataka suala hilo lichukuliwe kuwa ni ‘tukio la kiwakati’ kwani kwa zama hizo biashara ya watumwa ilikuwa kawaida, haikuonekana kuwa kosa.
Kuna wakati benki hiyo ililipa zaidi ya dola milioni 3.6 kama fidia baada ya kuhusishwa na uhalifu wa ukatili dhidi ya binadamu yakiwamo mauji ya kimbari yaliyofanyika enzi za utawala wa Hitler huko Ujerumani. Benki kama ililipa wengine kwanini isiombe radhi Waafrika na kusaidia kujenga taasisi zitakazotumiwa na kila mmoja kama viwanja vya ndege, madaraja, barabara na hata hospitali kubwa za kitaifa kwa kuwa ubinadamu wa Mwafrika ulidhalilishwa?


3.UTESAJI USIOVUMILIKA

Biashara ya utumwa hakika imeangamiza Waafrika, iliwadhalilisha kama wanyama maana enzi hizo pamoja na ukatili na vipigo visivyoelezeka, watumwa walisafirishwa ndani ya bahari wakilazimishwa kujisaidia haja zote ndani ya meli, maiti zilioza na kusafirishwa pamoja na walio hai. Wanawake walidhalilika na kutaabika kwa vile walipokuwa safarini na utumwani hawakuweza kujisitiri na aibu za kimaumbile zinazowapata kila mwezi.
Watu waliishi na wanyama kama panya ili kula uchafu kwenye meli, walikula choo cha binadamu, lakini pia waliwatafuna kama nyama.
Hivi Rais Obama, Afrika haikustahili kuombwa radhi kwa madhila hayo makubwa ya udhalilishaji uliopinduikia? Hivi Uingereza nayo ambayo ni sehemu ya G-7 inaonaje kuhusu kuisihi Afrika kwa unyama huo wa kupindukia ambao hauna mfano hasa pale Mwafrika alipozikwa akiwa hai?
Yaliyotokea Hiroshima na Nagasaki ni makubwa, lakini ya Afrika nayo hakika hayavumiliki. Pengine hakuna viongozi majasiri, wanasheria na watetezi wa haki za binadamu wasio na woga wanaoweza kuisimamia ajenda hii.


4.SERA YA ‘DESTABILIZATION’

Rais Obama anafahamu fika kuwa sera hiyo ya Marekani ya kuvuruga siasa za nchi za Kiafrika hasa zile zilizokuwa na mrengo wa Kijamaa na kuzidhoofisha kiuchumi, zina mkono wa G-7 na Marekani. Kushirikiana na iliyokuwa Urusi na mataifa ya Kisovieti imekuwa ni chanzo cha vurumai zinazoendelea kwenye mataifa mengi barani hapa mfano Somalia, Sudan na Congo.
Obama anajua kuwa chanzo cha Al Shaabab huko Somalia, ni kung’olewa Rais Mohamed Siad Barre, aliyekuwa mbabe wa kivita, kisa alikuwa anaelekea kuwa mshirika wa Urusi na kueneza Ukomonisti, aliangushwa mwaka 1991. Hivi kama Barre angekuwapo Somali ingeparaganyika wakati aliweza kuiunganisha?
Huko Zaire majasusi wa Shirila la CIA walisaidia kumweka Mobutu Sese Seko, madarakani ili kuhakikisha kuwa hakuna uhusiano na Moscow, baada ya kumuua Waziri Mkuu wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia Patrice Lumumba, mwaka 1961. Hata leo Congo hakukaliki.
Marekani inatajwa kuhusika kudhoofisha maendeleo ya kisiasa Angola kwa kumuunga mkono ‘hasimu wa kisiasa ili kukwamisha mafanikio ya uhuru hasa baada ya Angola kuelekea kwenye ujamaa.
Ilimuunga mkono muasisi wa chama cha Unita, Jonas Savimbi na kuendeleza vita iliyoua mamilioni huko Angola, kuanzia miaka 1975. Hiyo ilikuwa ni chuki ya dhahiri dhidi ya chama cha MPLA kilichokuwa kikisaidiwa na wajamaa wa Cuba na Urusi.
Muasi na gaidi huyu ambaye aliua mamilioni ya Waangola na kuharibu mali za umma na binafsi kwa msaada wa CIA, aliheshimika na kukaribishwa Ikulu ya Marekani na kuandaliwa dhifa ya heshima kubwa akiitwa ‘true here of our time au shujaa wa ukweli wa zama’ Mitandao inaripoti.
Ethiopia nayo licha ya kupigana na Eritrea kwa miongo kadhaa, Rais wake Mengistu Haile Mariam, aliangushwa mwaka 1987 na kukimbilia kizuizini nchini Zimbabwe hadi alipofariki dunia. Marekani anahusika kisa, Haile Mariam alikuwa anaelekea kuwa mshirika wa Ukomunisti.
Liberia nako, taifa linaloundwa na watumwa waliotoka Marekani, halijasahau madhila ya kupinduliwa na kuuwa Rais William Tolbert na Sajini Samuel Doe, huyu alikuwa mshirika mkubwa wa Marekani, akidaiwa kupokea misaada minono kuliko taifa lolote la Afrika Kusini ya Sahara.
Obama, Afrika haistahili kuombwa radhi kwa maovu haya ambayo yanaongeza umaskini na dhiki kwa mamilioni ya watu wasio na hatia?
 
Chukua hili wazo,sisi waafrika ni yatima katika hii sayari, ni sisi wenyewe ndio tutajikomboa kutoka katika vita hii endelevu,tusibaguane katika misingi ya dini au kabila na matabaka,tukikataa kubaguana tutakuwa tumeishinda moja ya mipango yao.
 
hii ni sawa kabisa maaan bado tuna makovu ya uovu ulotendeka
 
Back
Top Bottom