Mkuu
CHASHA FARMING hii ndio miundo ya mikataba walioiona fursa ya kuwatumia wakulima kwa kujua tatizo letu kubwa ni soko
Wasome hawa na ukivuna hizo pilipili hawana habari na hasara wakati wameisha kuuzia madawa na mbolea yao "maalumu"
*GHARAMA MUHIMU ZA KILIMO CHA MKATABA, ZAO LA PILIPILI KICHAA, NA MAKARU AGRO LIMITED, TANGA, TANZANIA*
*Kilimo hiki kama kampuni ya makaru AGRO limited, cha mkataba tumekianza mwaka juzi (2018) AUGUST, Na kwa sasa tuna wakulima Tanga, Dar, Morogoro, Mbeya, songwe, Moshi Na Arusha, Mwanza, Njombe, Songea, Bukoba Na maeneo mengine*
*Ni baada ya kuanza kuzalisha kisha kama kampuni kutokana na kupata quality nzuri iliyopendwa Na nchi kama Kenya (ambaye ndo tuliingia nae mkataba wa kwanza August 2017), Sudan Na India kuchukua sample Na wakaipenda. Kisha wakaomba mZigo mkubwa zaidi ya tani 5.5-39 kwa Mwezi wakati kama kampun peke yetu hatuwezi kufikisha kutokana na eneo tulilokuwa nao Na changamoto kubwa ya vibarua tuliyokumbana nayo mkoani Tanga*
*Ikawa kama kampuni tunahitajika kuwa Na wakulima wadogo wadogo katika mkoa wowote wenye eneo lenye maji, Na wenye eneo pia lisilotoamisha maji Na wenye kuweza kulipia gharama za kuwapa elimu, Madawa , Mbolea Na mbegu kuwapa ruhusa kwa kuwapa mkataba ili walime kisha tutaenda kununua kwao ili kuweza kufanikisha order hizo kubwa.*
*Kumbuka kilimo hiki cha kimataifa, Mkulima anahitaji kutumia Dawa maalumu tu na sio kila Dawa , hata Mbolea Pia ndo maana mambo haya yoote kama kampuni tukayasimamia ili tuweze kupata kile kinachohitajika, Na tunashukuru tayari kuna wakulima tuliowasimamia wamefanikiwa hayo, so far wengi wanatuuzia na store yetu ipo TANGA MJINI, ambapo mizigo kutoka Kwa wakulima wetu hukusanywa mikoani walipo Kwa gharama zetu mpaka tanga, ambapo hupack Na kusafirisha nje*
*Tumefanikiwa mpaka sasa kuwa Na wakulima japo bado tunahitaji wakulima.*
*Kwa Mkulima yeyote Yule ambaye atapenda kujiunga mlango bado upo wazi kikubwa aangalie gharama Hizi vyema kama ataweza. Kisha utanitafta Kwa ajili ya kuanza Na ukifanikiwa kuanza tu utawekwa pia katika group la wenzio walioanza tayari*
*Awamu ya kwanza:-*
*TUNAITA AWAMU YA UANDAAJI KITALU MAANA UTAPEWA ELIMU YA KITALU*
kuna kuwapo Na gharama hizi:-
1. Mbegu ekari moja 150,000/-
2. Madawa 50,000/-
3. Visits 135,000/-
*Jumla kama 335,000/-*
Hiyo namba 3 itabadilika kutokana Na eneo. Mfano mbeya sio 135,000 ni 290,000/- ila Moshi, Dar, Morogoro, Arusha koote ni hiyo 135,000/-
Kisha tutakutembelea awamu ya kwanza Na vitu vifuatavyo:-
1. Mkataba
2. Kitabu cha kuweka kumbukumbu
3. Kitabu (katasi mbili) cha kumsaidia kufanya revision
4. Mbegu
5. Dawa ya wadudu (mills 100) Kichupa kimoj
6. Dawa ya ukungu, fungal and other infection (1kg).
Awamu ya kwanza Na ya pili inatenganishwa Na siku 30-45
Then awamu ya Pili
Tunaita awamu ya kuhamisha:-
Utalipia gharama Hizi:-
1. Mbolea 2 kg @ 25,000/- 50,000/-
2. Pesticides 500 mills 125,000/-
3. Fungicide 2 kg @25,000/- 50,000/-
4. Visits 135,000/-
*Jumla kama 360,000/-*
Hapo tutakufanyia design ili miche iingie mingi, pamoja Na kutoa elimu ya kuhamisha ikiwa ni pamoja Na kuangalia maendeleo ya kitalu. Na utafunzwa namna ya kuweka kumbukumbu Na kuweka dawa.
Utakuwa free kupata utaalamu kila mara unapohitaji pamoja Na kushare Na wenzako walioanza mwaka jana. Ambao washaanza kuvuna. Tukija tunakuja Na hizo Dawa Na Vitu vyoote ulivyolipia.
Awamu ya pili kwenda ya tatu ni baada Ya siku 30-45 pia
Awamu ya tatu
1. Mbolea 2 kg @ 25,000/- 50,000/-
2. Pesticides 500 mills 125,000/-
3. Fungicide 2 kg @25,000/- 50,000/-
4. Visits 135,000/-
*Jumla kama 360,000/-*
Haina tofauti Na awamu ya pili.
Kwa ufupi Madawa utakuwa ukilipia Na kuchukua kwetu kila yanapokuishia.
Tunaita awamu ya kukausha. Hapa tukija utapata elimu ya namna ya kujenga nyumba ya ukaushaji, Pamoja Na namna ya kuvuna Na kukausha Na kuhifadhi kwa ujumla.
NB:-
*1. KUHUSIANA NA GHARAMA*
*_GHARAMA HIZI ZINAWEZA KUONGEZEKA HASA KATIKA MBOLEA NA MADAWA, MAANA MPIGA DAWA NA MUWEKA MBOLEA NI MKULIMA PEKE YAKE NA ENEO LAKE_*
*2. KUHUSIANA NA MAVUNO*
*_MKULIMA ATAVUNA MFULULULIZO BILA KUPUMZIKA KWA MIAKA MITATU, MAVUNO KWA MWEZI YANAWEZA KUFUATA MAKADIRIO YETU, YANAWEZA KUONGEZEKA ZAIDI AU YAKAPUNGUA KUTOKANA MA WAVUNAJI, HALI YA HEWA, AU SABABU NYINGINE ZA KIMAZINGIRA_*
*KuanZia hapa mwezi wa tatu ndipo utapoanza kuvuna KAMA UNA VIBARUA WA KUTOSHA UNAWEZA KUVUNA KUANZIA KILO 1000 ZILIZOKAUSHWA (Sawa Na kilo 2000 mbichi, sawa na vibarua 10 ndani ya ekari moja kila mmoja kuvuna kilo 10 Mbichi kisha kilo moja unampa kuanzia 285-500/- lNDANI YA MWEZI UTAKUWA NA TANI MOJA ILIYOKAUSHWA AU ZAIDI NA SISI KILO MOJA TUTANUNUA KWA 3500/- UTAPATA 3,500,000/-*
*3. KWA UFUPI IPO NAMNA YA KIPEKEE YA SISI KAMA KAMPUNI KUKUHUDUMIA KIMKATABA, ILI TUWEZE KUNUNUA LAZIMA UKUBALIENI NA KUTEMBELEWA AWAMU TATU NA UFUATE MAELEKEZO YETU PASI NA KUJALI KUWA UNA MTAALAMU WAKO, KAMA ILIVYOAINISHWA KATIKA MKATABA*
*MAVUNO HAYA HATUJAKADIRIA TUNALO SHAMBA NA TUMEONA KWETU*
*Kwa mawasiliano zaidi namna ya kujiunga piga simu hapa*
0652359818
0767359818
*Mwl Abuu*
MAKARU Agro Limited
P. O box 1805,
Tanga,
Tanzania
*Endapo yoote yaliyopo hapo juu umeyaelewa Tuma ujumbe kukiri umeelewa Na upo tayari kuanza, utapata invoice ya awamu ya kwanza,utayolipia ndani ya siku mbili, kwa ajili ya mbegu, madawa, Na kutembelewa Na baadhi ya document muhimu*
*NJOO ULIME NA WANAOLIMA PIA KWA GHARAMA NAFUU NA SOKO LA UHAKIKA, ACHANA NA MADALALI*