Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Leo nimeshtushwa sana, kama vile Mheshimiwa Dk. Nchimbi hakusikika alipowaonya watu kuhusu kampeni.
Madiwani hawa wanapaswa kuonywa, na ikiwezekana, kunyimwa posho kwa muda kutokana na kwenda kinyume na maagizo ya chama.
Mheshimiwa, ulitoa onyo wazi, likirushwa moja kwa moja kwenye televisheni, na ukaapa kuwa yeyote atakayeanza kampeni kabla ya wakati atakutana na madhara yake.
Lakini leo, madiwani wa Arusha wanapendekeza Gambo kuwa mbunge wa Arusha na kutaja majina ya wanaowataka wao, jambo linalokiuka utaratibu.
Ni vyema wakumbuke kuwa Gambo bado ni mbunge wa CCM hadi Oktoba 2025.
Nashauri wapewe adhabu kali kama funzo kwa wote wanaopuuza maagizo kwa sababu ya tamaa zao. Mheshimiwa Katibu, hili linapaswa kuchukuliwa kwa uzito wake.
Inasikitisha sana, lakini naamini kamati itafuatilia na kuchukua hatua stahiki dhidi yao.