Si Kila Mtu Anafaa Kuajiliwa Katika Biashara Inayoanza

Si Kila Mtu Anafaa Kuajiliwa Katika Biashara Inayoanza

Nkandi

Member
Joined
Nov 20, 2010
Posts
83
Reaction score
42
Salaam Mwanajamii,

Leo naanza kwa kuweka bayana hili, ifahamike dhahiri kuwa sina maana ya kutaka kuzuia au kushiriki katika kuhakikisha watu wananyimwa ajira na 'wajasiliamali wapya' bali ieleweke nia yangu ni kuwajuza waajili wapya namna ya watu wanaoweza kuwafaa katika biashara zao kuanzia hatua za mwanzo wa biashara zao.

Biashara inayoanza inafanana sana mtoto mdogo anayehitaji uangalizi mkubwa sana,kwa mtoto wazazi ujitahidi sana kumwangalia mtoto kwa umakini na ukaribu sana...kwa upande wa biashara zinazoanza,kwa hapa kwetu Tanzania nimebaini kwa kutumia utafiti usiyo rasmi kuwa wenye biashara wengi ni wale walioajiriwa sehemu nyingine,yaani wanaichukulia biashara kama kipato B katika maisha yao.

Wale wanaochukulia biashara zao kama Kipato B wanakawaida ya kufanya maamuzi ya watu wanaowaajili bila kuzingatia mambo mengi,si wao tu hata wale ambao wanategemea biashara zao kama chanzo kikuu cha mapato wanapaswa kufahamu mambo kadha wa kadha kuhusu watu wakuajiri.

Wajasiliamali wanatakiwa kufahamu kuwa si kila mtu anastahili kuajiliwa katika nafasi fulani,watu wenye vitu vifuatavyo wanafaa sana kuajiliwa na wajasiliamali:

  • Mtu anayejiamini,mwenye uwezo wa kuchukua maamuzi haraka
  • Mtu mwenye kuwa na hali ya ujasiliamali (Entrepreneurship Spirit)
  • Anayeweza kuvaa uhusika wa mteja
  • Kuwa tayari kujitoa zaidi kwa mteja hata kuzidisha muda wake wa kazi
  • Mtu mwenye kujali na kufahamu kuwa biashara hiyo ndiyo ajira yake,ikikuwa naye atakuwa kiuchumi
  • Awe mtu mbunifu na mwenye uwezo wa kuziona fursa nyingine
  • Awe mtu kuweza ku'interact na watu' na mwenye kuelewa kuwa wateja wanatofautiana
  • Awe na tabia ya kutoa mrejesho wa vitu
  • Awe 'mbaili' (Natural Economist)
  • Awe mwenye kuweza kutimiza ahadi zake

Watu wenyesifa za namna hii ni watu wanaofaa sana kuajiliwa na wajasiliamali kwakuwa wanaweza kuikuza biashara. Ingawa ifahamike dhahiri watu wa namna hii ni changamoto sana kuwa 'retain' katika biashara kwa kuwa wanaonana na watu wengi ambao upenda ufanyaji kazi wao na uwaahidi maisha bora kuliko hata yale ambayo sisi tuliwahi kuahidiwa hivyo yatakiwa kubuni namna ya kuweza kuwa 'retain' katika biashara vinginevyo wawezakujikuta unakuwa 'stepping stone' ya wengine

Biashara iliyokuwa iliyokuwa,imekuzwa na watu na ile iliyodindoka imedondoshwa na watu, hivyo uamuzi wa mmiliki uweza kupelekea hali yoyote kati ya hizo mbili.

Tuondoe ile dhana ya kwamba 'nina mdogo wangu kamaliza form 4 ngoja anisaidie' anagalie asijekukusaidia kuiua biashara kwa kuweka Bora mtu na si mtu bora katika biashara yako.

Mambo ni mengi na wakati umeisha,yanipasa niendelee na majukumu mengineyo.

Naomba kuwasilisha,

Majadiliano,ushauri na mikakati: kkmarketing61@yahoo.com
 
Mkuu inaonekana wewe ni mwalimu mzuri wa wajasirimali. Kama una vitabu maalum kwa ajili ya maelekezo yako naomba ni pm kwa kuwa navihitaji.
 
Nkandi, kweli kabisa,ila umesahau jambo moja muhimu sana,"uaminifu".

Kweli,sikuitaja hii ndiyo raha ya mjadala...full kukumbushana ingawa kwa mtu mwenye vigezo hivyo inategemewa kuwa mwaminifu.

Thanks kwa kutukumbusha.....Snochet
 
Mkuu inaonekana wewe ni mwalimu mzuri wa wajasirimali. Kama una vitabu maalum kwa ajili ya maelekezo yako naomba ni pm kwa kuwa navihitaji.

Bado tupo kwenye mchakato,kitakuwa ni kama kijarida kidogo ambacho mtu ataweza kukisoma na kuweka hata mfukoni...si wajua mazoea ya kusoma vitabu ni changamoto...
 
Mkuu ni kweli kabisa, Ila katika swala zima la kuwaajiri watu kuna pandembili ambazo ni lazima zote ziwajibike.
Ila ni vigumu kupima hayo yote unayo yasema kwa sababu hata spiri ta Entreprenership iko Moyoni mwa mwtu, na hata uaminifu nao uko moyoni na ni vigumu kuuona.

Kina cho takiwa ni kutoa elimu ya kutosha kwa anaye ajiriwa na hapa ndo tatizo lililipo kwa wajasirimali wengi, Unaweza muajiri mke/mme/shemeji/shangazi/mchumba na kazalika ila kikubwa ni kuwapa elimu ya jinsi ya kusimamia biashara na kikubwa ni elimu kama ya

1. Kuhudumia wateja
2. Biashara
3. Na mahesabu

Ni vigumu kutoa elimu ya uaminifu make mtu kama ni mwizi ni mwizi tu hata ukifanyaje,

Na kwa mwajiri ni lazima afanye yafuatayo

1. Aboreshe Masilahi ya mfanyakazi- Ni lazima alipwe vizuri

2. Ni lazima apewe mailahi mengine

3. Ni lazima uwe naye karibu sana

4. Ikibidi mwambie kama atafanya kazi vizuri utakuja kumfanya awe mmoja wa wamiliki wa kampuni yako, yes ni lazima saazingine ufikilie kumfanya awe sehemu ya biashara/mmiliki wa biashara yako

Bila kufanya hayo itakuwa ni kazi bure, sana sana wateendeleza hujuma zidi yako. huwezi sema mfanya kazi awe mwaminifu huku humlipi vizuri, unamcheleweshea mshahara wake, unamlipa pesa isiyo lingana na mapato unayo pata,

NB: Hii ni hadi kwa mke/mme/shemeji/kaka/dada na kazalika, ni lazima hawa walipwe vizuri la sivyo watakuwa ndo wanao ongoza kwa kukuhujumu, na hakuna watu wanao hujumu kama ndugu so ni lazima uwape elimu ya kutosha na ikibidi fikilia kumshirikisha kuwa na hisa
 
Mkuu,hayo yote yanaweza kufahamika kama itafanywa interview...si ile tuliyoizoea...mimi niliwahi kufanyiwa interview kwenye kampuni la kimataifa,baada ya kufanikiwa katika enterview wakanipa majibu yote....kuna namna ya kisaikolojia am bayo mtu uulizwa na kuambiwa kufanya ambayo majibu yake yatamtambulisha ni nani.

Naunga mkono hoja ya kuboresha hali ya wafanyakazi wote....ukaribu na undugu usimnyonye mtu yeyote
 
Back
Top Bottom