Mrekebishaji
Senior Member
- Mar 19, 2009
- 168
- 63
Ndugu watanzania,
Leo naandika huku nikiangalia hali ya afya zetu, watoto wetu na ndugu zetu wengine ambavyo hazina uhakika wa usalama.
Leo hii, mtoto akiugua kwa Dar, daktari mwenye uwezo mzuri wa kumtibu mtoto ni mmoja tu, Dr. Masawe ambaye yupo Morocco. Hata hivyo, huyu doctor kwa wanayemfahamu, kila siku kwa siku anazotibu huchukua watu kumi tu na lili umpate unahitaji ufike pale saa kumi usiku, mimi leo nimefika saa kumi na moja nimepata namba tano baada ya kumkosa kama mara nne hivi na nimekwenda kwa wengine bado sijapata huduma nzuri. Utasikia ma-doctor wa watoto ni wengi lakini, utaenda hapa na mtoto, utaambiwa hili, utakwenda pengine utaambiwa lingine. Huku watasema malaria, huku watasema si kweli, hizi dawa ulizopewa tupa.
Tutafakari yafuatayo;
1. Hivi wizara ya afya na ustawi wa jamii,hawawezi kufanya uchunguzi wa kubaini madaktari wasiofaa maana ni wagonjwa wengi wanapewa dawa zisizofaa.
2. Kutokaka na siasa zetu, watu wengi wenye uwezo wamekimbia kusoma u-dokta kutokana na maslahi duni ya fani hiyo na pia mfumo mbaya wa kuwapata ma-doctor. Angalia jinsi wanafunzi wa chuo cha tiba muhimbili wanavyolalamika namna shule yao inavyoendeshwa.
Siasa, inaua kila kitu.
Kweli maisha yetu yapo hatarini.
Yote haya yanatupelekea kuona kwamba kwa sasa ni kweli tunahitaji chama makini ambacho kitaiangalia nchi kwa jicho la tofauti. Chadema wanaonyesha nia hiyo.