Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Tatizo ni kwamba siku zote vyama vya upinzani vimeingia katika uchaguzi mkuu bila kuwa na agenda kuu ambayo inawapa changamoto kubwa CCM. Utakuta upinzani wanakuja na slogan kama ubwawa kwa kila mtu, nitawajaza mapesa nk, sera au ilani nyepesi zisizowafanya wananchi wafikirie kuwapa kura badala ya CCM.
Wakati fulani Chadema walijaribu kuja na sera ya majimbo. Kosa walilofanya hapa ilikuwa ni kutumia sera ambayo watu hawailewi. Ni wapiga kura wangapi wa Tanzania wanaelewa implications za kuwa na sera ya majimbo?
Sasa ushauri wangu kwa Chadema ni kwamba, ingieni katika uchaguzi ujao mkitoa ahadi kwa Watanzania kwamba mkishinda uchaguzi mtahakikisha Watanzania bara nao wanapata serikali yao kama ilivyo kwa upande wa Zanzibar. Waambieni wananchi kwamba hilo litakapotokea basi pia mtawapa Zanzibar uhuru zaidi wa kuamua mambo yao kama kujiunga na OIC hata na FIFA, nk, kwa sababu Tanganyika nao watakuwa na serikali yao na hilo halitawahusu. Hili litafanya mpate kura nyingi bara na visiwani, bila kukiuka kanuni ya kubomoa muungano.
Kimsingi, mtakuwa mnatumia uchaguzi mkuu kama referandum ya wananchi kuamua kuwa na serikali tatu, na hivi ndivyo vyama tawala vinavyokuwa challenged kwenye uchaguzi. Tumia slogans kama Vote for Chadema get Tanganyika, get OIC.
Zaidi ya serikali ya Tanganyika, angalieni vitu vyenye impact kubwa - create common enemies ambao Watanzania wataona mko upande wao - kwa mfano, kero za fine za trafiki barabarani, kuunda upya jeshi la polisi lililo rafiki kwa raia, kuondoa kero za BRT Dar, kurudisha Fastjet washindane na ATC ili kila mwananchi apande ndege! Hiyo ndio lugha wananchi wanaelewa. Kampeni za kusema mtahakikisha hakuna ufisadi, madawati sijui, hazitawafikisha popote! Kila mtu anajua hata Chadema mkishika madaraka kutakuwa na mafisadi ndani ya chama chenu.
Na pia acknowledge Magufuli for the good he accomplished for the country, while minimizing the bad things he subjected the country to, kwa kumtafutia excuse kwa nini alifanya hivyo na kuonyesha mmemsamehe kwa sababu alikuwa na nia nzuri japo alikosea. Kuendelea kumlaumu Magufuli haisaidii kwa kuwa hamtampeleka mahakamani! Tafuteni areas ambazo mtakiri kukosea ili watu wawaone mna unyenyekevu. Hiyo ndio siasa.
Give CCM a run for their money, wamezoea mteremko. Waahidi Tanganyika serikali yao, na Zanzibar mamlaka zaidi ya serikali ya Zanzibar, mtaona matokeo!
Nawasaidia Chadema kwa kuwa nimekatishwa tamaa uongozi ambao unapewa taarifa waziri wako kapiga hela kiuhakika hapa wizarani halafu unachofanya ni kumhamishia wizara nyingine, kwa kuwa tu huyu mtu ni mzuri katika kujieleza! Kwa nini asikabidhiwe kwa Takukuru kama kweli uko serious na ufisadi?