Sia sauti isiyochosha masikioni..

Sia sauti isiyochosha masikioni..

hassandilunga

Senior Member
Joined
Mar 17, 2020
Posts
146
Reaction score
149
Ni kama nilichelewa kumsikia huyu mwamke mwenye muziki mtaamu wazazi wake waliamuu kumpatia jina la Sia.

Mwanamuziki kutokea Australia alieifanya sauti yake kusikia nyema ndani ya Marekani na Dunia kwa ujumla yes ni Sia.

Mara ya kwanza namsikia ilikuwa katika moja ya nyimbo zake iliyoitwa "Chandelier" Aaah nilisikiliza kila ulipoisha nikaona kuna kitu cha zaidi nikaitaji kumsikia zaidi kumbe nlikuwa nimechelewa.

Nikakutana na Album nyingi kutoka katika mikono yake Sia Album kama 1000 Form of fear ya mwaka 2004,This is Acting,Everyday is Christmas n.k.

Masikion yangu yaliisikia sauti tamu kutoka kwa Sia sauti kweli kweli.

Nikasikiliza Chandelier,Cheap Thrills,Titanium,Elastic Heart(zote hizi zina watazamaji zaidi ya Billion 1)

Kuna The Greatest original na remix akiwa na Kendrick Lamar,Unstoppable,Big girls cry,A Live,Rainbow,Breath Me,Fire meet gasoline,Never give up,Soon well be found,Eye of Needle.

Zote zilitoka katika Album mbali mbali za Sia. Mziki wa Pop ulishamili katika kichwa cha Sia akatoa mashairi matamu na nyimbo za kuvutia..

Akajitofautisha na Adele,Elie Gouling,Rihanna n.k Video zake nyingi akamtumia American Dancer( Meddie Ziegler)

Mikono yake imekuwa na uwezo mkubwa wa kuandika mashaili kwa wasanii wengine wakubwa na nyimbo zikaenda zinakotakiwa kufika.

Sia Aliandika ngoma kama..

Diamond-Rihanna
Pretty Hurts-Beyonce
You lost me-Christian Aguilera.
Radioactive-Rita Ora
Let me love you-Neyo
Loved me back life-Celina Dion
Standing in the sun-Beyonce
Double Rainbow-Katty Perry
Acid Rain-Alexis Jordan
Try Everything-Shakira
Perfume-Britney Spears
Invicible-Kelly Clarkson
Expertease-JLo
My heart is open-Maroon 5

Zayn Malik yule Member wa zamani wa kundi la One Direction walipokutana kupika ngoma ya Dusk till dawn basi ikawa ngoma ya Zayn kuwahi kufanya vizuri zaidi mbali na Pillowtalk.(ngoma moja hatari sana🔥🔥)

Eminem aliitaji Chorus ishikwe na Sia kwenye Guts over fear unyama alioufanya humo Sia ni hatari..


Sia ndi mwanamziki wangu bora wa Pop

NB: Cha kushangaza sijawahi kumuona akishinda tuzo ya Grammy au kawahi kufanya hivyo????
 

Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    5.9 KB · Views: 7
Back
Top Bottom