Siafu na Sangara, yupi ni hatari zaidi

dr samg

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2012
Posts
292
Reaction score
163
Nimekuwa nikiwatafakari hawa wadudu wawili na sifa zao ambazo kidogo zinataka kufanana, Siafu mwenye tabia za kung'ata kwa kushtukiza maeneo nyeti ayajuayo yeye hata kama ulishaondoka eneo la tukio na sangara, mdudu mdogo mwenye meno makali kama ndege tai, yeye hung'ata pale atakapo fanikiwa kupafikia hasa miguuni, ni mdudu pekee anaeweza anza kumnyofoa steki mdudu mwenzie kabla hata hajafa (nyoka wanamfahamu vizuri sangara), wanajamii niambieni mnavyowajua hawa wadudu wawili.
 
hivi sangara ni mdudu??!?!?! mie najua samaki?!?!?
 
Sangara samaki au???

hivi sangara ni mdudu??!?!?! mie najua samaki?!?!?

Ni mdudu kwa umbo yupo kama siafu, ni super active kuliko siafu, nlishuhudia hospitali 2 bagamoyo zimefunga kabisa huduma ya mortual bcz ya sangala, ukilaza maiti mkija asubuhi mnakuta amesha ng'olewa macho
 
Mh,bas huyo sangara ni nouma
 
Ni mdudu kwa umbo yupo kama siafu, ni super active kuliko siafu, nlishuhudia hospitali 2 bagamoyo zimefunga kabisa huduma ya mortual bcz ya sangala, ukilaza maiti mkija asubuhi mnakuta amesha ng'olewa macho

Basi atakuwa anaitwa Sangala na sio Sangara
 
Siafu anajulikana huyo sangara umetumia lugha ya kwenye mtaje kiswahili tukusaidie
 
Siafu anajulikana huyo sangara umetumia lugha ya kwenye mtaje kiswahili tukusaidie

Kwa wenyeji wa kibaha, bagamoyo hata tanga ni jina la kawaida
 
Attachments

  • 1392093150650.jpg
    88.8 KB · Views: 130
Sangala ni wadudu wanapatikana maeneo ya kusini MWA Tanzania hasa vijijini nimekulia huko nawafahamu vizuri Sana nafikiri hamna afadhali maana siafu wanatembea wanaweza kutembelea chumbani hata saa nane ya usiku wakaanza kukung'ata, na sangala wakikung'ata wanaacha harufu hao wadudu hamna afadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…