Si KWELI kwamba Kiba& Diamond ndio wasani pekee Tanzania

Mwinjilist mtume nabii

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2015
Posts
2,437
Reaction score
1,097
Bwana Yesu asifiwe!!!

Watu wengi wameshindwa kupambanua na hatimaye kutengeneza Upinzani kwa wasanii wawili A. Kiba na D. Platinum kana kwamba ndo wasanii maalum na ndo wenye vipawa vya kuimba hapa nchini kuliko wasanii wengine.

Na nilichogundua kwa vijana wengi mashabiki wa wasanii hao,,,,,Si kwamba wanashabikia ubora wa uimbaji wa wasanii hao,,,bali maisha ya wasanii hao kwa ujumla pamoja na mali wanazomiliki.

Tukiangalia malengo ya sanaa/muziki lengo kuu ni:

1. KUELIMISHA JAMII-- Ambapo hili ndilo linastahili kuwa la kwanza. Lakin kwa wasanii hao hakuna aliyefikia lengo hili,,,hivyoo nyimbo zao wala HAZIWEZI kusimama kama icon ya Taifa.

2. BURUDANI--- hii ni lengo la pili la muziki au sanaa,,,,,ambalo halina nguvu sana kama lile la kwanza. Na hapa ndipo wasanii wengi walipojikita pamoja na hao. Wanaimba kama burudani tuu na wala c kuisaidia jamii.

Sasa kwa mantiki iyo,,,,,Msanii anaeimba nyimbo ya Kuelimisha Jamii ndiye anaestahili kuwa juu kuliko anaeimba za kuburudisha jamii. Lakn cha ajabu watu hawataki kujipanua na hatimaye kutengeneza upinzani kwa wasanii Hao wawili"" Kiba na D.Pltnum lakn zaidi wakiwalinganisha maisha yao kwa ujumla.

Mm kama Mchungaji nakataa ""Hao c wasanii pekee hapa nchini kwa kuzingatia nyimbo zao"" na maudhui za nyimbo zao ikiwa wapo wanaoimba "Ujumbe"" na mashairi yanayoeleweka,,,,nyimbo ambazo zinaweza hata tafsirika kwa lugha nyingine za kigeni kwa urahisi kabsa.

Kwaiyo mnaweza kuwagawa wasanii sasa ktk makundi mawili.
1. Wanaoimba kuelimisha jamii
2. Wanaoimba kuburudisha jamii.

Mm kama Mchungaji nashauri tuwe watu wa kupambanua mambo kuliko kjiingiza ktk ushabiki ukiwa hata sbb au hoja ya msingi.

MUNGU WABARIKI WASANII WETU UKAWAPE UFUNUO ZAIDI ILI WAKAONE MAHITAJI YA JAMII NA TAIFA Kwa Jina la Yesu Kristo.
Amen
 
Kwani wanaoimba gospel vp hailipi mbona umepotea njia nilijua unaongelea C Shushu v R Muhando maana huko ww ndio kunakuhusu huku bongo fleva umefuata nn au na wewe unasikiliza nyimbo za shetan umeacha za Mungu na kwamba umehasi imani???
 
Mchungaji naye anasikiliza bongo flavour tena anafuatilia kabisa
Kweli Diamond na Kiba wanabamba.
 
Nilicho furahi ni kuwa jamaa wana fanya kazi mpaka pastor unawajua, big up dimond na AK .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…