Sijui ni nini huwa kipo nyuma ya pazia kuhusu masoko kuungua hovyo. Hii sio Tanzania pekee bali África kwa ujumla!
Ushauri wangu ni kwamba kama unafanya biashara kubwa sokoni na hilo soko ni kongwe kuanzia miaka 5 kuwa makini sana, usiwekeze pesa zote hapo lolote litatokea muda wowote na utakosa cha kuanzia!
Mara nyingine ni bora kukubali kulipa kodi kubwa sehemu za kawaida kuliko kukimbilia sokoni kwenye bei kitonga!
Mwenye macho haambiwi tazama.