Siamini kama kuongeza mishahara na motisha kunapunguza rushwa

Siamini kama kuongeza mishahara na motisha kunapunguza rushwa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Habari za huko?

Kuna hii kauli naisikia toka zamani Sana kwamba kuwaongezea watumishi mishahara au motisha Basi kunapunguza tamaa za wao kufanya ufisadi.

Hebu tuchukulie kwa mfano kada Kama za udkatari au uaskari let's say mfanyakazi analipwa Million moja kwa mwezi na kila siku ana force apate rushwa ya 30000 yaani ameshazoea tayari, je ni kweli kwamba ukimlipa millioni mbili kwa mwezi ataziacha zile pesa anazopata kwa rushwa.

Hili si kweli nachojua Mimi kipato cha mtu kikiongezeka Basi na matumizi yanaongezeka maradufu ikumbukwe hakuna mtu anashiba pesa hata Mimi japo Sina njaa Ila sijaridhika Bado na kiwango nachopata.

Hivyo namalizia kwa kusema hii kauli haina ukweli wowote Kama mnawapa watu motisha wapeni kama nyongeza wapeni ili kukabiliana na maisha lakini sio kusema itapunguza rushwa na vitendo vya kifisadi haipunguzi hata robo.

Kuongeza maslahi ya mfanyakazi hakuna uhusiano na kuzuia rushwa Kama NI NJIA nyingine Basi itafutwe kukabiliana na rushwa.
 
Ingekuwa matumizi yanabaki pale pale labda ingewezekana! Leo hii, ukiongezewa tu kipato, unabadili BAR, GARI, SEHEMU ZA STAREHE, HATA MARAFIKI.
 
Ingekuwa matumizi yanabaki pale pale labda ingewezekana..! Leo hii, ukiongezewa tu kipato, unabadili BAR, GARI, SEHEMU ZA STAREHE, HATA MARAFIKI
Yeah na ndo mademu na madeni pia yanaongezeka so itabidi upambanie Tena kombe kuzipata nyingine.kuna kipindi magufuli alikwenda kutembelea sijui NI mizani ama bandarini..eti akaamrisha wale wafanyakazi wanaokaa usiku na mchana waangaliwe maslahi Yao ili wasipate tamaa za kuomba rushwa.nikabaki najiuliza Ina maana Rais hajui watu huwa hawashibi pesa.yaani hajui mtu hata Kama NI billionaire Ila mchongo wa 10000 ukitokea hawez kuuacha.
 
Nadhani inasaidia kupunguza vitendo vya rushwa, kwa mfano mtu anatoka nyumbani kwenda kazini ameondoka nyumbani ameacha hakuna hata unga wa kupika mchana ataacha kuchukua rushwa. Lkn ukiwa katika hali nzuri kiasi kimaisha mshahara wa kutosha inapunguza tamaa na inasaidia kusimamia misingi ya kazi yako.
 
Back
Top Bottom