Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363

Moja ya namna nzuri sana ya kula kiporo ni kukibadilisha kua chakula kipya kwa kukipa ladha au kionjo kipya kitakacholeta utofauti na Chakula ulichokula jana au juzi .
Jumapili iliyopita nilikusanya viporo vyote vya wali vilivyokua frijini na kuvichanganya kisha nikaongeze vionjo vipya ndani yake ili kupata ladha mpya.Tulitusmia kiporo hicho kwa mlo wa mchana.

Nilichanganya aina tatu tofauti za pishi la wali,ambavyo vyote vilikua viporo vya wiki hiyo.Nilichanganya Wali wa nyanya,wali wa carry powder na wali mweupe au wali wa maji.
Kwakua mapishi haya yote yanaladha tofauti kutokana na uasilia wa viungo na mahitaji yaliyotumika kuviandaa,niliongeza vionjo vipya ili kuvipa vyakula hivi vitatu ladha moja iliyovijumuisha kwa pamoja na kuvibadilisha kua chakula kimoja ,chenye ladha moja.
- Katika sufuria niliweka mafuta kiasi,
- Nikaweka vitunguu maji vingi vilivyokatwa vipande vidogo.
- Nikakaanga adi vitunguu vikasinyaa na kuiva,sikuacha vibadilike rangi.
- Nikaongeza viporo vyote vya wali na kukaanga kwa muda mfupi.
- Nikafunika na kuuacha wali upate moto kwa muda adi ukafanana na wali uliopikwa siku hiyo(joto lake)

Siri kubwa katika kuongeza vionjo kwenye kiporo cha wali ili kukipa ladha mpya ni:
- kutumia viungo vinavyoweza kuivishwa na mafuta tu na visivyohitaji kuchemka kwa muda mrefu.vituguu,nyanya,giligiliani,majani fresh ya vitunguu,dania,na tangawizi mbichi ni baadhi ya viungo vinavyofaa.
- Kupasha kwa kutumia mafuta utakayoungia viungo bila kuongeza maji.kwakua kiporo ni chakula kilichoiva tayari.Ukikiongezea maji kuna uwezakano mkubwa sana wa chakula hicho kuwa rojo au boko.kwa ujumla wali unapoteza ile hali ya kuchambuka.
- Tumia moto mdogo.Baada ya kuunga viungo,pale tu unapoweka kiporo cha wali punguza moto.Tumia moto mdogo sana kwani lengo ni kuhakikisha kiporo kimepata moto vizuri na kua kama wali fresh uliopikwa siku hivyo.

Unapotenga chakula mezani nivyema kukiremba ili kumvutia mlaji.
IPE FAMILIA KILICHO BORA