Si Nyerere bali ni Mseven ndo alimlipua Oyite-Ojok

Si Nyerere bali ni Mseven ndo alimlipua Oyite-Ojok

MkamaP

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2007
Posts
8,146
Reaction score
3,235
Corbis-U1962997.jpg

On December 3, 1983, a helicopter crash in central Uganda claimed the life of Obote's feared Commander, Maj. Gen. David Oyite Ojok.FRED GUWEDDEKO reports that after the crash, the Yoweri Museveni-led rebel NRA issued a tough statement, saying there were no tears to shed for Oyite because he was a victim of his crimes.


However, fast forward to January 26, 2010, Oyite Ojok was named among the "NRM heroes" during celebrations to mark the 24th NRM anniversary in Mbale.

Earlier in 1979, President Museveni and Oyite Ojok had led the two Uganda armed groups (Kikosi Maluum and Kikosi Vita) that together with the Tanzanian government forces overthrew Idi Amin.

Museveni and Oyite Ojok, using their armies, were again instrumental in ousting the post-Amin presidents, Prof. Yusuf Lule and Godfrey Binaisa in 1979 and 1980. When Museveni went to the bush to start a guerrilla war in 1981, it was Oyite Ojok's assignment to protect the government of Apollo Milton Obote.

Oyite.jpg

His sudden death was therefore seen as a turning point in the guerrilla war in NRA's favour.
With the threat out of the way, the NRM can afford to play the reconciliation card. It is indeed difficult to tell whether the real feelings of the NRA/Museveni towards Oyite Ojok are to be found in his recent declaration as a hero, or the callous press release that was issued after his death.

Below is the statement reportedly issued by the NRA on December 6, 1983.

Oyite Ojok death explained

National Resistance Army
Headquarters

6th December, 1983

Oyite-Ojok.jpg

So many lies have been told by the UPC regime about the death of their principal murderer, Oyite-Ojok, that it is really pointless to go on arguing with these gentlemen because they are shameless and incorrigible liars. After all, what does one expect of people who stole gold in 1966, or who usurped reins of government in both 1966 and 1980?

Whether Ojok was shot down by the NRA, was bobby-trapped by his own colleagues due to in-fighting, or quarrels over business deals, was bobby-trapped by ordinary soldiers who are being used by UPC as cannon-fodder while the UPC war-chiefs are downing champagne in Nile Mansions, or the reckless overuse of the machines (the helicopters) brought about the disintegration of Ojok's helicopter, or whether it was God's punishment for his numerous crimes, it all amounts to the same thing: that a leading murderer of hundreds of thousands of civilians in Luwero, Mubende, Mpigi, West Nile, Madi, Mukono and Kampala, has finally perished by the sword he has been using to kill Ugandans.

The murderer of Katambwa, Busabala, Nateete, has got his more than deserved punishment; the murderer of his fellow officers; Lt. Col. Ndahendekire, Lt. Col. Ruhinda, Lt. Col. Oboma, Lt. Karenzi, to name only a few, has come to the same end to which he brought so many innocent people in Uganda.

The lies of UPC notwithstanding, it is our duty to tell the world what happened on the 2nd of December 1983 and the week preceding that date:

On that day: Three helicopters were frantically and stupidly flying over the battle-field of Ngoma area. They would fly over the various river-crossings where our forces were either stationed, or in the vicinity, e.g. Wankaka, Birima, Nyakashangazi, Bulyamishenyi (all in Luwero district), and then proceed to Kyankwanzi (Mubende district), in addition to calling on the enemy detachments at Kasozi, Wankaka, Katundu, Kijunjubwa (Masindi district), and Kyankwanzi.

The NRA has got many units in the area of Ngoma, Wakyato and Singo over which the three helicopters were flying. All these forces have got orders to shoot down any helicopter if it comes in on a low altitude.

These helicopters were dropping leaflets for the guerillas to surrender and were directing and co-ordinating the latest enemy offensive against us. They were not "visiting" troops as we were told by Radio Uganda. We have got irrefutable proof of this.

On that day, Ojok brought some Katyusha and 122 mm howitzer, in the area of Kyankwanzi and Kyakamunywero, etc. The orders to UPC troops were to advance on the 3rd of December from all fronts in one more useless offensive.

One week previously: The same Katyusha, 122mm howitzers and 14.5 mm AA guns had supported Obote soldiers who crossed from Kasozi to Ngoma side and dug in. Later on, they tried to advance further and they were given a nasty blow, which forced them to go back to their defence near the river bank.

There, they stayed without moving. It seems Ojok, knowing their reluctance to go on with the war, had come to urge them on. That is why his three helicopters spent the whole of the 2nd December 1983 flying desperately around the battle-field.

In criss-crossing the battle-field, one of the helicopters attracted fire from our forces in Biduku area. It, however, flew on towards Kasozi. Then around 8.00 p.m., our soldiers who were on the Ngoma side of Kasozi heard the helicopter take off in darkness; then, after a short while, saw a spark of fire on the flying helicopter which was quickly followed by the fire engulfing the whole helicopter and the whole helicopter came down burning until it thudded to the ground - just 3 kms from where our soldiers were. We think that the fire of our soldiers in Biduku must have caused some damage which eventually resulted in the crash of Ojok's helicopter.

This is not the first time we have shot down Obote's helicopters in the same way: In September, our forces in Nshaka area shot down another helicopter which went and crash-landed behind the enemy lines. We have got irrefutable evidence of all these facts.

It is high time the international community knew the Obote clique for what they are - liars. In July we destroyed an enemy battalion at Luwero; afterwards one of the UPC officials said that Luwero had been destroyed by a "storm"! What else can one expect from the UPC regime?

The people of Uganda, however, know the truth about the UPC regime. As for us we shall go on delivering blows on the UPC regime until they either grant the democratic and human rights of the people of Uganda or they are put on the dung-heap of history.

Moreover, we are no longer going to show lenience to the crimes of UPC leaders - especially genocide against some of the peoples of Uganda - (especially to the authors of these crimes). Our lenience to the UPC leadership has given too much license to these thugs to murder our people, from the security of Nile Mansions.

This Ojok died after, indeed, supervising the murder of 28 Ugandans at Nyekashagazi, 8 at Wankaka and 8 at Kyabalango - all innocent civilians who were trying to flee the war to Buruli. Justice caught up with him as he was taking off to Kampala and the pleasures of the Nile Mansions and the weekend.

He thought that it was a picnic to murder Ugandans and come back to his own family and a happy weekend. As to Ojok's contribution to the anti-Amin cause, the record should also be set right:

Firstly, it was Obote and Ojok, who groomed Amin in the first place, until they quarreled over the loot of office. Secondly, Amin is no worse than Obote and Ojok. In fact, Amin confined his killings to the middle-class only; he never murdered peasants, a job at which Obote and Ojok have more than excelled.

Thirdly, in the anti-Amin struggle itself the Obote-Ojok clique spent more time creating problems for the resistance than assisting it. For instance, in the 1972 debacle, the Obote-Ojok mistakes caused the death of 500 anti-Amin fighters between the 17th and 18th of September 1972.

After the 1979 fall of Amin, the Obote-Ojok clique nullified the gains of the democratic forces by their plot to usurp power and turned the UNLA into a corrupt, murderous and thieving group that unroofs people's houses, rapes women and murders numerous civilians.

Again we have got incontrovertible evidence of this. Therefore, we condemn the role of Oyite-Ojok in the 1966 crisis, in the ensuing tribalisation of Uganda Army before the Amin take over, and in the confusion created by Ojok and Obote in the anti-Amin forces in Tanzania between 1971-79.

We also condemn his criminal activities ever since the l979 illegal recruitments into the UNLA, murders in various parts of Uganda already enumerated above, and the transformation of UNLA from an army of liberation into a repressive and corrupt force.

The bankruptcy of the Ojok military clique is shown by the stupidity with which they were criss-crossing the battlefield as if they do not know that a helicopter can be shot down with even a semi-automatic rifle, or a G-3, or even the hunting .375, not to mention LMGs and MMGs, all of which are used by the NRA.

Further, the bankruptcy of the UPC regime is shown by the worship of Ojok by the UPC. Ojok, a mere "chief" of "staff" which simply means a principal staff officer at headquarters, would take precedence over ministers, not to mention the chief-of-defence, Tito.

This was all because there is nobody in UPC who had got an idea as to how to run an estate, or how an army should he organised.

Ojok was, of course, taking advantage of this for his own ambitions which had been partly responsible for the conflict between Obote and Amin that cost Ugandans so much and for the disintegration of the old Uganda Army, and whatever little professionalism it was beginning to acquire.

Yoweri K. Museveni,
Chairman of High Command,
NRA
 
Uganda noma. Ndo maana Museveni hataki kuachia madaraka.
 
Historia ya Major-General David Oyite-Ojok
Major-General David Oyite-Ojok alizaliwa April 15,1940 huko Loro wilaya ya Lango,alimaliza shule ya msingi katika shule ya Loro aliendelea na masomo katika shule ya Nabumali high school huko wilaya ya Mbale kuanzia 1958 mpaka 1962 baadaye alijiunga na Jeshi wakati huo lilijulikana kama Uganda Rifles na mwaka 1963 alipelekwa kusoma Uingereza kwenye chuo cha kijeshi cha Mons officer cadet.na aliporudi alipandishwa na kuwa Luteni usu(Second lieutenant)na alipelekwa huko jinja kuongoza kikosi cha askari wa miguu ambako alitumika kama platoon commander.
Major-General David Oyite-Ojok baadaye 1966 alihamishiwa Fourth Infantry Battalion,Mbarara hatimaye alihamishiwa tena Kampala kuwa mkuu katika ofisi ya mkuu wa utawala Jeshini,baadaye tena alipandishwa cheo na kuwa Army`s Quartermaster General na alienda kusoma huko Uingereza katika chuo cha kijeshi cha Cumberley Staff College na alirudi Uganda 1967.kwa wakati ule kwa cheo alichokuwa nacho na kwa kuwa alikuwa Mpwa wa Rais Obote alikuwa mtu mhimu sana katika Uganda.
Major-General David Oyite-Ojok alimuoa Rebecca Ojok na alikuwa na ndugu waliokuwa jeshini mmoja wapo ni Lt Col Martin Okech aliyekuwa katika jeshi la anga la Uganda kipindi hicho Idd-Amin na David Oyite-Ojok walikuwa marafiki sana na waliheshimiana ingawaje kila mmoja alimuona mwenzie kuwa kama anaheshimiwa sana jeshini kuliko mwingine,lakini wote walikua maarufu sana Jeshini kuliko mtu yeyote.Kwa upande wa David Oyite-Ojok alijiona yeye kuwa ni Kamanda mkuu mtarajiwa katika jeshi la Uganda na alijiona hana mpinzani isipokuwa Idd-Amin pekee, Hivyo kwa kutumia ukaribu aliokuwa nao na Rais Obote aliweza kuingiza mambo ambayo yangemharibia sifa Idd-Amin kwa Rais Obote hata hivyo Rais Obote hakuona tatizo lolote kwa Idd-Amin
Katika tukio moja lililotokea katikati ya 1960 Oyite-Ojok wakati huo akiwa Lieutenant-Colonel aliwakilisha repoti ya uchunguzi ikimtuhumu Idd-Amin kwa kupanga njama za kumpindua Rais Obote,Ripoti hiyo ilimfanya Rais Obote aamuke toka usingizi dhidi ya Idd-Amin na akataka ushauri toka kwa Oyite-Ojok ni njinsi gani atamdhibiti Idd-Amin hapo ndipo Oyite-Ojok alipata fursa ya kummaliza Idd-Amin kwa kumwambia Rais Obote amwachie kazi hiyo yeye.Oyite-Ojok alipanga mpango wa Kumkamata Idd-Amin lakini mpango huo ulivuja na Idd-Amin alipata habari na hapo hapo alivaa mavazi rasmi ya Kijeshi na akabeba Pistol mbili na kuelekea kwenye majengo ya Bunge iliko ofisi ya Rais Obote akiwa amevalia Kijeshi(Full battle fatigues)na aliweza kuongea na Rais lakini haikujulikana ni nini aliongea na Rais Obote.
Baada ya tukio hilo 1969 Oyite-Ojok alibuni mpango mwingine wa kumuua Brig.Okoya na kusukuma lawama zote kwa Idd-Amin,Oyite-Ojok alimchukua Capt Okoth wa kikosi cha polisi wa Jeshi pamoja na Capt.Fredrick Guweddeko na Lt.Kasule Lutalo ambaye alikuwa anafanya kazi katika kituo cha anga cha Guru wanajeshi hawa waliteswa sana ili waweze kukiri kuwa Idd Amin alihusika katika mauaji ya Bri.Okoya lakini wanajeshi hao walikana kabisa kumhusisha Idd-Amin na mauaji hayo hivyo kulipelekea wao kutupwa Gerezani huko Luzira.
Baadaye ililipotiwa kuwa Oyite-Ojok aliwatembelea huko gerezani na kuwacheka kwa kuacha kuitumia hiyo nafasi kumkandamiza Idd-Amin hivyo walipoteza nafasi ya kupandishwa vyeo pamoja na kupata kitita kikubwa cha pesa walichoahidiwa kupewa ikiwa tu wangeliweza kumuunganisha Idd-Amin na mauaji ya Brig.Okoya na aliwaambia wakae waozee humo gerezani.
Baadaye katikati ya Dec.1970 Oyite-Ojok alijaribu mpango mwingine wa kumtia hatiani Idd-Amin,Siku moja usiku Oyite-Ojok aliendesha gari lake aina ya Mercedes Benz kuelekea kwenye kambi ya kijeshi ya Malire na alichagua askari wa ngazi za chini 12 na wote walipangwa karibu na lango kuu la chuo kikuu cha Makelele na wengine walipangwa Balintuna road huko Namirembe lwenye vilima vinavyotazama jiji la Kampala,Askari wote hao walikuwa wanatoka katika kambi ya kijeshi ya Malire,Oyite- Ojok aliwapa maagizo waangalie gari aina ya Peugeot 403 iliyokuwa na Antena mbili maalum za kijeshi aliwaagiza kipindi watakapoiona walimiminie risasi bila kusita.
Wakati askari hao wanasubiri hiyo wale askari waliokuwa wamewekwa kwenye lango kuu la chuo kikuu cha Makelele walianza kuulizana kuhusiana na lile gari walilopewa amri kuliangalia na baadaye kulimiminia risasi walijua ni lile gari la mkuu wa Majeshi Major General Idd-Amini maana hakuna gari aina hiyo yenye Antena mbili maalum za kijeshi nchini Uganda isipokuwa ni ile ya Idd-Amin,Askari hao walijiuliza kwa nini Oyite-Ojok anataka kumuua Idd-Amin na kwa nini anataka kushirikisha wanajeshi katika kitendo hicho?Askari hao walipeana habari na wakaamua kutotekeleza amri hiyo ya Oyite Ojok wakikumbuka kwa yale yaliyowatokea wenzao waliokuwa wamefungwa kenye gereza la Luzira.
Wakati wanajadiri hayo ghafla gari tajwa likaonekana likiwa na antenna maalum mbili za kijeshi likitokea Barabara ya Makelele kuelekea Nakulabye ilikuwa saa 8 usiku na Idd-Amin alikuwa akiendesha peke yake bila Bodyguard,Amin aliwaona askari wawili barabarani akasimama akawauliza kwa nini wanafanya ulinzi eneo la chuo kikuu cha Makelele??Mmoja wao alimjibu Kuwa hata wao walikuwa wakijiuliza usiku wote na Idd-Amin aliwapakiza kwenye gari yake na kuwaondoa katika lindo hilo wakati wakiwa ndani ya gari ya Idd-Amin waliendelea kumsimulia njinsi Oyite-Ojok alivyowapa maagizo ya kumuua,Idd-Amin aliapa mapumziko ya siku 14 askari wote waliokuwa kwenye mpango wa kumuua.
Asubuhi yake Oyite-Ojok alijuwa wazi kuwa mpango wake wa kumuua Idd-Amin umeshindwa na yeye kwa cheo chake hana mamlaka ya kuwaadibisha askari hao,hivyo kulimweka katika hali mbaya kwa jamii na kwa hasimu yake Idd-Amin
Hatimaye Rais Obote alikwenda kwenye mkutano wa Commonwealth huko Singapore Idd-Amin alipata wasaa mzuri na aliweza kutekeleza mapinduzi ya kijeshi January,25,1971 wakati huo Oyite-Ojok alikuwa kwenye majengo ya Bunge na aliponea chupu-chupu kukamatwa na askari waliokuwa eneo hilo hivyo alitimkia kusikojulikana.
Kesho yake Mwambata wa kijeshi wa Israel nchini Israel Col.Baruch Bar-Lev aliwauliza askari watiifu kwa Amin kama Oyite-Ojok amekamatwa au ameuwawa,lakini walipomjibu kuwa hajulikani wapi alipo Bar-Lev alisema mapinduzi hayo hayakufanikiwa,Mwambata huyo alisema hivyo kutokana na umaarufu aliokuwa nao na mafunzo aliyokuwa nayo Oyite-Ojok alikua na Imani ya kuwa na uwezo wa kutengua mapinduzi hayo.
Baada ya mapinduzi hayo ya January 25,1971 Oyite-Ojok alikimbilia Sudani kusini kupitia Adjumani na alienda kwenye sehemu iliyojulikana Owiny Kibul,hakuweza kusafiri mara moja kwenda Tanzania.Akiwa kwenye mji wa Owiny Kibul alianza kuwakusanya askari ili baadaye waanze mapambano ya kumtoa Idd-Amin madarakani.
Wengi wa askari aliowapa mafunzo ya kupigana vita kumuondoa Idd-Amin madarakani walikufa wakio bado kwenye kambi za mafunzo huko Sudan kusini,lakini baadaye walihamishiwa Masange Tabora na wengine Morogoro na wengine Nachingwea Tanzania,kwa msaada wa serikali ya Tanzania walipewa sehemu nzuri na silaha.
Katika mwaka huo 1971 akiwa askari wa msituni Oyite-Ojok aliweza kusafiri na kwenda Kampala na Sudan kusini kwa kutumia passport ya Sudani alikuwa kila mara anafikia kwenye hotel ya Soweto,vilevile alikuwa na kikosi maalum kilichokuwa kinamiliki mashua inayokwenda kwa kasi katika ziwa Victoria ambayo ilikuwa na uwezo wa kufika katika maeneo yote ya Uganda kupitia ziwa Victoria. waliweza kuteka silaha toka majeshi ya Amin ambazo walizificha huko Mayunge,mbarara Uganda ambazo baadaye walizitumia katika mapambano ya kumtoa Idd-Amin.Alishiriki kikamilifu katika vita vya kagera akiwa katika Kikosi Maalum(Special Force) akiwa na Tito Okello Lutwa na Kaguta Mseveni

Katika mwezi huu wa December ulimwengu ulikuwa ukiomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika kusini ambaye alikuwa alama ya mapambano ya kupinga ubaguzi wa Rangi,Na miaka 30 iliyopita mwezi huu wa December Uganda walipoteza mmoja wa mashujaa waliokuwa wanaongoza, kiongozi huyo alijulikana kwa jina la Major-General David Oyite-Ojok aliyekuwa mkuu wa utawala jeshini aliyekuwa taa ya kuongoza katika mapambano ya kumng`oa Idd-Amin.
Ilikuwa jumapili December 2,1983 helicopter iliyokuwa imembeba Major-General David Oyite-Ojok ilianguka katika kijiji cha Kashozi Wilaya ya Nakasongola alikoenda kukagua mapambano na waasi wakati huo waasi walikuwa wakiongozwa na Yoweri Kaguta Mseveni.
Kifo chake kilileta mshituko mkubwa kwa Taifa, Major-General David Oyite-Ojok alikuwa ni mtu wa mwisho kwa Waganda kumtegemea kufa kwa wakati huo na kwa ajali kama hiyo.maana toka vita vya kumng`oa Idd-Amin Major-General David Oyite-Ojok alionekana kuwa shujaa na watu wengi wakiwemo askari wa Tanzania waliopigana vita vya kumtoa Idd-Amin katika ardhi ya Tanzania na hatimaye kumng`oa katika madaraka,alionekana kuwa kiongozi wa kijeshi mwenye nguvu pia kulikuwa na uvumi kuwa alikuwa na nguvu kama Rais Obote na kumzidi aliyekuwa makamu wa Rais wakati ule Paulo Muwanga.
Baada ya kifo cha Major-General David Oyite-Ojok nchi iliingia kwenye maombolezo ya kitaifa,Radio Uganda na Television viliendelea kutoa salamu za rambi-rambi kwa Rais na Makamu wake na waziri mkuu wakati huo Otema Alimadi na kwa serikali nzima ya Uganda kulikuwa na makundi makubwa ya watu huko Kampala,Lira na miji mingine walionekana wakiomboleza kifo cha shujaa huyu.
 
ndiye Yule aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar?
 
Tunashukuru kwa historia kaka, ila ile sehem ya tatu ya Vita ya Kagera vipi?, maana bado tunaisubiri.
 
Hebu tupe na historia ya Huyo aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar, maana wengi wanatuchanya na historia imeshindwa kuweka waz. Thanx
 
Hebu tupe na historia ya Huyo aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar, maana wengi wanatuchanya na historia imeshindwa kuweka waz. Thanx
Wakati Tunasherehekea siku ya mapinduzi Zanzibar yaliyofanyika January 12,1964,Mapinduzi hayo ya Zanzibar yamenifanya nimkumbuke Mwanamapinduzi Field Marshal John Gideon Okello aliyetoa mchango mkubwa katika mapinduzi hayo yaliyoleta Ukombozi wa Zanzibar pamoja na kwamba walikuwa na zana duni sana,Field Marshal Okello aliweza kuwashtukiza polisi na waliweza kuchukua madaraka.
Field Marshal Okello hakupaswa kusahaulika katika nchi zote mbili yaani Uganda na nchi aliyoikomboa ya Zanzibar,Kitu cha mhimu sana jamaa na ndugu za Field Marshal Okello wanaishi katika maisha ya ufukara na umaskini mkubwa sana wakati wa vita vya Kagera nimewahi kufika katika kijiji chake alikozaliwa na baadhi ya Wanajeshi tuliokuwa nao tulipenda sana kuwaona ndugu na jamaa za Mwanamapinduzi huyo.Tuliweza kufika katika kijiji cha Iyama huko Moroto, Tuliikuta familia ya Field Marshal Okello inaishi maisha ya kimaskini kabisa Utafikiri familia hiyo haijafanya chochote tulikaa pale kwa siku nzima na mimi nilibahatika kupata kitabu alichokiandika field marshal okello kiitwacho Revolution in Zanzibar kitabu hicho kinaelezea mengi sana kuhusiana na mapinduzi hayo ya Zanzibar kuna sehemu field marshal john okello aliandika; , " I understand African thinking and I understand that what I did in Zanzibar, had it been done in any other country for the sake of Africans, I would still have been judged wrong and borne blame. But I acted alone during the revolution and had to remain alone afterwards. If anyone can claim he was with me during the planning and thinking through of the Revolution, let him come forward and explain it" Okello then went on by saying that " Only God almighty knows what went on in Zanzibar. If anyone claims to have trained me or taught me to act as I did, let him come forward and describe it. I had been an ordinary worker in Zanzibar and went originally to work. A man of class and limited education certainly could not have gone abroad easily and why should I have known by or been acceptable to, and nothing proves this more than the wild claims made about me after the revolution and yet no one knew anything about me at all. I was reported to be a jaluo man from Kenya and a former member of Zanzibar police, yet a check of records in Zanzibar would not reveal my name on any police employment rolls, other people claimed they had seen me in Cuba and in Cairo and in some socialist countries. But there has been any evidence to refute any claims that I have never been outside East Africa to assert that I was an agent of some power, is foolish. How would anyone known I could manage revolution? And why did no one know me after the revolution?
God alone knows and still knows what is happening with me. He is my teacher and whatever he taught me about revolutionary activities is within me and no one on earth can discern it. My power in regard to the revolution was as a messenger of God, and God alone helped to master and eradicate the imperialists on the Island. Tulipigwa na butwaa kuona familia ya mwanamapinduzi huyo kuishi maisha kama hayo ya shida wakati yeye alifanya kazi kubwa ya ukombozi wa Zanzibar
Historia yake
Field Marshal John Gideon Okello alizaliwa mwaka 1937 huko wilaya ya Lango sasa hivi ni Lira Alipokuwa kijana ni mambo machache sana yanayofahamika kuhusiana na maisha yake hata hivyo Field Marshal John Gidion Okello alikuwa Mkristo na alibatizwa akiwa mdogo na jina lake la Ubatizo aliitwa Gidion,alipofikisha miaka 11 wazazi wake walifariki na alilelewa na ndugu zake wa karibu.
Alipofikisha miaka 15 alianza kutembelea nchi mbali-mbali za Afrika mashariki kutafuta kazi na kuna wakati alifanya kazi ya ukarani na kazi za nyumbani na shambani,pia alifundishwa kazi ya kutengeneza matofari ya kuchoma,kuna kipindi alikamatwa na Polisi huko Nairobi,Kenya sababu haikujulikana na alifungwa miaka miwili na katika kipindi hicho alipendezwa sana na Fikra za kimapinduzi vile vile kulikuwa na fununu kuwa Okello alikuwa ameishi Cuba na alifundishwa Ukominist na Fidel Castro
Mwaka 1959 aliondoka na kuelekea Pemba ambako alijaribu pia kutafuta kazi katika shamba moja,lakini badala yake alipata kazi ya Polisi na mwaka huohuo alijiunga na chama cha Afro-Shirazi cha Sheikhe Abeid Karume na akawa mwanaharakati shupavu aliweza pia kuwakusanya vijana na kuwaunganisha ili kupinga unyanyasaji wa waarabu huko visiwani. chama hiki kilikuwa kinapinga ukiritimba wa waarabu katika visiwa vya Zanzibar na Pemba.
Mwaka 1963 Okello aliondoka Pemba na kuelekea Zanzibar, Ambako alikutana na viongozi wa vijana wa Afro-Shiraz Umoja huo wa vijana wa Afro-Shiraz ulikuwa na mikakati ya kufanya mapinduzi ili kuondoa nguvu ya Waarabu huko Zanzibar,Okello pia alikuwa mwanachama wa chama cha wapaka rangi majumba maana naye siku ambazo hakuwa na kazi ya kufanya alikuwa anafanya kazi ya kupaka majumba rangi pia aliunda kikosi kidogo cha wazalendo kilichokuwa kinadhamini U-afrika kikosi hiki kilikuwa na miiko ya kutofanya mahusiano na wanawake,Kutokula nyama na kutokunywa pombe
January 12, 1964,akiwa na kikosi chake cha watu zaidi ya 600 Kwa kuungwa mkono na jamii ya visiwa waliokuwa wananyanyaswa na waarabu,Okello na kikosi chake walipigana kuelekea mji mkuu wa Zanzibar ambako Sultan alikuwa akikaa pamoja na kwamba walikuwa na zana duni,Okello na kikosi chake walilishtukiza Jeshi la Polisi la Zanzibar na kuweza kuteka silaha nyingi na ghala la silaha lilikuwa chini yao hivyo waliweza kuchukua madaraka,Wakati wa kutangaza mapinduzi hayo kwa njia ya Radio Okello alijitangaza mwenyewe kuwa yeye ni Field Marshal wa Zanzibar na Pemba na alimpa Sultan Amri ya kuwauwa familia yake na baadaye ajiue yeye mwenyewe la sivyo Okello angewauwa yeye mwenyewe,Hata hivyo Okello alikuwa amechelewa maana Sultani alikuwa amekimbilia kwenye meli ya Uingereza lakini waziri mkuu na mawaziri wengine hawakuweza kutoroka walikamatwa na walifungwa miaka mingi.Katika mapinduzi hayo zaidi ya waarabu 20,000 waliuliwa hasa hasa waliokuwa Zanzibar kati ya January 18 na 20, 1964.
Field Marshal John Gideon Okello aliunda Baraza la mapinduzi na alimchagua kiongozi wa Afro Shiraz Abeid Karume kuwa Rais na Sheikhe Abdulrahman Muhamad Babu kuwa waziri Mkuu,Kipindi hicho Karume na Babu walikuwa wanaishi Tanganyika,Na hawakujulishwa mapema kuhusiana na mapinduzi hayo, lakini walienda Zanzibar baada tu ya kukaribishwa na Okello.
Kuna habari pia kuwa Karume alikuwa anajua kutatokea nini maana alijulishwa na Field Marsha Okello kuwa wanampango wa kufanya mapinduzi hapo 12/01/1964 hivyo aliwataka viongozi wa juu wa Afro Shiraz Party kuondoka Zanzibar ili kama Zoezi litashindikana basi viongozi hao wawe salama na asiwepo wa kuwahisi kuwa walikuwa wanajua njama hizo za Mapinduzi.
Kufikia January 3,1964 Zanzibar ilirudia hali yake ya kawaida na Karume alikuwa amekubalika na jamii kuwa Rais,Field Marshal John Okello aliunda kikosi cha Jeshi kilichokuwa kikiitwa Freedom Military Force(FMF)kutoka kwa vikosi vilivyokuwa vikimuunga mkono ambavyo vilianza kufanya doria mitaani na sehemu zingine mhimu baada ya mapinduzi kupita okello aliweza kusafiri kwenda dar-es-salaam aliporudi alikuta hali si nzuri kwake askari wake walikuwa wameanza kupokonywa silaha hii iliashiria kuchafuka tena kwa hali ya hewa kwa Field Marshal John Gideon Okello.
The People's Liberation Army (PLA)Jeshi la Ukombozi wa wananchi liliundwa mwezi April 1964 na lilikamilisha kazi ya kuwapokonya silaha askari wote wa Okello,Tarehe 26/04/1964 Karume alitangaza kuwa amefanya mazungumzo ya kuingia kwenye Muungano na Tanganyika na kuunda nchi moja ya TANZANIA Haikuweza kujulikana mapema ni nini ilikuwa nia ya Karume kuingia kwenye Muungano huo lakini wengi walisema Karume aliingia kwenye muungano na Tanganyika ili kuwazuia watu wenye siasa kali toka chama cha Umma wasichukue nchi au kupunguza uwezekano wa kuwavutia wakominist katika afrika mashariki. Na wengine walihisi kuwa kwa sababu Field Marshal John Okello na karume kulikuwa na sintofahamu kati yao ndiyo maana aliamua kufanya muungano na Tanganyika ili asichukue madaraka tena toka kwake.kwa ujumla okello alikumbana na shida nyingi sana baada ya mapinduzi hayo.
Tatizo lingine alilopata ni kutokana na Dini yake yeye alikuwa Mkristo na ASP yote walikuwa Waislam hivyo alionekana mbele yao kama KAFIR hivyo hakusitahili kuongoza waislamu, wengine walihisi hivyo ndiyo maana jeshi lake lilipokonywa silaha na wafuasi wa Karume na wale waliotoka chama cha Umma,Na baada ya yeye kwenda Tanganyika aliporudi kwenye uwanja wa ndege Sheikh Karume alimwita Okello na kati ya mambo yaliyozungumzwa ni ya yeye kukataliwa huko visiwani hakuruhusiwa kuongea na yeyote,baadaye mamlaka ya mapinduzi walimzuia kuingia Zanzibar na inasemekana sheikh karume aliongea na nyerere ili naye oangee na rafiki yake obote asimruhusu okello kurudi Zanzibar tena.
Baadaye Okello alikaa Kenya,Congo-Kinshasa mwishowe Uganda alikuwa akizunguka katika nchi hizi mara kwa mara mwaka 1971 alionekana akiwa na Rais wa Uganda Idd Amin baadaye alitoweka maana Idd Amin hakupendezwa nayeye Okello kujiita Field Marshal maana alijiuliza watakuwa ma-Field Marshal wangapi Uganda hata hivyo Amin hakumwamini alimwona kama ni kitisho katika utawala wake hivyo inasadikiwa Idd Amin aliamua kummaliza mwaka 1971 baada tu ya kuchukua madaraka toka kwa Rais Obote.
 
Mkuu Echolima nashukuru sana kwa elimu unayotupatia,God bless you
 
Last edited by a moderator:
hayo mambo ya uislam na ukiristo umechapia.itakua vichekesho (the comedy) Karume akimbie ukristo Okello akajifiche ktk ukristo wa nyerere ha!!haha!!.tatizo Okello alikua mganda si muunguja hana asili unguja wala pemba atukuaje mtawala? mbona elimu hiyo iko wazi.rejea kisa cha nyamlenge M23. kushiriki mapinduzi zaire na kukatiliwa na wazaire asilia kupewa uongozi zaire pamoja na kushiriki kwao kumtoa Mabutu seseko kuku wazobanga
 
Historia ya nchi hii imepindishwa sana. Hivi wanajisikiaje pale wanaposema karume aliongoza mapinduzi matukufu wakati karume alikuwa anakoroma tu kwake huku wenzie wakiweka roho mkononi. Hata kama hakua Mzanzibar, angeweza kupewa namna nyingine ya kuishi badala ya kumtupa kama takataka.

Swali ninalijiuliza mara nyingi ni hili, "Ni lini katika maadhimisho ya mapinduzi itakuja kuelezwa kuwa Okello ndiye aliyeongoza mapinduzi, na kuwakabidhi akina Karume ofisi?" "Ni lini ukweli utajasemwa?".
 
hayo mambo ya uislam na ukiristo umechapia.itakua vichekesho (the comedy) Karume akimbie ukristo Okello akajifiche ktk ukristo wa nyerere ha!!haha!!.tatizo Okello alikua mganda si muunguja hana asili unguja wala pemba atukuaje mtawala? mbona elimu hiyo iko wazi.rejea kisa cha nyamlenge M23. kushiriki mapinduzi zaire na kukatiliwa na wazaire asilia kupewa uongozi zaire pamoja na kushiriki kwao kumtoa Mabutu seseko kuku wazobanga

Mkuu, ndiyo maana jamaa kasema kuwa kuna watu wanahisi kuwa uenda alikataliwa kwasababu ya Ukristo wake. Na inawezekana ni kweli na ndiyo maana historia imepindishwa isijeonekana kuwa aliyeongoza Mapinduzi ni mkristo. Hata kama siyo Mzanzibar na asingeweza kuwaongoza Wazanzibar, basi wasingemfanyia mambo ya upuuzi kama hayo, na je, kwanini hawakumkataa asiongoze kufanya Mapinduzi kwasababu siyo Mzanzibar? Unafiki wa Wazanzibar haujaanza leo.
 
Mkuu, ndiyo maana jamaa kasema kuwa kuna watu wanahisi kuwa uenda alikataliwa kwasababu ya Ukristo wake. Na inawezekana ni kweli na ndiyo maana historia imepindishwa isijeonekana kuwa aliyeongoza Mapinduzi ni mkristo. Hata kama siyo Mzanzibar na asingeweza kuwaongoza Wazanzibar, basi wasingemfanyia mambo ya upuuzi kama hayo, na je, kwanini hawakumkataa asiongoze kufanya Mapinduzi kwasababu siyo Mzanzibar? Unafiki wa Wazanzibar haujaanza leo.

unapo piga ramli piga sehemu zote mbili kma utangangania sehemu moja itaonekana unatatizo ktk ramli yk. unaposema huenda alikataliwa kwa dini pia sema huenda alikataliwa kwa kabila.alafu soma vizuri okello alienda zanzibar kutafuta maisha hali kwao uganda ilikua ngumu kwake na movements za mageuzi huwakumba wengi walio katka eneo lile soma mageuzi ya libya jinsi watunisia walivyo shiriki leo ktk utawala libya hakuna hata mtunisia nawao walikataliwa kwa dini yao? wanyaruwanda na zaire leo wanyaruwanda hawamo ktk utawala zaire nawo wamekataliwa kwa dini yao? weka huru mawazo yako kanisa lisiyagandamize kiasi cha kukupa upofu.
 
Gen.Tito Okello Lutwa alizaliwa katika kijiji cha Nam Okora wilaya ya Kitgum wakati wa vita vya kwanza vya Dunia mwaka 1914,Kuhusu elimu yake mengi hayajulikani mengi hata hivyo alijiunga na Kings African Rifles(KAR)May 16,1940 kama ilivyokuwa kwa Idd-Amin naye alipigana vita vya Mau-Mau huko Kenya wakiwa upande wa waingereza mwaka 1957.
Gen.Tito Okello Lutwa alijiunga na Jeshi la Uganda na alipanda cheo kufikia Lieutenant mwaka 1962 na alifikia kuwa Colonel mwaka 1968.Wakati Amin anampindua Obote mwaka 1971 Gen.Tito Okello Lutwa alikimbilia Tanzania na alikaa sana Dar-es-salaam lakini pia alishawahi kukaa Nachingwea,Morogoro na Masange Tabora.
Mwaka 1978 wakati wa vita vya kumng`oa Idd Amin Gen Tito Okello Lutwa aliongoza kikosi maalumu(Special-Force)kikosi ambacho mimi mwenyewe nilikuwemo tulipigana bega kwa bega na waganda hao mpaka kung`oa Idd Amin madarakani mwaka 1979.
Mwaka huo huo 1979 baada ya Amin kuondolewa alikuwa sehemu ya Tume ya kijeshi,na baadaye 1980 alikuwa mkuu wa Majeshi wakati huo huo akiwa kwenye Tume ya kijeshi.Mwaka 1984 Alipandishwa cheo na kuwa Lieutenant General.
Gen.Tito Okello Lutwa alipitia magumu sana kipindi hicho maana kulikuwa na mambo mabaya sana jeshini Ukabila ulikuwa umetawala sana kulikuwa na vita kati ya makabila ya Acholi na Langi ilimuwia ngumu sana hata katika uteuzi wa maafisa wa jeshi mfano alimteua Bri.Smith Opon Acak toka kabila la Langi kuziba pengo la Maj.Gen.David Oyite-Ojok uteuzi huo ulipingwa sana na wanajeshi toka kabila la Acholi ambao wao walitaka mtu kutoka kabila lao Brig.Olara Okello ambaye alikuwa na uzoefu katika nafasi hiyo
Mwaka 1984 vita na waasi wa NRA alikuwa ameongeza mashambulizi yao kwa serikali hii pia iliezesha jeshi la taifa kugawanyika vipande viwili uapande mwingine ukiunga mkono Acholi na mwingine Langi kabila la Obote na Oyite Ojok.
Baada ya migogoro isiyokwisha ndani ya Jeshi la taifa UNLA na mapigano makali yaliyokuwa yakiongozwa na NRA chini ya Mseven Gen.Tito Okello aliamua kumpindua Rais Milton Obote July 25-27,1985 na Obote kukimbilia Kenya ka nia ya Barabara na kaenda uhamishoni Zambia ambako alifariki October 2005.
Baada ya mapinduzi hayo Gen.Tito Okello Lutwa alitangaza kuwa Uganda itatawaliwa na Baraza la kijeshi nay eye akiwemo kwa miezi 12 kabla ya Uchaguzi kufanyika.hata Gen.Okello alijaribu kuliunganisha jeshi ambalo tayari lilikua vipande vipande alijaribu kuunda serikali ya Mseto iliyojumlisha vyama vya Federal Democratic movement,Uganda National Rescue Front,Uganda Freedom Movement na NRA iliyokuwa inaongozwa na Yoweri Kaguta Mseven,Hata hivyo aligundua janja ya nyani aliyokuwa anataka kucheza Gen.Tito Okello na akakataa serikali hiyo na kuendelea na mapambano dhidi ya majeshi ya serikali UNLA
Yoweri Kaguta Mseven aliweka masharti magumu ili kukwamisha mazungumzo ya Amani yaliyokuwa yanaendelea huko Nairobi chini ya Rais Daniel Arap Moi wakati huo vikosi vyake vya NRA vilizidi kusonga mbele katika miji ya karibu na Kampala Barabara ya Masaka,Mubende,Mbarara na Katonga zote zilifungwa na kusababisha usalama katika maeneo yote kuwa hatarini Askari alianza uporaji na utekaji wa magari na vituo vya Mafuta,Maskini Gen.Okello hata hakumaliza kipindi alichoweka ili uchaguzi ufanyika na akapinduliwa January 26,1986 na alikimbilia uhamishoni hatimaye June 3,1996 alifariki akiwa na umri wa miaka 82,na mabaki ya mwili wake yalirudishwa Uganda na kuzikwa nyumbani huko wilaya ya Kitgum katika mazishi yake Rais Yoweri Kaguta Mseven alimtaja kuwa alikuwa mtu mkuu aliyelitumikia taifa lake na atakumbukwa kwa juhudi zake za kuleta Amani Uganda.
January 2010 wakati wa kumbukumbu ya vita vya Kagera alitunukiwa nishani ya Kagera National Medal Kwa heshima yake kwa kupigana vita kwenye miaka ya 1970-1979 dhidi ya Nduli Idd Amin.

Unanikumvisha. Mbali sana na jeshi la ukombozi
 
Back
Top Bottom